Je ni sahihi kwa watu kumzonga na kumzomea mwanamke kwa mavazi yake

tatizo lipo hapo Mertyina: what to wear and where to wear!

Kijijini kwetu siwezi kuvaa leggings na top dress, watanishangaa na kunilaani lakini daslamu wala hakuna anayekushangaa.

Yeye akawavalie wanyalu lesi lesi hizo alifikiri nini?.

Wakati mwingine tunajidhalilisha wenyewe tu.

ina maana iringa mjini kipi wasichokijua mpaka wamghasi dada yetu?
 
hapana ila wewe apo umeona kinini cha kuwafanya wanaume wale wamletee zengwe?yupo uchi?au kila saa tuvae kama tunaenda kanisani?
Ni sawa na ufungue kibanda cha kunyolea nywele sehemu wanayoishi watu wenye vipara unategemea nini????
 
Kina dada hamna mpango kabisa.Mavazi yana mahali pake,vazi la kulalia mwavaa barabarani.Utakuta dada kavaa sketi fupi,anapanda daladala,kasheshe akikaa katika kiti,mapaja nje!Utakuta mwenyewe anahangaika kuyafunika,ulivalia nini?
mimi navaaga nikikaa nimekaa sihangaiki wewe utahangaika mwenyewe.
 
kwani hapo unaona maumbile ya ndani?mbona wazungu wanavaa vikaptula chupi flani unawakuta mtaani wakijiacha sembuse hii
mshauri nae ajichubue ngozi nyeusi awe kama mzungu na awe anatembea amevaa lichupi
 
Uhuru wa Mwanamke si kujiweka uchi au nusu uchi.

"O children of Adam! Surely we have bestowed upon you a garment to cover your shame, as well as to be an adornment to you, and the garment of piety is the best." (al-A'raf, 26)

Qur'an: Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamngu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu mpate kukumbuka.

[FONT=Arial, Helvetica]Bible: I also want women to dress modestly, with decency and propriety, not with braided hair or gold or pearls or expensive clothes, but with good deeds, appropriate for women who profess to worship God.[/FONT][FONT=Arial, Helvetica] (NIV, 1 Timothy 2:9-10)[/FONT]
 
Back
Top Bottom