Wajue Wapinzani wa Yanga Klabu Bingwa, Cercle de Joachim

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,310
Hawa ndio Cercle de Joachim wanao kutana na Yanga SC February 14 kwenye kipute cha klabu bingwa Afrika.

12717438_159965437716576_1348577227276228175_n.jpg


Timu hii inayopatikana katika jiji la Curepipe ni mabingwa wa Maurtian League mara mbili mfululizo 2014&2015 .

Ni timu inayoongoza kwa mashabiki nchini humo wakiwa na upinzani wa jadi kwa watoto wa mjini Curepipe Starlight. Huenda Yanga ikapata mashabiki kutoka kwa timu hiyo ikiwa ni dhana ya kuwaunga mkono ili mpinzan wao ashindwe.

Licha ya kisiwa hicho kuwa na timu nzuri kama AS porto lakini mabingwa hawa wanao miliki uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 6200 waliokaa , wanasifika kwa soka safi la chini wakilingia golikipa wao mkongo Boubacar ( 32) na kiungo wa kati anaechezea timu ya taifa Jean.

Yanga itawahitaji mpira wa kasi muda wote kuwafunga hawa na kuwakataa kumiliki mpira . Sehemu kubwa ya wachezaji wake wapo timu ya taifa hivyo wana uzoefu mzuri.

Tayari matajiri wa kisiwa hicho wameanza kutoa ahadi nono endapo wataweza kuifunga Yanga .

Chanzo: Samuel Samuel
 
tutawapiga hao si chini ya 6 timu gani haina uzoefu, wakija bongo tutawaruhusu mashabiki wa simba wawashabikie!
 
Back
Top Bottom