Wajumbe wa nyumba kumi wa CCM balaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe wa nyumba kumi wa CCM balaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakati, Aug 1, 2012.

 1. Kakati

  Kakati Senior Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamiiforums,

  Hivi mtu akitaka kutoa maoni yake kwa tume ya katiba online atatakiwa afanyeje? Tume ya Warioba ina website kwa ajili hiyo?

  Mimi kuna jambo linanipa shida sana. Leo mtu kaenda kujiandikisha ili apate kitambulisho cha taifa. Yule mwandishi akamwambia apeleke barua ya mjumbe wake wa nyumba kumi bila hivyo hawezi kumwandika hata kama ana vitambulisho gani! Ugonvi ulikuwa mkubwa.

  Mimi natafuta njia ya kufikisha pendekezo la kumaliza tatizo hilo kwa njia ya katiba. Ninapendekeza katika katiba mpya kuwekwe kifungu kinachozuia watu kunyimwa huduma fulani hadi watambulishwe na kiongozi aliyepatika kutoka chama fulani. Hawa watu wanaoitwa wajumbe si viongozi wa kuchaguliwa na wananchi. Kiongozi wa chini kabisa kiutawala wa nchi hii ni Mwenyekiti wa Mtaa au Kitongoji (mijini/vijijini).

  Kama tukitaka wajumbe wawe ni chombo cha kuwatambua watu kwa karibu zaidi badala ya viongozi wa mitaa au vijiji na vitongoji, basi tuweke utaratibu wa watu hawa kuchaguliwa na watu wa vyama vyote ndani ya eneo husika kama inavyofanyika kwa wenyeviti wa mitaa.

  Najua CCM wanafurahia hali ya kutokuwa na kiongozi rasmi wa serikali katika ngazi ndogo badala yake wanaweka kiongozi wa CCM na wanataka watu wanaendelea na utamaduni wa zamani wa kutumia balozi/mjumbe wa shina ambaye hapo zamani alikuwa na kofia ya chama na serikali. Wanajaribu kuwafanya waTanzania wasitofautishe kati ya CCM na Serikali lakini. Hii haitusaidii na kuna wakati/mahali inaleta vurugu.

  Tuondoe habari ya mjumbe au tuifanye ya kuchaguliwa na watu wote. Mwenye mawao tofauti au anayejua jinsi gani naweza kuwasilisha hoja hii anisaidie.
   
 2. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kuna vyama 19 vya siasa, na kila chama kwa utaratibu wake, kina mjumbe wake wa nyumba 10/10. Je ukiulizwa umtaje wa chama gani?
   
 3. lynxeffect22

  lynxeffect22 JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 625
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
 4. Kakati

  Kakati Senior Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante kwa link hii.
   
 5. Kakati

  Kakati Senior Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni kweli vyama vipo vingi lakini ni kweli kwamba bado watu wanahangaishwa kwa kutakiwa wapate utambulisho wa wajumbe wa nyumba kumi wa CCM!
   
 6. M

  Mzee Kabwanga Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama kuna jambo hilo afadhali kusiwe na vyama vingi turudi kwenye chama kimoja au ni janja ya serikali kuweka kitu hicho. Inatakiwa ipingwe kabla ya kuandikishwa mikoani suala la uraia siyo la kuleta masuala ya chama.
   
 7. Kakati

  Kakati Senior Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Lakini kwa kweli hali ndiyo hiyo. Yaani hapo kwenye vituo vya kuandikisha waandikishaji wameambiwa bila ruaa ya mjumbe hakuna kuandikishwa. Kuna siku jambo hili litaleta shida. Nasikia hata Chadema, CUF nk wameanza kuchagua wajumbe wao wa mashina. Mimi nasema hivi: kama hawa ni wa lazima basi wachaguliwe na wananchi wote eneo husika bila kujali vyama, sawa na viongozi wa mitaa.
   
Loading...