Wajumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar watuhumiana kuhusika na Mihadarati (Madawa ya Kulevya) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar watuhumiana kuhusika na Mihadarati (Madawa ya Kulevya)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Emils, Jun 29, 2011.

 1. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MWAKILISHI wa Matemwe, Abdi Mosi Kombo (CCM), amedai kuwa, dawa za kulevya zinaletwa na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Kombo amesema leo kuwa, wajumbe hao wanaingiza dawa hizo kupitia uwanja wa ndege na kupokewa na polisi baada ya kupigiwa saluti.

  Kabla ya kauli hiyo, Mwakilishi wa Mwajuni, Mbarouk Wadi Mussa (CCM) alisema tatizo la dawa za kulevya halijadhibitiwa kikamilifu, kwa sababu wanaofanya biashara hiyo wapo na wanajulikana na Serikali.

  "Hili suala naona hatujalifanyia kazi kikamilifu, kwa sababu wanaofanya biashara hiyo wapo na wanajulikana na wengine wamo humu humu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi," alisema Mussa.

  Kwa kauli hizo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) , Othman Masoud Othman, aliwataka wajumbe hao kuthibitisha kauli zao kwa kuwa baadhi zinatoa shutuma nzito kwa Serikali na taasisi nyingine za kisheria.

  "Hizi ni kauli nzito sana na zinatakiwa kuthibitishwa na mjumbe ... kauli hizi zinadhalilisha wawakilishi na baadhi ya taasisi kama Jeshi la Polisi na wananchi kwa kusikia watadhani kwamba kumbe dawa za kulevya zinaletwa na viongozi," alisema Othman.

  Mwanasheria Mkuu alimtaka Kombo kuthibitisha madai yake au kuomba radhi, ambapo Mwakilishi huyo aliomba radhi na kusema ni makosa ya kibinadamu tu. Othman aliwakumbusha wajumbe kuheshimu kanuni zinazoendesha Baraza la Wawakilishi, ikiwamo kutoa kauli kwa kuthibitisha na si kwa dhana tu.

  Hata hivyo, Othman alikiri kuwapo kasi kubwa ya kukua kwa biashara ya dawa za kulevya zinazoingizwa nchini na kusema sheria zipo, lakini zinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kwenda na wakati. Kwa mfano, alisema Sheria ya Kudhibiti Dawa za Kulevya ipo Zanzibar tangu mwaka 1917 hatua ambayo inaonesha wazi nia ya Serikali ya wakati huo.

  "Nataka mjue, kwamba suala la matumizi ya dawa za kulevya lipo tangu zamani sana ... lakini tunahitaji kuzipitia sheria zetu upya, ili ziende na wakati na kudhibiti tatizo hilo," alisema Masoud


  Source: HabariLeo
   
 2. Zanzibar-Nyamwezi

  Zanzibar-Nyamwezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2013
  Joined: Jun 11, 2013
  Messages: 770
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Mheshimiwa aliejaribu kusema ukweli alibidi tena aombe radhi?
   
 3. Android 00

  Android 00 JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2013
  Joined: May 23, 2013
  Messages: 776
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  aliogopa kufanywa amina chifupa
   
Loading...