jd41
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,756
- 4,842
Salaam!
Nimesoma taarifa kwenye gazeti la Mwanaspoti la jana tarehe 10.02.2020, kwamba Simba SC inajiandaa kuwachukulia hatua wachezaji wake wanaoonekana kucheza chini ya kiwango, wanadai wachezaji wamekuwa wakiihujumu timu kwa kukubali kuhongwa na timu pinzani ili Simba ipoteze mechi zake.
Hili limenishangaza, nikajiuliza kwanini viongozi (wajumbe wa bodi) wanakwepa majukumu yao, ni wao ndio waliochukua maamuzi ya kumfukuza Aussems katikati ya msimu, tena bila sababu yoyote ya maana, wakidai wachezaji hawana nidhamu kama vile hiyo ni kazi ya kocha, na timu imeshuka kiwango sababu tu Simba ili draw mechi moja, na kupoteza moja!
Baada ya hapo wakaamua kumpa kazi kocha asiye na experience yoyote kwa soka ngazi ya vilabu barani Africa, kocha ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa timu za taifa za Zambia, na Cameroon, tena nako aliishia kufukuzwa na hizo timu sababu ya matokeo mabaya.
Kwa maoni yangu, viongozi wa klabu ya Simba na wajumbe wa bodi zote mbili ndio wanaotakiwa kujiuzulu nafasi zao kwa kuchukua maamuzi ya kukurupuka yanayo igarimu klabu wakati huu, timu inacheza mpira mbovu, haina muunganiko, mambo yanajiendea hovyo tu.
Wasilete visingizio kwamba wachezaji wanaihujumu klabu, kama wao walimuona kocha asiejua lolote kuhusu mpira wa ngazi ya klabu Afrika ndio anaifaa Simba ndio wahujumu namba moja wa klabu, kwanza wameidharau klabu yenye hadhi ya Simba kwa kumleta kocha wa aina hiyo, wawajibike kwa maamuzi yao ya kukurupuka, wasituchezee akili wapenzi na mashabiki wa Simba SC.
Sent using Jamii Forums mobile app