Wajumbe wote wa Bodi ya SABC Waachia Ngazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe wote wa Bodi ya SABC Waachia Ngazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akili, Jun 27, 2009.

 1. a

  akili Member

  #1
  Jun 27, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajumbe wa Bodi, Mameneja na Watangazaji TBC ya Afrika Kusini wajing'atua wenyewe.....
  ASILIMIA kubwa ya wajumbe wa bodi na Wafanyakazi wa South Africa Broadcasting Corporation [SABC] wamelazimika kuacha kazi kwa kuruhusu kutumiwa na wanasiasa badala ya kufanya kazi kama chombo huru.

  Wengi wao walikuwa wakimuunga mkono Thabo Mbeki ama wale waliokimbia ANC na kujiunga na vyama vingine vya Kisiasa au kuanzishwa kwa kile cha the Congress of the People.

  Tumiwa yao iliwaacha kwenye tuta baada ya Zuma sio tu kuwa Mwenyekiti wa ANC bali kuchaguliwa kama Rais wa nchi hiyo. Alichokifanya Zuma ni kutojishughulisha nao na kumwambia Waziri wake wa Fedha awachangamshe kidogo kwa kuwasahau kimishahara na kimasilahi.

  Prof. Guy Burger, Gwiji la Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Rhodes University anasema haya yote yanatokana na ushabiki wa kisiasa ndani ya chombo cha kiserikali ambacho kilikuwa hakistahili kusimamia upande wowote.

  Hapa Tanzania bado Vyombo vya Habari vya serikali vinatumika kama vile ni vyombo vya chama tawala.

  Wakati huohuo, ninaitambua RASMI Televisheni fulani ya Tanzania inayoonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuonesha KIPINDI CHA BUNGE kuanzia manane ya usiku hadi alfajiri kumi na mbili na nusu.

  Lakini nina maswali kadhaa ninayojiuliza hivi ni kwa sababu ipi kati ya hizi hapa chini:
  . ukata wa kununua vipindi vizuri ndio unaosababisha hili,
  . mwenye TV ana mapenzi kweli na nchi na bunge lake,
  . kipindi kinaoneshwa wakati huo kwa sababu wanajua hakuna anayekitazama ila anayewania kuwa mbunge hapo baadaye,
  . kwa kuwa ni mkanda uliorekodiwa bure basi unawapa nafasi wafanyakazi wake kulala,
  . kwamba jamaa bado ana mawazo ya kizamani kudhani maendeleo yetu yatatoka juu, yaani, kwa rais au wabunge,
  . ushahidi tosha wa kwamba baadhi ya TV nchini Tanzania zinaweza kufungwa na mwananchi asione kama kakosa kitu.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wajumbe wote au asilimia kubwa?
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hivi cyrill ramaphosa yuko wapi?
   
 4. Amosam

  Amosam Senior Member

  #4
  Jun 27, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kipi unachoshangaa wakati wajua wazi mmiliki wake alishawahi kuwa waziri wa TZ?Yeye yupo bungeni unafikiri watu wake watamwonaje?Wacha awape shida watu wa kanda ya ziwa kukesha macho kumwangalia mhe.akiwa bungeni.
   
Loading...