Wakaguzi wa tiketi ndani ya treni TRC fanyeni kazi kwa uaminifu

mandwa

JF-Expert Member
Aug 13, 2013
1,438
326
Habari,

Hivi karibuni nimepanda treni ya TRC toka DSM to Shinyanga daraja la 3 nilichokutana nacho ndani ya treni inasikitisha rushwa imetawala Sana yaani wakaguzi wa treni kwa jina lingine Titii wanalazimisha pesa kwa abiria pasipo na msingi.

Mfano wale abiria wanaopanda gari njiani hawapewi tiketi wakijaribu kuomba tiketi wanajibiwa kwa ukali hadi wanaogopa kuendelea kudai tiketi Jambo kubwa lililonishangaza wakati narudi na treni hiyo hiyo ordinary tokea Shinyanga to DSM tukiwa maeneo ya morogoro mkaguzi wa tiketi au Titii anapita kwa kila abilia na kuchukua tiketi kwa madai ni Mali ya ofisi ikabidi nishangae toka lini tiketi zikarudishwa ofisini?

Mimi Kama kawaida yangu huwaga sipo nyumba katika kutaka kujua Mambo nikamuuliza Titii kwanini unachukua tiketi zetu akasema zinarudi ofisini Kama unaitaka tiketi yako inabidi uandike barua ya kuomba kurudishiwa tiketi aisee nilibaki nimekaa kimyaa maana sikumuelewa yule mkaguzi akisaidiwa na polisi ambaye huwa anakua naye kwenye ukaguzi.

Kwa kifupi abiria wanazulumiwa haki zao maana wanalipa nauli hawapewi tiketi pesa zinaenda mifukoni mwa matitii wachache wasio waaminifu serikali inakosa mapato ya kutosha.

Na haya wanafanya kwa wale abiria wasiojitambua wasiojua kuhoji wakikuona unajitambua wanakuogopa hawakuletei usumbufu.
Ombi kwa wahusika kuondoa wafanyakazi wa Aina hii ndani ya treni TRC
 
Back
Top Bottom