Wajumbe kutoka Marekani wawasili Korea ya Kaskazini tayari kwa maandalizi ya mkutano kati ya Trump na Kim

African Believer

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
436
425
Mkutano uliokua uwakutanishe viongozi wa Marekani na Korea ya Kaskazi na baadaye kufutwa na raisi Trump umerejea tena ambapo wajumbe kutoka marekani wamewasili Korea ya Kaskazini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa kilele kati ya Raisi wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Korea Kim Jong Un.

Hayo yameripotiwa kupitia akaunti rasmi ya Twitter ya raisi wa Marekani Donald Trump.....
wp_ss_20180528_0001 (2).png
 
aisee kim jong un wamemkamata mahali patamu sanaa ila huyu dogo bhana sijui ngoja tuangalie
unajua mtoto akianza ubabe akiwa na umri mdogo ukubwani kuna asilimia kubwa akaja kuwa mtukutu na mkorofi mnoo
 
Kwanin Ufanyike Korea Na Sio Marekani?
Nadhani mkutano utafanyika Singapore hao wameenda kufanya tu maandalizi ya mazungumzo si unajua hapaingiliki kiurahisi, hivyo hayo ni kama matokeo chanya ya mazungumzo ya awali.
 
aisee kim jong un wamemkamata mahali patamu sanaa ila huyu dogo bhana sijui ngoja tuangalie
unajua mtoto akianza ubabe akiwa na umri mdogo ukubwani kuna asilimia kubwa akaja kuwa mtukutu na mkorofi mnoo
Wachunguzi wanadai vikwazo vimefanya hali ya uchumi wa Korea kuwa mbaya sana, nahisi dogo ameamua kusurrender. Lakini acha tusuburi tuone ni nini kitaendelea kwani hata China na ushawishi katika hilo kwani amekua mshirika wa muda mrefu wa KK
 
nililisoma na kulisikia hilo ila kutekeza silaha zake sidhanii
 
Na ndio maana twahitaji kuweka akiba ya maneno. Lakini pia Tutambue historia mpya huandikwa kila siku. Kingine watu wanadai dogo anapenda sana bata na amefungiwa kwa muda mrefu, hivyo anatamani afunguliwe ili aanze kuizunguka dunia hasa ulimwengu wa magharibi
 
Akina Kim wamekwishatambua kuwa kiburi sio maungwana na kuwa hakilipi hasa unapopambana na mataifa nguli kama ya magharibi.

Na kwamba, "If you can't defeat them, join them" ndio philosophy walioamua ku-adopt sasa na hasa baada ya mshirika wao mkuu China kuwekewa ngumu na Marekani.
 
Hasa ukizingatia vikwazo vya karibuni kuhusiana biashara kati ya Marekani na China
 
Wachunguzi wanadai vikwazo vimefanya hali ya uchumi wa Korea kuwa mbaya sana, nahisi dogo ameamua kusurrender. Lakini acha tusuburi tuone ni nini kitaendelea kwani hata China na ushawishi katika hilo kwani amekua mshirika wa muda mrefu wa KK
China ushirika wake huwa wa kinafiki.Sijawahi ona mshirika wake hata mmoja aliyefanikiwa.Mohd Gaddafi,Sadam Hussein,Mugabe,Tanzania ya CCM n.k.Kim kawashtukia mapema!
 
Na ndio maana twahitaji kuweka akiba ya maneno. Lakini pia Tutambue historia mpya huandikwa kila siku. Kingine watu wanadai dogo anapenda sana bata na amefungiwa kwa muda mrefu, hivyo anatamani afunguliwe ili aanze kuizunguka dunia hasa ulimwengu wa magharibi
ooh kumbee basi afunguliwe akale bata
 
Mkutano uliokua uwakutanishe viongozi wa Marekani na Korea ya Kaskazi na baadaye kufutwa na raisi Trump umerejea tena ambapo wajumbe kutoka marekani wamewasili Korea ya Kaskazini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa kilele kati ya Raisi wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Korea Kim Jong Un.

Hayo yameripotiwa kupitia akaunti rasmi ya Twitter ya raisi wa Marekani Donald Trump.....View attachment 788024
Mimi naomba Mungu tu haya mazungumzo yafanyike. Pia mashauri Mh. Rais Trump kama inawezekana asiongee sana kabla ya mazungumzo, akae kimya halafu kama kuna choochote ataongea baada ya mazungumzo.
 
Kwa yeyote anaipenda amani atatamani hayo mazungumzo yafanyike kwa ufanisi mkubwa ili kuifungulia milango KK na kusitisha uhasama uliodumu kwa zaidi ya miaka 65 tangia wakati vita vya rasi ya Korea.
 
Wachunguzi wanadai vikwazo vimefanya hali ya uchumi wa Korea kuwa mbaya sana, nahisi dogo ameamua kusurrender. Lakini acha tusuburi tuone ni nini kitaendelea kwani hata China na ushawishi katika hilo kwani amekua mshirika wa muda mrefu wa KK
Siyo kusurrender la hasha, ila Kim ameona saa hii ana nguvu ya kuzungumza na kusikilizwa maana tayari ana madude ya nyuklia! Hawezi kutishiwa kama mtoto, ndio maana walivyomtisha akasema kama ni mazungumzo acha yavunjike na kama mnataka tuonyeshane kwa nyuklia sawa tu! Hiyo ni lugha ya mtu mwenye nguvu! Jaribu na wewe kuiambia marekani hivyo uone kama kutakucha salama!
Kim kasema wazi kama ni kuondoa silaha za nyuklia na marekani aondoe za kwake na askari wake kule Korea ya Kusini.
 
Lakini pamoja na hayo inaonesha South na North Korea wamechoshwa na uhasama, kwani sasa inaonekana wanaenda poa. Na pia wamekubaliana kuondoa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea.
 
Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema. Pindi mkutano kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini ukifanyika tu na Trump na Kim wakipeana mkono itakua ni ishara ya kumtambua Kim kama kiongozi halali wa Korea ya Kaskazini na ataanza kua mshirika mpya wa Marekani.

Je, Mchina atakubali hili litokee au ushirika kati KK na China utachukua sura gani?
 
KK anatongozwa ili Uchina na Urusi wakaliwe chini kabisa na kuangaliwa nyendo zao kwa urahisi
Nalog off
 
Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema. Pindi mkutano kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini ukifanyika tu na Trump na Kim wakipeana mkono itakua ni ishara ya kumtambua Kim kama kiongozi halali wa Korea ya Kaskazini na ataanza kua mshirika mpya wa Marekani.

Je, Mchina atakubali hili litokee au ushirika kati KK na China utachukua sura gani?
China kwani atafanya nini, hali ya sasa haimpi faraja yoyote, anaathirika mno kiuchumi.
 
Back
Top Bottom