Wajumbe wa bodi zote mbili Simba SC ndiyo tatizo

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,756
4,842
Salaam!

Nimesoma taarifa kwenye gazeti la Mwanaspoti la jana tarehe 10.02.2020, kwamba Simba SC inajiandaa kuwachukulia hatua wachezaji wake wanaoonekana kucheza chini ya kiwango, wanadai wachezaji wamekuwa wakiihujumu timu kwa kukubali kuhongwa na timu pinzani ili Simba ipoteze mechi zake.

Hili limenishangaza, nikajiuliza kwanini viongozi (wajumbe wa bodi) wanakwepa majukumu yao, ni wao ndio waliochukua maamuzi ya kumfukuza Aussems katikati ya msimu, tena bila sababu yoyote ya maana, wakidai wachezaji hawana nidhamu kama vile hiyo ni kazi ya kocha, na timu imeshuka kiwango sababu tu Simba ili draw mechi moja, na kupoteza moja!

Baada ya hapo wakaamua kumpa kazi kocha asiye na experience yoyote kwa soka ngazi ya vilabu barani Africa, kocha ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa timu za taifa za Zambia, na Cameroon, tena nako aliishia kufukuzwa na hizo timu sababu ya matokeo mabaya.

Kwa maoni yangu, viongozi wa klabu ya Simba na wajumbe wa bodi zote mbili ndio wanaotakiwa kujiuzulu nafasi zao kwa kuchukua maamuzi ya kukurupuka yanayo igarimu klabu wakati huu, timu inacheza mpira mbovu, haina muunganiko, mambo yanajiendea hovyo tu.

Wasilete visingizio kwamba wachezaji wanaihujumu klabu, kama wao walimuona kocha asiejua lolote kuhusu mpira wa ngazi ya klabu Afrika ndio anaifaa Simba ndio wahujumu namba moja wa klabu, kwanza wameidharau klabu yenye hadhi ya Simba kwa kumleta kocha wa aina hiyo, wawajibike kwa maamuzi yao ya kukurupuka, wasituchezee akili wapenzi na mashabiki wa Simba SC.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ile iliyokuwa inasemwa Simba mbovu ya Ausems haikuwahi kuwa na kiwango hiki cha Simba ya Sven. Mimi nimeisoma hiyo habari kwenye mwanaspoti nikashangazwa na hizo tuhuma kuwa wachezaji wanahujumu timu kwa kupewa pesa na wapinzani ili wacheze chini ya kiwango.

Nafikiri Simba inapaswa kutafuta kiini cha kiwango cha timu kushuka na kuwa wakweli ili kutibu maradhi badala ya kuhamishia matatizo kwenye timu nyingine. Wachezaji wa Simba ndio wanalipwa vizuri na wana maisha mazuri kuliko wachezaji wote wa timu za ligi kuu halafu leo waihujumu timu? Sitaki kuamini hilo la hujuma lakini labda inawezekana tusubiri tuone uchunguzi wao utakapokamilika.

Na kinacholalamikiwa sasa hivi Simba sio kupoteza mechi tu hata bali timu inachezaje? Hakuna mfumo unaoeleweka uwanjani kila mchezaji anatumia kipaji na uwezo wake binafsi, wachezaji wanakaba kwa macho, timu imegawanyika katikati mabeki kwao fowadi kwao.

Kabla ya kuja Sven ulikuwa ukiangalia Simba ikicheza inamiliki mpira na unaona kabisa kuna mipango goli linatafutwa lakini sasa hivi utaona timu inazidiwa umiliki wa mpira hata na timu za kawaida. Kiukweli mechi na Mwadui, Polisi na Namungo timu ilicheza vibaya sana hata matokeo ya ushindi tuliyopata kwenye hizo mechi sidhani kama Simba ilistahili.
 
Joo Wane, Tupo pamoja:

Matokeo kwenye zile mechi tatu hatukustahili, na ile ingefaa kuwa wake up call kwa viongozi, but wakaendelea kulala tu.

Simba ya Aussems alikuwa hata akifanya rotation performance iko palepale, tumeupiga mpira mwingi dhidi ya JS Saoura, AL Ahly, Mazembe, na Vita hapo taifa, but leo siamini macho yangu kama ile Simba ya msimu uliopita ndio hii ninayoiona, yaani kiwango kimeshuka kwa spidi ya kutisha.

Viongozi (wajumbe wa bodi) wasitafute mchawi, wao ndio tatizo kwa kukurupuka kwao kwenye maamuzi ya msingi kuhusu klabu, hakukuwa na ulazima wa kumfukuza Aussems wakati huu ligi ikiwa inaendelea, sasa hivi Simba inaruhusu magoli kila mechi, defensive lapse zipo kila mechi, wapinzani wameshatusoma wameona udhaifu wetu, kocha anashangaa tu.

Enzi ya Aussems timu ikionekana kuyumba kidogo tu, anabadilisha mfumo, kama ilikuwa 4-3-3, then atahamia 4-1-2-3, mambo yanajipa tu, but huyu waliyetuletea hamna kitu, kila siku mfumo huo huo na tunaruhusu magoli hata hashtuki!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom