Wajuzi na watumiaji wa mashine za kutotolesha vifaranga (incubators) tubadilishane ujuzi

kahogo

Member
Sep 20, 2015
21
36
Habari zenu wajasiriamali na wahangaikaji wenzangu nakuiteni kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika utumiaji wa mashine za utotoleshaji vifaranga kwa matokeo mazuri nini na kipi mtumiaji wa incubator anaweza kukifanya na kipi anatakiwa kua makini kutokifanya ili kupata asilimia za kiwango cha juu za kutotolesha mayai karibuni sana.
 
Habari zenu wajasiriamali na wahangaikaji wenzangu . Habari ni nzuri ndugu, mimi ni mjasiriamali kwenye eneo hilo ila sio mhangaikaji. Nafanya nachopaswa kufanywa sihangaiki.
nitaongelea maeneo mawili;
eneo la kwanza ni mayai kuwa na mbegu. Ni tatizo kubwa maana wengi wana mashine ila sio wengi wanaweza kuzalisha au kupata mayai ya kutosha yenye mbegu. kwa uzoefu wangu, nimewahi kununua mayai toka kwa wazalishaji wengine na kupata hasara kubwa kutokana na mayai kutokuwa na mbegu. hivyo nikaanza uzalishaji wa mayai yenye mbegu ambayo naweza kufwatilia kwa karibu ili kupata matokeo sahihi. hiki ni kilio cha waanguaji wengi, wapo wenye mashine kubwa sana ambazo hawajawahi kuwasha kabisa kutokana na kukusa mayai ya uhakika yenye mbegu mabayo yatazalisha vifaranga bora.

eneo la pili ni chanzo cha nishati cha uhakika. Zipo aina tofauti za mashine ambazo hutumia aina tofauti ya nishati. zipo za kutumia umeme- ambazo ni nyingi zaidi, umeme wa jua, mafuta ya taa, gesi, na vyanzo vingine. Ni vizuri kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha nishati au chanzo cha uhakika cha nishati. hivi karibuni wapo wajasiriamali wa kitanzania wameleta mashine zinazotumia Gesi ya kupikia ambazo zinafanya vizuri sana. nyingi zinazotumia umeme wameweza kuweka majenerator au mfumo wa kuhifadhi umeme inapotokea dharura.
 
Back
Top Bottom