Wajumbe wa kamati za kudumu za bunge zimulikwe

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
17,521
13,600
Kamati za kudumu za Bunge ni kamati ambazo zinatakiwa zisimamie miswada mbalimbali kwa manufaa ya taifa badala ya kutetea maslahi ya wachache.

Wiki liyopita kulikuwa na miswada mbalimbali ya sheria, mfano ni kupiga marufuku mifuko ya plastic ifikapo jan.2017 na mswada ya kuiwezesha Sumatra kuchukua hatua kubwa dhidi ya wanaovunja sharia mbalimbali.

Mfano ktk ktk mswada wa kupiga marufuku mifuko ya plastics kuna wabunge ndani ya kamati hizi walikuwa wanaongea as if hawaishi hapa Tz. ili kuona madhara ya mifuko hii na athari zake kwa mazingira na ustawi wa Nchi. Kwa kiasi kikubwa baadhi walikuwa wakiitetea bila hata aibu!

Ukija kwa suala la Sumatra kuna wabunge wa kamati ya sheria na katiba ambao ni wamiliki wa vyombo hivi na walikuwa wakipinga kila kitu bila kuweka mbele maslahi ya watumiaji wa huduma hizi. Kibaya zaidi kuna mmiliki mmoja ambae ni mbunge ktk kamati hii alisema ' nitatatetea hili hadi kaburuni'.

Nachelea kusema au kuhusisha na ewepo wa vyama vya wamiliki mabasi na malori Dodoma kama ulichochea 'kitu nje ya ukumbi' au uwepo wa wamiliki wa viwanda vya plastics kuwa ndio unawafanya wajumbe wetu 'kujitoa ufahamu' ila ni vzr kama Takukuru na Tiss wangekuwa wanafuatilia kwa ukaribu ili kuondoa 'figisufigisu'.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom