Wajumbe Wa NEC Kutoka Wilayani: Ni Usanii? (Tafakari Yangu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe Wa NEC Kutoka Wilayani: Ni Usanii? (Tafakari Yangu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Apr 13, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Inasemekana kwamba wajumbe wengi wa NEC ya sasa wanahongeka kirahisi kiasi kwamba mzee wa Kaya ameamua kuwatema 'wahongaji' hodari; na hapohapo ikapendekezwa kwamba wajumbe wa NEC sasa watatoka mikoani ili kudhibiti hiyo hali na kufanya kile kilichoelezwa na Wilson Mukama kuwa 'chama kuwa karibu zaidi na wananchi'.

  Hilo la chama kuwa karibu na sisi (wananchi) tuliache; maana mtu aliyekaa mbali na wewe kwa miaka 50 leo akasema anataka kukaa na wewe karibu, huo ni unafiki tu. Isipokuwa kama una matatizo ya kufikiri, huwezi kukubaliana na hoja ya CCM kujisogeza karibu na wananchi wakati huu. Ni ghilba.

  Labda hili la kwanza: kuachana na wachumia tumbo wa mikoani na kuleta wapya kutoka wilayani. Haya ni maigizo. Sheria za nchi ziko wazi, na hata Kambarage alisema Mtanzania yeyote anaruhusiwa kuishi popote Tanzania hii ali mradi havunji sheria za nchi.

  Wajumbe wa sasa wa NEC (wa kutoka mikoani) wanao uhuru wa kuishi popote pia. Kama leo CCM wanainuka na kusema sasa ni muda wa kuachana na watu wa ngazi ya mkoa, mimi hainiingii akilini. Ni watu walewale kwa mtindo uleule watajivua gamba la ngazi ya mkoa na kujivika gamba la ngazi ya wilaya na ndiyo hao hao watakaoendelea kuwa wajumbe wa NEC kwa mbinu ileile ya kuhonga wapiga kura.

  Tusubiri tuone hao wajumbe wapya wa Wilaya.

  kama yupo wana-ccm yeyote hapa jamvini anaye elewa vema dhana hii ya wajumbe wa nec kutoka ngazi ya wilaya badala ya mkoa, atufafanulie zaidi.
   
 2. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  As long as hii issue imeanzia kwa Jakaya basi ujue ina kasoro kubwa tu.
  Mimi naishi Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tarafa Ilemela, Kata ya Nyamanoro, Mtaa wa .....

  Sipati mantiki unaweza vipi kumpata mtu kutoka eneo fulani, ambalo haliko mkoa fulani, Nadhani hii
  ni assignment ya kwanza kwa Mkama na Nape kuzielezea kwa ufasaha kauli/hoja za Bosi wao.
   
Loading...