Wajumbe wa CCM wapata ajali, 85 wajeruhiwa, mmoja afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe wa CCM wapata ajali, 85 wajeruhiwa, mmoja afariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Sep 30, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kada mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekufa papo hapo na wengine zaidi ya 85 wamejeruhiwa vibaya baada ya lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T420 APM walilokuwa wakisafiria kwenda kwenye mkutano wa uchaguzi wilayani Chunya kupinduka.Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 2:30 asubuhi katika eneo la Matundasi umbali wa kilometa 21 nje ya mji wa Chunya, wakati wajumbe hao wa CCM zaidi ya 100 wakitokea katika kata za Lupa, Upendo na Mamba kwenda kwenye mkutano wa uchaguzi.NIPASHE ambalo lilifika kwenye eneo la tukio na baadaye kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chunya, lilishuhudia magari ya kubeba wagonjwa zaidi ya matatu yakisomba majeruhi kuwatoa eneo la ajali na kuwapeleka hospitalini, huku wengi wao wakiwa na majeraha mabaya katika sehemu mbalimbali za miili yao.Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Chunya, Dk. Henry Mwansasu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa amepokea mwili wa mtu mmoja pamoja na majeruhi 85.Amemtaja mtu aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni Issaya Nchimbi (45), ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa tawi la CCM la Madimbwini katika kata ya Mamba wilayani Chunya.Alisema kati ya majeruhi hao, 11 hali zao ni mbaya na wamelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi, huku majeruhi wengine 63 ambao walipata mshtuko na majeraha madogo madogo wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

  SOURCE: NIPASHE
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Get well soon magambaz. Next time msikubali kubebwa kwenye fuso kama matenga ya nyanya.Imagine watu 86 kwenye fuso moja.
   
 3. a

  adolay JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Nawatakia pole nawapate nafuu, Watanzania tujifunze kutokana na kadhia hii.

  Mungu ibariki tanzania.
   
 4. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Poleni sana, Alafu utakuta traffic njiani wanayaangalia tu kwa kuwa ni magamba.
   
 5. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Safi sana. Wakati ule CUF walikuwa wanabeba watu kwenye mafuso walitungiwa sheria kali na marufuku ikapigwa, sasa leo wao wenyewe yamewakuta.
   
 6. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Polisi wa usalama barabarani waliona na wakaruhusu coz ni chama chao! Kila uchao kitengo cha usalama barabaran kinakataza haya malori kubeba abiria!! Cha kushangaza, hii sheria imekuwa "double standard". Sipati picha kama ingekuwa chama kingine cha siasa, "pangechimbika".

  Nawapa pole wafiwa na majeruhi pia. Mnapotaka kuingia kwenye siasa mnatakiwa muione leo kabla ya kesho kama tai!
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Gamba acheni kutumia Fuso kusafirishia binadamu! Mungu ampe stahili yake marehem
   
 8. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R.I.P Nchimbi, ila magamba mkome kujazana kwenye fuso. :rockon:
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Kwa nini sisiemu hawafati sheria za barabarani?
  Kwanini watumie mafuso kusafirisha binadamu?

  R:I.p marehemu
   
 10. peoples power

  peoples power JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 468
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Poleni sana wafiwa.na majeruhi wote mpone mapema.
   
 11. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Sio wakome tuu bali washindwe na kulegea kabisa...Thamani ya Binadamu ni kubwa sana. R.I.P Nchimbi
   
 12. k

  katalina JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini usubili polisi akuzuie barabarani wakati wewe mwenyewe unajua hilo ni kosa? Watanzania tujifunze kutii sheria bila....... Anyway nawapa pole.
   
 13. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  washakuambia wao ni chama tawala yaani wanatawala sheria zote,za barabarani,wizi,ufisadi,chaguzi zao rushwa njenje ila takukula hawaoni!
   
 14. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lazima ni CDM ndio wamesababisha ajali
   
 15. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ukilaza
   
 16. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CCM hakuna sheria inayowadhibiti. Sheria ya udhibiti ni kwa vyama vya upinzani tu. CCM itaanza kuonja utamu wa kudhibitiwa kuanzia 2015 wakiwa chama kikuu cha upinzani nchini (sio bungeni tu) Unaonaeeeh?
   
 17. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ndio jina lako Siku hizi?
   
 18. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,859
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hii ni aibu na fedheha kwa Gambazi!! Pia Hawa wananchi ambao ni wafuasi wa Gambazi wanapokubali kubebwa kwenye Malori (Watu zaidi ya 94) wanakuwa akili zao wameziweka rehani? au kuziacha nyumbani? Mungu awasamehe waliojeruhiwa ila next time wawe na akili Kumkichwa!!
   
 19. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na iundwe tume na ndugu wa marehemu mh, nchimbi waziri wa mambo ya ndani......itaongozwa na mwanasheria mkongwe mzee wa washili.ili kazi ikamilike haraka tutampatia watu arobaini wakumsaidia pitieni pale toyota tanzania mchukue magari vx v8 40 kwa ajili ya kuwarahisishia usafiri, gharama ziletwe wizarani tume hii ilete riport ndani ya miezi sita kwangu naomba wananxhi muwape ushirikiano............fool
   
 20. y

  yaya JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hapo kwenye wekundu si vema.
  Siasa siyo uadui. Ndiyo maana hakuna nyumba, mitaa, miji wala mikoa ya chama fulani tu. Watu wote wa itikadi tofauti hushirikiana kama ndugu. Kwa maana hiyo ni vema kuwaombea wapone kuliko kufurahia janga. Ni maoni yangu tu mkuu.
   
Loading...