Wajuzi naombeni ushauri kuhusu vyakula navyotakiwa kula katika hali hii ya ujauzito wa wiki 23

Pisi kali

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,215
2,418
Hello wanajf,

Bado siku 1/2 hivi tukacheze duduke

Naombeni mnijuze ni sawa? Mimi ni mjamzito wa week 23 sasa ratiba yangu ya kula kila siku

Asubuhi mayai mawili nachemsha na viazi vitamu viwili na maziwa nusu lita, saa2 asubuhi

Saa4 lazima ninywe uji (unga nimeutengeneza mwenyewe

Mchana lazima ugali mrenda (bamia na nyanya Chung tu) na samaki wale wadogo wa mafungu

Saa12 nanasi zima au tikiti peke yangu, Au machungwa mawili

Saa2 usiku magimbi naweka nazi

Hiyo ni ratiba yangu ya kila siku ni LAZIMA, nikibadilisha labda nikipata mgeni/wageni ila nikiwa mwenyewe ndio ratiba yangu

Sasa ni sawa kwa mama k jamani? Au kuna vitu namnyima mtoto jamani? Nimejitahidi mboga zingine labda maharage tu na kuku basi, wali siupendi dagaa ndio sili kabisaa

Saa4 usiku nameza FEFO

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu umejitahidi sana mimi ninakuongezea vyakula muhimu vyengine kuvila ili upate kuongeza madini ya chuma kwa faida yako wewe na mtoto aliyeko tumboni.Kwanza ikifika wiki 28 uwe unakula kila siku Tende 6 mpaka wakati wa kujifunguwa utajifunguwa pasipo na kufanyiwa operesheni ukifuata huo ushauri wangu.

Vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito anastahili kula

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini. Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku. Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora. iliweza kukundalia vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula 1. Jamii

Kunde Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini. Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya,Peas,Karanga, Alfa alfa,Mikunde, maharage.

2.Mayai Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi ya magonjwa mbali mbali.

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi. Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli, Ni muhimu kwa damu yenye afya,

kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.
4. Viazi tamu Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto,ngozi na mifupa

5. Nyama ya ,kuku au ngombe huwa na protini mingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

6. Nafaka na vyakula vya Wanga Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni.Vyakula hivi ni kama mahindi,mtama ,mihogo,vyakula vya ngano kama mkate n.k.

7.Avocado Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Avocado inasaidia katika ukuaji wa ubongo,ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.

8 .Mboga za majani Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha. Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.

9. Mafuta ya samaki Mafuta ya maini ya samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.

10.Maji Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)

VYAKULA VYA MJA MZITO.jpg
 
Asante sana

Hiyo ya tende nimesikia pia, kuhusu mayai wananitisha kua mtoto atakua mkubwa nitashindwa kupush kua niache kula mayai, mboga za majani nakula ila kwa wiki mara mbili.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mbona hujamtaja mwenye mzigo au ndo kenda chimbo ? Pole sana next time awepo kuchochea njia ifunguke vyema. Si unajua tena?
 
Mbona hujamtaja mwenye mzigo au ndo kenda chimbo ? Pole sana next time awepo kuchochea njia ifunguke vyema. Si unajua tena?

Kila mwisho wa mwezi anakuja.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hongera sana Pisi kali! Niamini mimi, hakuna furaha ya mwanamke yeyote hapa duniani inayoizidi ile ya kuwa na mtoto katika wakati na mazingira sahihi.

Jitahidi kula MLO KAMILI wakati wote wa ujauzito na siyo kung'ang'ania vile vyakula unavyo vipenda tu! ili tupate mjukuu mzima na mwenye afya tele. Nb:Ujitahidi pia kupunguza kumdekea jamaa! maana wanawake mlio wengi, wakati wa ujauzito mnadeka sana!
 
Hahahahaha simdekei sana ila akiniudhi tu namnunia siku nzima sipokei wala kujibu msg zake

Najitahidi ila nikila vitu vingine Naona hata sijashiba roho hairiziki

Kweli ni raha sana kua na mtoto hapa tu bado sijamuona face to face ila nasikia raha haswa akipiga mateke naenjoy sana na baba k akimshika tu lazima aruke ruke

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Asante sana

Hiyo ya tende nimesikia pia, kuhusu mayai wananitisha kua mtoto atakua mkubwa nitashindwa kupush kua niache kula mayai, mboga za majani nakula ila kwa wiki mara mbili.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kula Mayai na ikiwezekana mboga za majani jaribu kuongeza kwa wiki kula mara 4 badala ya mara ya 2 kwa wiki. Kwani mboga za majani ni muhimu sana kwako kuliko vyakula vyote unavyo kula. Mboga za majani zinakuongeza kinga ya mwili dhidi ya maradhi na kukuongezea damu mwilini mwako na mboga zamaji zina amdini ya chuma aka iron ni muhimu san kwa mama mjamzito tumia sana mboga za majaji kwa wingi kuliko kitu chochote kile. Ukiwa unakula tende zitakusaidia kupata kuzaa kwa wepesi sana pasipo na kufanyiwa operesheni.

DR SEBI - WHAT ABOUT PREGNANT WOMEN

Umri wako ni miaka mingapi isije kuwa nashauri mtoto mdogo. Ngojea ukikua utayajua.Wawezakumfanya hata siku moja tu kabla uchungu haujaanza
Unajifanya mjuaji.
Kwanza mwanamke mjamzito anakua hana hisia za mapenzi. Jumlisha na ule ukubwa wa tumbo. Hata wewe mwanaume huwezi enjoy.
 
Hello wanajf,

Bado siku 1/2 hivi tukacheze duduke

Naombeni mnijuze ni sawa? Mimi ni mjamzito wa week 23 sasa ratiba yangu ya kula kila siku...
Huko sio kula bali ni KUFUKIA....Ukishajifungua kwa Mwendo huo lazima umpite mwili ASHA BOKO.
 
Hello wanajf,

Bado siku 1/2 hivi tukacheze duduke

Naombeni mnijuze ni sawa? Mimi ni mjamzito wa week 23 sasa ratiba yangu ya kula kila siku

Asubuhi mayai mawili nachemsha na viazi vitamu viwili na maziwa nusu lita, saa2 asubuhi

Saa4 lazima ninywe uji (unga nimeutengeneza mwenyewe

Mchana lazima ugali mrenda (bamia na nyanya Chung tu) na samaki wale wadogo wa mafungu

Saa12 nanasi zima au tikiti peke yangu, Au machungwa mawili

Saa2 usiku magimbi naweka nazi

Hiyo ni ratiba yangu ya kila siku ni LAZIMA, nikibadilisha labda nikipata mgeni/wageni ila nikiwa mwenyewe ndio ratiba yangu

Sasa ni sawa kwa mama k jamani? Au kuna vitu namnyima mtoto jamani? Nimejitahidi mboga zingine labda maharage tu na kuku basi, wali siupendi dagaa ndio sili kabisaa

Saa4 usiku nameza FEFO

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwani hiyo mimba iliingiajeinngiaje Pisi kali na je umezaajezaaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom