Wajuzi wa Lugha, Nisaidieni Kuhusu jina Middle

Oltung'anyi

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
284
196
Wadau, huwa ninapata shida kwenye matamshi ya jina linaloandikwa Middle.

Mwenye jina hulitamka "Middle" lakini linavyoandikwa, kwa uwepo wa d mbili, naona kama linakuwa so jina katika lugha ya Kiswahili. Hivyo, kwa namna linavyoandikwa, pengine lingetamkwa Mido.

Sijui wadau mnaonaje. Yawezekana mwenye jina akasoma Uzi huu pia, anaweza tu kutolea ufafanuzi, kwa mini jina linasomeka/tamkwa Midle badala ya Mido.

Binafsi ningependekeza kama ni jina la Kiswahili, liandikwe Midle na lisomeke hivyo hivyo.

Kama ni jina la kimagharibi, basi liendelee kuandikwa hivyo hivyo, Middle na lisomeke na kutamkwa Mido.
 
Ungetaja hata mtu mmoja anaetumia hilo jina labda ningejaribu kujibu mkuu
Mkuu, mmoja wa watu wenye jina hili na anayelitamka Midle wakati linaandikwa Middle ni mtangazaji wa radio One/ ITV Farhia. Ukifuatilia wakati anasoma habari ITV, jina lake linaandikwa Middle lakini yeye analitamka Midle. Ninaona hapa kuna mchanganyiko wa lugha.
 
Sawa
Hilo jina linatamkwa midle lakini kwa kuikaza hiyo d iwe kama dd ndio maana anaiandika middle
 
Ukisikia taarifa ya habar inasema middle east, Wapalestina wamewashambulia Waisrael we unaelewaje hapo?
 
Sasa mtu ataikaziaje DD kwenye 'Middle'?.. Sawa na kutamka AIREEN, AIRYN na IRENE utaweza vipi kuzitofautisha kwenye matamshi zaidi ya kwenye kuandika!.
Tofauti zingine zibaki kwenye kuandika lakini kwenye matamshi ni kazi kuzionyesha!.
 
Sawa
Hilo jina linatamkwa midle lakini kwa kuikaza hiyo d iwe kama dd ndio maana anaiandika middle
Namba linavyoandikwa na namna linavyotamkwa ndipo palipo na shida. Linaandikwa kiingereza, linatamkwa kwa kiswahili. Namna linavyoandikwa(Middle) ilitarajiwa lisomeke Mido, ila linatamkwa Midle.
 
Hapana usilisome kiingereza ni jina la kisomali middle (midd le) na sio mido
 
Sasa mtu ataikaziaje DD kwenye 'Middle'?.. Sawa na kutamka AIREEN, AIRYN na IRENE utaweza vipi kuzitofautisha kwenye matamshi zaidi ya kwenye kuandika!.
Tofauti zingine zibaki kwenye kuandika lakini kwenye matamshi ni kazi kuzionyesha!.
Kweli kabisa na ni ngumu kuielezea kwa kuiandika.
 
Mkuu, mmoja wa watu wenye jina hili na anayelitamka Midle wakati linaandikwa Middle ni mtangazaji wa radio One/ ITV Farhia. Ukifuatilia wakati anasoma habari ITV, jina lake linaandikwa Middle lakini yeye analitamka Midle. Ninaona hapa kuna mchanganyiko wa lugha.
Yeye mwenyewe huwa analitamka kama lilivyoandikwa, yaani ukimsikiliza anavyolitamka ni MIDDLE, yaani ulisome kama lilivyoandikwa. Ndo Kiswahili chenyewe
 
Ila, hakuna jina katika Kiswahili linaandikwa hivi. Ila, kama ni la kiarabu, inaeleweka. Hakuna shida.
 
Back
Top Bottom