Wajue Wafilisti/Wapalestina

Wafilisti ni watu walioishi Kaanani ambao waliokuwa maadui wakubwa sana wa Israeli enzi za agano la Kale. Hawa walikuwa ni kundi mojawapo la wenyewe wa nchi ile kabla ya Israeli kuifikia kutoka Misri.

Lakini wana wa Israeli walipokiuka maagizo ya Mungu ya kuwaua wenyeji wote wa miji ile yaliyoikuta,ili wamiliki, wao wakazembea hawakuwaua wote, kinyume chake wakawabakisha baadhi yao ikiwemo hawa wafilisti na ndio hao baadaye wakaja kuwa mwiba mkubwa sana kwao kama vile Mungu alivyowaambia.

Kipindi baada ya kipindi walikuwa wakiwashambulia waisraeli, na walipomlilia Mungu, (Waamuzi 10:7-8 ), basi Mungu aliwanyanyulia waamuzi wa kuwaokoa kutoka katika mateso yao, mfano Samsoni.

Wafilisti kwasasa ndio Wapalestina, unaowasikia pale mashariki ya kati, jina hilo lilizaliwa kutoka katika lugha ya wagiriki, ambao waliwaita wafilisti wapalestina. Na ndio mpaka sasa limezoeleka hivyo.

Wafilisti ni nchi gani?

Kama tulivyoona wafilisti ni watu waliokutwa Kaanani kabla ya wana wa Israeli, lakini sio taifa au nchi. Japokuwa enzi zile walikuwa na miji yao mikuu mitano nayo ni.

  1. Gaza,
  2. Ashdodi,
  3. gathi,
  4. Ashkeloni, na
  5. Ekroni
(1Samweli 6:17, Yoshua 13:3).

Walikuwa na wakuu/Wafalme wao watano pia kila mmoja na mji wake soma (Waamuzi 3:3). Sasa Miji hii yote ilikuwa kusini magharibi mwa taifa la Israeli.

Lakini Habari za wafilisti zinatufundisha nini?

Yapo mambo ambayo Mungu anaweza kutuagiza kufanya yakayazembea na madhara yake yakawa mpaka vizazi vya baadaye, kama vile tunavyoona hawa wafilisti/Wapalestina, hawakuwa mwiba tu kwa Israeli wakati ule..Bali hata sasa ni mwiba mkali sana..Kama wewe ni mfuatiliaji wa diplomasia za kimataifa utaweza kufahamu ni kitu gani kinaendelea pale Israeli saa hii , kila kukicha ni machafuko.

Hivyo tuwe makini sana na maagizo ya Mungu, anayotuagiza tusiyapuze hata kidogo,.


View attachment 1792182
Mkuu, kiini hasa cha ugomvi wote huu ni kipi? Je ni mipaka, madaraka ama hao wafilisti wanataka kuitawala Islael?
 
Crazy God ever heard,yaani huyo Mungu ni wazimu na hafai yaani alijichagulia kakikundi ka wanywa mvinyo kutoka uru ya walkadayo na kuwapa mamlaka wanyang'anye ardhi ya watu kwa sharti et awaue wakazi wote hadi watoto na wanawake
Katili Sana huyo YHW Mungu wa islael aisee hivi kwanini asingewaongoza hao watu wake waje kusini ya misri nikimaanisha huku east Africa ambako kulikua na ardhi ya kutosha wakaja fyeka mapori na kutengeneza nchi mbaka akaamua kuwapeleka sehemu ya makazi ya watu wasababishe Vita na umwagaji damu ?
Fyeka Waamori,wagirgash,wafilisti,
wahivi,waakron na wengine wengi ili apole ardhi aiseee

Hizi dini za mashariki ya Kati na huyo Mungu wao ana walakini waafrika tuamke tuachane na huyo Mungu hafai kabisa
NB miungu yetu waafrika ilikua ya upendo Sana kabla hawa kenge kutoka middle East kuja kuharibu bongo za babu babu zetu,mwanzo walikua wanaishi kwa ushirikiano na upendo mkubwa ila hawa wavaa kobazi,kanzu na vilemba walipotua tu na majahazi yao biashara za kuuza watu zikaanza!
Walipokuja wagalatia ndio mweeee walitugawa kimakundi kabisaaaaaa

Wake up you black race!
Tunapigwa kamba!
We jamaa wew! Yaan unamshangaa MUNGU wa Israel (JEHOVAH) Me mpaka leo namshangaa huyu bwana Allah ambaye wafuas wake wakiua wanamsifia halaf yey anaona poa tu. Binafs Scriptures za Bible naona angalau znaonyesha mtiririko mzur mpaka kufikia dunia ya sas lakni hzi zilizoshuka kama allien zna walakini. So kwa kumalizia naweza sema si
Ajabu kwa JEHOVAH kuwakataa watu ambao waliabudu miungu ya kiboya ambayo wanaiabudu mpaka leo.
 
1. Yaani MUNGU alitaka wapalestina wafe wote ili Israel akae kwa raha mustarehe?
2.Je MUNGU wa UPENDO ndo huyo huyo ?


NB: Imani ni jambo gumu
Swali zuri sana hili mkuu, mimi mwenyewe nashangaa sana sijui ni MUNGU wa aina gani huyo wa kuagiza watu wauawe, labda hao Wapalestina hawakuumbwa na yeye.
 
Back
Top Bottom