Wajue viongozi kumi walioonja madaraka kwa kipindi cha muda mfupi

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,538
John F Kennedy JFK anafahamika kama miongoni mwa marais wa Marekani waliokaa madarakani muda mchache zaidi
Sasa leo tunawajadili viongozi waliokaa madarakani(walioyatumikia madaraka) kwa muda mchache zaidi
Kati yao hakuna aliyefikisha hata kawiki kaamoja akiyatumikia hayo madaraka aliyoyapata/pewa
Hapa kuna Wafalme,mawaziri wakuu n.k

--------------------------------------------------------------------

10/Sultan Khalid Bin Bargash
c7e51578062c3b7c441aaa64d41a1092.jpg
713afc3eddd2e862ca06e9ad8344a7a4.jpg

Huyu alikuwa Sultani wa Zanzibar mnamo mwaka 1869 baada ya kifo cha binamu yake lakini akaonja madaraka kwa siku mbili tu
Waingereza baada ya kusikia Bargash kawa kiongozi wa Zanzibar walimpa masaa 24 aachie madaraka kwa hiyari yake sababu hakuwa chaguo lao, lakini akawagomea na kupelekea baada ya siku moja kupita Waingereza watume meli zao za kivita na wanajeshi

Hapo ndo ikazaliwa vita iliyojulikana kama Anglo Zanzibar War ambayo ilidumu kwa muda wa dk 38 pekee iliyoisha August 27 1869 na kuwa Vita fupi zaidi kuwahi kutokea duniani
Wakati wa vita hiyo wazanzibar waliokufa na kujeruhiwa ni 500 wakati mwingereza aliyeumia ni mmoja pekee, boti mbili zilizama

Hivyo jamaa huyu sultan alitawala Zanzibar kwa muda wa siku 2 tu
 
9/Diasdado Cabello
51ed2618c894957224504e8723a80fbc.jpg
be7f71f0f51b445e06596b5eb62feb45.jpg

Alizaliwa April 1963
Huyu bwana alionja Urais wa Venezuela kwa muda wa siku moja pekee baada ya Rais kujiuzulu kufuatiia kuonekana anasapoti ubepari
Hivyo Cabello akachukua madaraka kisha akamchagua Hugo Chavez kuwa Makamu wake wa rais halafu yeye mwenyewe akajiuzulu na Chavez kuwa Rais..
.Mchezo ndo ulivyochezwa na kuisha kijanjajanja tu

Yaani kautumikia urais kwa muda wa siku moja pekee hata gwaride hakukagua
 
8/Ratu Tevita Momoedomu
0e301dcb2e9e11bb0ee8913abdf25488.jpg
8a4265a9ae777a1b09a2b6cfb0925c8d.jpg
Alizaliwa Januari 13 mwaka 1946
Huyu jamaa alikuwa Waziri mkuu wa Fiji katika muhula/vipindi viwili vifupifupi kama stuli za Tandale pale Manzese..
Mwaka 2000 alikaa madarakani kwa muda wa masaa mawili pekee wakati mwaka 2001 alikaa madarakani kwa siku mbili tu
Mnamo mwaka 2000 yalitokea mapinduzi/maasi ambapo yeye pekee akajikuta ndo amebaki kwenye jengo la serikali hivyo kuwa kiongozi kulingana na katiba ya nchi hiyo .....yaani kama ngekewa vile halafu mwaka 2001 akachaguliwa tena baada ya kuachia madaraka ili kukidhi matakwa ya kikatiba
 
7/Roger LaFontant

ed9ebc9d1e64cb67532771fa8c7cf71e.jpg
5ea442ff84823ad7319487673718fbe5.jpg
Alizaliwa mwaka 1931 na kufariki dunia 1991 akiwa na umri wa miaka 60
Huyu alikuwa kiongozi wa kijeshi huko Haiti ambapo mwaka 1991 alikuwa Rais kwa masaa 24 tu
Kisura anafanana na mchungaji Mtikila

Rais alijiuzulu hivyo Katiba ya nchi hiyo kumpa madaraka Jaji Mkuu Estha Pascal Trouillot ambaye aliitisha uchaguzi wa kidemokrasia
Lakini bwana mkubwa Fountant akatumia fursa hiyo kufanya mapinduzi na kujitangazia Urais
Ghafla bin vuuuu wajanja zaidi yake wakampindua ndani ya masaa 24 tu yaani wakati anaamka tu huko Ikulu akijiadaa kupiga mswaki hata swimming pool hakugusa

Alikuwa rais kwa masaa 24 pekee
 
6/Joseph Goebbels
2fc5ffb62bc836b7695c1d273a4b04d6.jpg
8f933951b27496c4eaeb71c3b42b0cc5.jpg

Alizaliwa mnamo mwaka 1897 na kujiua mwaka 1945 akiwa na umri wa miaka 47
Huyu alikuwa Kansela wa Ujerumani kwa muda wa masaa 5 pekee mwaka 1945 May 1

Wakati Vita Kuu ya Pili ikiendelea na Adolf Hitler kuonekana kuzidiwa akaamua kumteua swahiba wake Goebbels kuwa Kansela akiamini ni Waziri wa Propaganda ndo pekee anayeweza kumuokoa jahazi lake linalozama.
Lakini hata kabla hawajaanza propaganda zao za Hamphrey Polepole wakagundua wamezingirwa hivyo kuamua kujiua
Kuna badharia nyingi kuhusu kifo chake pamoja na cha Adolf Hitler

Jamaa kaonja ukansela masaa yasiyozidi matano pekee
 
5/Boris Yeltsin
ecace9321b02e553fc75758354aa19c2.jpg
98a5cbf3c244e27ef07db058ccb4d9ac.jpg
614aede5e039e0bc20eb5d090e3bd8d8.jpg
Alizaliwa mnamo mwaka 1931 na kufariki dunia 2007 akiwa na umri wa miaka 76 baada ya kupambana na maradhi kwa kipindi kirefu
Huyu mzee alijiteua mwenyewe kuwa Waziri mkuu wa Urusi mnamo mwaka 1998.
Hii ilikuwa wakati yeye akiwa Rais na mgogoro wa kisiasa ukiwa umepamba moto hivyo akaamua kumpunguzia majukumu Waziri Mkuu kwa kujiteua yeye mwenyewe
Baada ya kukosolewa vikali na wananchi wake na wapinzani na kuambiwa ni dikteta na mzee wa kukurupuka kama yule wa Chato akaamua fasta kuachia huo Uwaziri mkuu na kumteua mtu mwingine

Yaani alikuwa Waziri mkuu ndani ya masaa manne tu...kukurupuka ni kubaya!!
 
4/Skender Gjinushi
51723b7774b7ed774cd1572c12ca61f6.jpg

2a0eefd31e321576f5d47168006ec8a8.jpg
6cd413ceedaa6228f59570d36402238b.jpg
Alizaliwa Disemba 24 mwaka 1949
Huyu alionja Urais wa nchi ya Albania kwa muda kiduchu kama masaa mawili au manne tu
Ilikuwa mwaka 1997 baada ya uongozi wa kibepari wa Sali Berisha kushindwa uchaguzi wa kidemokrasia halafu kukataa kuachia madaraka hivyo Spika Slender akaamua kuchukua madaraka kwa mujibu wa katiba kuwa Rais wa mpito
Kisha Bunge la Albania likaamua kumtangaza mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu Rexhep Meidani kuwa Rais mpya wa Albania

Hii ilifanyika ndani ya masaa manne pekee
 
3/Carlos Manuel Piedra
61cc9bccfc1f53841562b4c15ffb11b0.jpg
79c2c69f418072ff64685eadf48689b9.jpg
4b5eac014d7745ed889043b33018e5a1.jpg

Alizaliwa mnamo mwaka 1895 na kufariki dunia 1988 akiwa na miaka 93
Huyu alikuwa Rais wa mpito kwa muda kati ya masaa 2 hadi 5 baada ya kujiuzul ;Fulgencio Battista mwaka 1959.

Hii ilikuwa baada ya Makamu wa Rais naye kuingia mitini kufuatia mapinduzi yaliyoongozwa na vijana matata akina Fidel Castro, Camilo Confuegos n.k
Katiba ilikuwa ikimraka Jaji Mkuu mwenye umri mkubwa zaidi ndo achukue madaraka hivyo Piedra akatangazwa Rais mpya halafu fasta ndani ya nasaa machache akina Castro walikuwa washaiteka Havana hivyo akakimbilia Ubalozi wa Marekani na akina Castro kuchukua madaraka

Yaani alidumu kati ya masaa mawili au manne tu
 
2/[]>Siaka Stevens[/b]
782da69fbd91bb41004c518a6fa69416.jpg
d35149c768e0add43fefd3abb377d771.jpg
45063988dd57f9da547b67aef857512a.jpg

Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki dunia mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 82.....
Aliwai kuwa Rais wa Sierra Leone kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1985
Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Sierra Leone mnamo March 21 mwaka 1967 aliapishwa kuongoza Taifa hilo

Lakini ndani ya nusu saa tu waasi wakamzingira na kumkamata hivyo kuwa nwiaho wa utawala wake wa kiKassimu Majaliwa
Baadaye akafanikiwa kurudi madarakani kuanzia mwaka 1968

Yaani alitawala nusu saa tu mwaka 1967 kama Waziri Mkuu
 
1/Prince Luis Felipe
8ba9e83df749b6ede19ac40057d91b19.jpg
cc4afb89250189268128fe976671338a.jpg
Kama mnavyojua utawala wa kifalme mrithi hujulikana mapema hata kabla ya kifo cha Mfalme
Sasa mwaka 1908 Mfalme Carlos wa Ureno aliuawa papo hapo wakati wa ziara ya kifalme ambapo pia mwanawe Luis Felipe alijeruhiwa
Sasa wakati anawahishwa hospitali tayari alitambulika km Mfalme mpya wa Ureno japo alikuwa bado hajavalishwa taji rasmi...ndani ya dakika 30 akafariki dunua akiwa njiani kupelekwa hispitali kutokana na kupoteza damu nyingi

Yaani mwanamfalme alikuwa Mfalme kwa nusu saa pekee
.
.
.
.
.
.
.
Mwisho
The Bitoz
----------------
 
Back
Top Bottom