Wajumbe tume ya katiba hawajapata barua zao hadi sasa, wengi hawajajiuzulu kazi zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe tume ya katiba hawajapata barua zao hadi sasa, wengi hawajajiuzulu kazi zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, May 2, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu mpaka leo, pamoja na kuwa wajumbe wa tume ya katiba wameshaapishwa bado hawajapewa mkataba(barua) itakayowapa ujasiri wa kuacha ajira zao ili waanze kazi hiyo mpya waliyopewa na JK mwanahalisi linaripoti.
  Gazeti linadai pia kuwa hadi leo tarehe 2 may wajumbe hawajawahi kukaa kikao cho chote cha maandalizi ya kazi hii nzito na muhimu kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu.
  Jambo hili inakwenda kinyume na kauli ya Rais kuwa tumeamua kuwaapisha mapema zaidi (badala 30 april) ili wajiandae kuacha kazi zao mapema.
  Mmoja wa wajumbe wa tume hiyo aliongea na mwanahalisi alisema, tangu tuapishwe hatukuwa na mawasiliano na Serikali wa mkiti wetu (Warioba)
  Warioba alitumiwa msg ktk simu yake na mwanahalisi lakini hakujibu kabisa.
  Kabla ya kutumiwa msg, gazeti linadai kuwa alipigiwa simu na kuwajibu kuwa yuko ktk kikao cha ccm (yeye ni balozi wa Nyumba kumi) na akawaambia hawezi kuongea kwa kuwa wako ktk uchaguzi.

  My take;
  Ninaanza kuelewa hoja na msimamo wa Mwanakijiji kuhusu katiba mpya ninaousoma magazetini na JF.
   
 2. p

  potokaz Senior Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35

  Mkuu, nadhani wanasubiri Fungu, nijuavyo serikali imefulia
   
 3. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  If that is the case, tunahitaji kufikiri upya kama taifa kama tutafika 2015 salama, achilia mbali kuwa na au kutokuwa na katiba mpya.
   
 4. m

  member2012 Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka waliiambiwa kuwa wataanza kazi mwezi huu , na ndio kwanza watu wanatoka kwenye Mei Mosi, wengine wapo kwenye matayarisho ya budget.

  Hivi lakini kwanini waache kazi , hapo mbona sijafahamu, kwani hii si ni kazi ya muda tu. nahisi wangeeomba likizo tu kwa manufaa ya TAIFA
   
Loading...