Wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania 2016/17 waiangukia Serikali kuomba iwasaidie kupata wafadhili

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Lundenga-akikana-jambo.jpg

Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wameiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim Lundenga wakati akiongea na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokutana nao mjini Dodoma.

Lundenga alisema changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa ni kupata ufadhili wa mashindano hayo ambayo yanafaida kwa mabinti wanaoshiriki hii ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kuwa viongozi wazuri wa baadaye.

“Mwezi wa tisa warembo wanatarajiwa kuingia kambini watakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja ambako watapewa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja kufundishwa jinsi ya kujitambua na kujiendeleza kielimu”, alisema Lundenga.

Kwa upande wake Mhe. Wambura aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kuandaa mashindano hayo na kuwaahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha mashindano yanafanyika kama ilivyotarajiwa.

Mhe. Wambura alisema, “Nawapongeza washiriki wa mashindano haya walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia kwani wameweza kushika nafasi nzuri katika mashindano ya makundi mbalimbali pia hawajawaangusha waandaaji wa mashindano kwa kuwa wanaendelea kuisaidia jamii inayowazunguka.

Naye Miss Tanzania, Lilian Kamazima alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kukubali kukutana nao na kusema kuwa mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa lisha ya washiriki kupewa zawadi mbalimbali lakini pia wakiwa katika maandalizi ya mashindano wanafundishwa jinsi ya kuwa wanawake wa kuigwa katika jamii, kuishi na kuisaidia jamii inayowazunguka.

Mashindano ya Miss Tanzania Taifa yanatarajiwa kufanyika mwezi wa kumi, hivi sasa mashindano ya vitongoji (Vituo) yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini baada ya hapo yatafuatiwa na mashindano ya Kanda.
 
Mm naona kama vile wanafundisha zaidi umalaya na siyo kujitambua na uongozi kama wanavyodai

Nachukulia mfano miss tz 2006
 
Sasa mbona mshindi wa mwaka jana hashiriki kutetea ushindi wake, huu ni uonevu, kwa sababu kwa mr. Tanzania mshindi ana haki ya kushiriki mwaka unaofuata
 
Serikali inashughulikia sukari na ilimu bure jamani hayo ya wafadhili tafuteni wenyewe
 
Ni wakati mzuri sana kwa serikali ya Magufuli kuyapotezea(Kuyapa kisogo) kabisa hayo mashindano ya mabinti kuonyesha TUPU zao. Kama inawezekana ayafute kabisa.
Ni mashindano yaliyoharibu kabisa mabinti zetu wa Kitanzania.
 
Alikuwa anapata wadhamini wa nguvu, na fedha ya maana akadharau wenzake na kuleta figisu ya kulazimisha mshindi fake, matokeo yake akafungiwa na kuomba radhi weee mwisho kafunguliwa anafikiri kuna mdhamini mwenye akili atatia pesa yake hapo alipoonesha ubabaishaji? Kama voda ndio hawana hamu na awamu hii ya kulipa kodi "inayowaridhisha" viongozi. N a aseme tu hayo mashindano ndio yanaendesha maisha yake hapo mjini asisingizie kuwanufaisha mabinti kama vile yeye hafaidiki.
 
Wakose wadhamini shindano life. Kuna uchafu mwingi ndani yake. Mungu futa shindano hili.
 
View attachment 348139

Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wameiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim Lundenga wakati akiongea na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokutana nao mjini Dodoma.

Lundenga alisema changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa ni kupata ufadhili wa mashindano hayo ambayo yanafaida kwa mabinti wanaoshiriki hii ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kuwa viongozi wazuri wa baadaye.

“Mwezi wa tisa warembo wanatarajiwa kuingia kambini watakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja ambako watapewa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja kufundishwa jinsi ya kujitambua na kujiendeleza kielimu”, alisema Lundenga.

Kwa upande wake Mhe. Wambura aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kuandaa mashindano hayo na kuwaahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha mashindano yanafanyika kama ilivyotarajiwa.

Mhe. Wambura alisema, “Nawapongeza washiriki wa mashindano haya walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia kwani wameweza kushika nafasi nzuri katika mashindano ya makundi mbalimbali pia hawajawaangusha waandaaji wa mashindano kwa kuwa wanaendelea kuisaidia jamii inayowazunguka.

Naye Miss Tanzania, Lilian Kamazima alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kukubali kukutana nao na kusema kuwa mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa lisha ya washiriki kupewa zawadi mbalimbali lakini pia wakiwa katika maandalizi ya mashindano wanafundishwa jinsi ya kuwa wanawake wa kuigwa katika jamii, kuishi na kuisaidia jamii inayowazunguka.

Mashindano ya Miss Tanzania Taifa yanatarajiwa kufanyika mwezi wa kumi, hivi sasa mashindano ya vitongoji (Vituo) yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini baada ya hapo yatafuatiwa na mashindano ya Kanda.

Naomba wadau wanaojua wanifahamishe LINO AGENCY INTERNATIONAL ni kampuni, au ni shrika lisilokuwa la kibiashara? Tangu hawa jamaa waanze hii kazi ya mamiss ni siku nyingi sana na kila mara wamekuwa wakipata ufadhili wa makampuni. Hawakujua kwamba sponsorship hizi zina mwisho wake... leo inataka serikali iwatafutie sponsorship?
 
Kama hawa viongozi wameshindwa kutafuta wafathili au kujitegemea kifetha ni bora tu uongozi uliopo waachie ngazi wachaguliwa wengine wenye good idea jinsi ya kurani hii miss Tanzania bila hela za walipa kodi.
 
wanapewa elimu ya kujitambua?? INA maana miss tz 2006, alikua kilaza? au alikua mtoro darasani? mmeharibu kwa MTT wa mtemvu na kutetea uongo,na ole wenu makampuni mkubali,ujinga wa kimagharibi mnatuletea hapa?
 
Lundenga na team yake hawakutakiwa kurudi front wao tena, lile sakata la Bi mdada wa TMK limeonyesha udhaifu mkubwa katika maandalizi haya na team yote kwa ujumla, upangaji wa matokeo na wengine kudhalilishwa
 
Serikali hii ni ya viwanda, mlishaambiwa. Kwani umiss nao ni viwanda?
 
Lundenga kama umeshindwa kuendesha hilo shindano achia wengine. Serikali inafanya Kazi na sekta binafsi na wewe ni mdau wa hiyo sekta. Yaani umeshindwa kujiongeza hadi uombe Serikali ikusaidie kutafuta wadhamini.
Kupewa kibali cha kuendesha hilo shindano ni msaada tosha. Hivyo unauwezo kuwashirikisha wadau wengine wowote kutoka sehemu zingine popote. Iweje urudi kuomba Serikali ikutafutie?
Angalizo ni kuwa Kamati ya shindano la Miss Tanzania inalalamikiwa sana kwamba haitendi haki kwenye kupata washindi. Kamati ijitazame kisha ijiongeze na siyo kukimbilia Serikalini kuficha hayo madhaifu.
Serikali Kwa upande wake iitazame Kamati hasa LlNo Enterprise Agency , imelalamikiwa kwa muda mrefu sana. Kama inakiuka masharti ya Kazi inyang'anywe uondeshaji wa shindano.
 
lundenga ni tapeli.... serikali bora iwape wachina tu kama tazara watusaidie kuendesha miss Tanzania than lundenga
 
Back
Top Bottom