Wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Umma washichaguliwe kiholela

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Kumekuwa na utamaduni mbaya wa bodi nyingi za mashirika ya umma kutokujua wanatakiwa kufanya nini. Bodi nyingi wanaona kuwa mjumbe ni kama biashara ya kupata pesa bure za vikao, kumwendesha mkurugenzi wapate wanachotaka, kuweka watu wao kwenye tenda za vitu mbali mbali. Tumeona hii TPDC, Tanesco, TPA .

Mimi nawalaumu hawa wanao mpelekea Rais majina ya wajumbe. Wengi wanaweka marafiki zao na watu ambao ni wasomi lakini hawajui walifanyalo.

Ushauri wangu ni kwamba bodi waweke watu wenye uwezo wa ukaguzi na kila bodi kuwe na mtu mmoja ambaye kapendekezwa na CAG na mwingine wizara ya sheria yaani mmoja lazima awe mkaguzi na mwingine mwana sheria kwa kila bodi. Kazi yao hawa iwe kuhakikisha mikataba ni mizuri kabla hata ya utekelezaji.

Ukaguzi wa CAG hausaidii kama pesa zinakuwa tayari zimeliwa! Hivyo inatakiwa pesa za wizi zizuiwe kabla ya kutumika. Lakini vilevile kwa bandari na Tanesco kuwe na kikosi maalumu kwa muda wote maana hizi ndizo sehemu kubwa za wizi wa kila mara
 
Back
Top Bottom