Kitia
JF-Expert Member
- Dec 2, 2006
- 418
- 77
Wakati wa chama kimoja, CCM iliweka utaratibu wa kuwajuimuisha na kuwashirikisha wananchi katika ngazi zote, kuanzia juu mpaka chini kabisa. Utaratibu huo ulileta kuwepo kwa Wajumbe wa Nyumba Kumi, ambapö mjumbe alikuwa na nyumba zake kumi katika mtaa ambapo aliwafahamu watu wote waliokuwa wanaishi katika nyumba hizo. Nakumbuka wakati ule ambapo bidhaa mbali mbali zilikuwa adimu, k.m. sukari, unga, mchele n.k kila nyumba (household) ilibidi kujiandikisha kwa mjumbe na kupata kadi ya ration ya kununulia chakula. Mfumo wa nyumba Kumi ulisaidia katika kulinda usalama wa raia, ambapo hata ulinzi wa sungusungu ulikuwa uanafanyika katika misingi ya nyumba kumi. Kwa kila mtoto aliyezaliwa ilibidi kwanza aandikishwe kwa mjumbe. Hata vyeti vya kuzaliwa kulikuwa na nafasi ya kujaza jina la mjumbe. Pale mtu alipouifa pia ilibidi pia mjumbe awe na taarifa . Mgeni yoyote akija, ilikuwa lazima akatambulishwe kwa mjumbe, anatoka wapi na atakaa muda gani.
Faida ya kuwa na Wajumbe wa Nyumba Kumi ni nyingi. Ukusanyaji wa taarifa na data ulikuwa ni rahisi. Usalama wa raia ulikuwa wa kuamminika, na zaidi ya hapo jamii ilikuwa imefungamana na kufahamiana vizuri. Mfumo huu ungetumiwa kwa wakati huu ungelirahisishia taifa mambo mengi. Kwa mfano hesabu ya watu (census) ingefanyika kwa urahisi zaidi. Pili usalama wa raia ungekuwa imara zaidi na ujambazi kupungua. Hizo ni faida chache tu ambazo nimeziweka hapa, wengine mnaweza kuongezea.
Natoa ushauri kuwa ingekuwa vyema Wajumbe wa Nyumba Kumi warudishwe, sio chini ya chama, bali chini ya Serikali za mitaa. Faida zake ni nyingi kuloko hasara. Wana JF mnasemaje?