Wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, mchagueni Mama Samia kuwa mwenyekiti wa CCM na Ashraf Sadru Kiobya kuwa mjumbe wa NEC

View attachment 1768574
Ndugu Ashraf Sadru Kiobya


Ndugu wajumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa.
Poleni kwa Safari na Majukumu mazito ya ujenzi wa Taifa na chama

Naomba kuchukua nafasi hii kuwaombeni kwa unyenyekevu mkubwa mumchague Mama yetu, Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa CCM.

Mama Samia ni kiongozi makini, Mwenye utu, anachukia ufisadi na ana vision kubwa ya wapi anataka kuipelea nchi hii.

Kikubwa zaidi ni mtu mwenye sense ya Haki. Kwa hiyo naamini akuwa Mwenyekiti ataweza kuwa na nyenzo zote za kichama na serikali za kuiongoza nchi yetu vizuri.

Pia ndugu Wajumbe, Naomba Mumchague Ndugu Ashraf Sadru Kiobya kuwa mjumbe wa NEC.

Ndugu Ashraf anagombea nafasi hiyo kupitia viti 2 vya bara.

Ashraf ni kijana aliyepikwa na chama akapikika na anakipenda chama, ni kijana mpenda mashirikiano (team worker), ana busara na hekima, ni kijana mpatanishi, mchapakazi na mzalendo kwelikweli wa nchi hii.

Kwa Taaluma yeye ni mwalimu(amefuata nyayo za viongozi wetu Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi na Hayati John Joseph Pombe Magufuli ambao kitaaluma nao walikuwa walimu) na pia ndugu Ashraf Sadru Kiobya ana kisomo kizuri (Masters degree) aliyoipata katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Nawambeni ndugu Wajumbe mtusaidie kutuletea kijana huyu ili nyie pamoja naye mtusaidie kwenye kujenga CCM Imara ambayo itamsaidia mama Samia Suluhu Hassan kuiletea nchi yetu mafanikio makubwa.

Historia fupi ya Asili ya Ndugu Ashraf
Familia ya Kiobya ya Ndugu Ashraf ni familia yenye mzizi mrefu katika historia ya nchi hii, yeye ni Kilembwe wa Hayati Kiobya Kya Mihigo aliyekuwa Mtawala(Governor) wa nchi ya Karagwe na Kihanja chini ya Omukama Kahigi wa huko Kagera wakati wa Utawala wa Muingereza.

Ashiraf ni Kitukuu cha Mustafa Kiobya aliyekuwa Mwami wa Ibwera na Hakimu mkuu wa eneo hilo wakati wa Mjerumani mpaka mwanzoni mwa miaka ya awali ya Uhuru, Huyu Mustafa Kiobya ni miongoni mwa wazee waliompokea Mwalimu Nyerere huko Bukoba mwishoni mwa miaka ya Sitini katika harakati zake za Kushawishi wananchi kuwa Wanaweza kumng'oa mkoloni na kuleta uhuru Tanganyika.

Pia ni mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya CCM bukoba vijijini Ndugu Sadru Athumani Kiobya.

Ndugu wajumbe, simuombii Ashraf kura kwa sababu ya eti kwa kuwa ukoo wake una asili ya uongozi basi naye lazima awe, La hasha nimeweka haya ili mjue kijana huyu historia ya asili ya familia yake ndani ya Tanzania na ndani ya chama haina chembe ya shaka.

Kwa hiyo ndugu wajumbe, Kijana huyu ni kijana wenu, familia yake inaeleweka, namleta kwenu ili Mumpe kura zote za Ndiyo ili awe Mjumbe wa NEC
Huyo kijana amaekaa kwenye chama muda gani?Kata yake ya Ibwera ndo inaongoza kwa majanga ya kukosa maji safi na salama.Vijiji kibao havina maji.Yeye kafanya nini hapo kwao?Hata baba yake alipokuwa mwenyekiti wa CCM BK,Bado Ibwera iliendelea kuwa imedorola.Pia huo mpango ulisukwa na Katibu mstafu....
 
Bashiru hii ndio sura yake au? Mbona kama amekuwa mnyonge sana.
Screenshot_20210430-124841.png
 
Back
Top Bottom