Wajue Mashujaa na Maadui wa Katiba Mpya, Madui wa Muungano/Mashujaa wa Zanzibar!

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
1,045
Watanganyika tuna ugonjwa mbaya sana wa kupuuzia tahadhari za msingi wakati zinapotolewa na kusahau haraka kiasi kwamba tunashindwa kukumbuka hata baada ya madhira kutufika> Tunakuwa utadhani hatukuwahi kupewa tahadhari.

Kwenye suala la Katiba na Uhai wa Muungano sitasahau kamwe jinsi Tundu Lissu alivyotaanabaisha mara nyingi juu ya athari na maana ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Leo hii mkwamo utakaopelekea Mchakato wa Katiba mpya kuvunjika ni suala la Zanzibar kujitambulisha kama nchi kwenye Katiba yake mpya. Kama kuna muujiza haujapata kutokea duniani na unasubiriwa kwa hamu utokee basi ni muujiza wa Bunge la Katiba kubadilisha Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba na kisha kupata 2/3 ya kura za Wajumbe ili kunusuru Muungano wa nchi mbili na Serikali mbili!

Mpaka hatua hii ya mchakato wa Katiba nawatunuku wafuatao vyeo vifuatavyo:

Mzee Joseph Sinde Warioba -- Baba wa (Rasimu ya) Katiba ya Wananchi
Mh. Tundu Lissu --Shujaa wa Kulinda Katiba ya Muungano
Mh. Jakaya Kikwete --Mwanamageuzi Yabisi/Adui wa Muungano
Mh. Ismail Jussa -- Shujaa wa Dola ya Zanzibar

Changia kwa kuongeza orodha!!
Julai, 2012 katika Bunge Mh. Tundu Lissu alisema haya:
"Mheshimiwa Spika, katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano si tu una serikali kamili, Bunge kamili, Mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa Serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya," KAMBI ya upnzani Bungeni imelitaka Bunge kutumia mamlaka yake kuchukua hatua za kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba kwa kushindwa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Muungano kama kiapo cha kazi yake kinavyomtaka.

Archieve
: Jumuiya ya UAMSHO Zanzibar

Lakini kabla mnamo Novemba 2011 Mh. Tundu Lissu alikwisha onya kwa kuandika haya:

Muungano wetu hauwezi kuokolewa kwa maneno matamu kama 'Muungano ni lulu', etc. tu. Muungano huu umekuwa na matatizo makubwa ya kimsingi kwa miaka yote ya uhai wake. Kujifanya matatizo haya hayapo ni kuchopeka vichwa vyetu kwenye mchanga kama mbuni na kutokuyatafutia ufumbuzi. Hii ndio hatari kubwa zaidi kwa Muungano kuliko 'wapigania uhuru' wa Zanzibar kama ZARFA au wanaotaka Tangayika ifufuke kama sisi wanaCHADEMA. Napendekeza msome hotuba yangu Bungeni juzi juu ya nafasi ya Zanzibar kama bado hamjaipata. (Bofya hapa kupakua nakala)

Kwa wanaopenda kuangalia the ugly truth on its face, napenda kuwaomba mtafakari mambo yafuatayo ambayo yametokana na Muafaka wa CCM na CUF Zanzibar na kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Haya, kwa maoni yangu, yame-sound the death knell ya Muungano wetu lakini hakuna mtu yeyote kati ya machampioni wa Muungano mwenye kudiriki kuyasema hadharani:

1) Ibara ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi kwamba "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano." Ibara ya 2 ya Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

2) Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Muungano inampa madaraka Rais wa Muungano "... kuigawa Jamhuri ya muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo...." Hata hivyo, kabla hajaigawa Zanzibar katika mikoa, "... atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar...." Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inampa Rais wa Zanzibar madaraka ya "... kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo...."

3) Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Muungano inatamka wazi kwamba Rais wa Muungano ni "Mkuu wa Nchi" (ya Tanzania?) Ibara ya 26(1) ya Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kwamba Rais wa Zanzibar "ni Mkuu wa Nchi ya Zanzibar...."

4) Ibara ya 4(3) ya Katiba ya Muungano ikisomwa pamoja na Ibara ya 147(2) na vifungu vya 3, 4 na 7 vya Nyongeza ya Kwanza inaipa Serikali ya Muungano mamlaka ya ulinzi na usalama, polisi na uhamiaji na uwezo wa kuanzisha majeshi katika Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 121 ya Katiba ya Zanzibar inaunda 'Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar' ambazo ni JKU, KMKM na Chuo cha Mafunzo. Aidha, Ibara ya 121(3) inampa Rais wa Zanzibar uwezo, "... ikiwa ataona inafaa kuanzisha Idara nyingine yoyote kuwa Idara Maalum." Ibara ya 123(1) inamfanya Rais wa Zanzibar "Kamanda Mkuu wa Idara Maalum na atakuwa na uwezo wa kufanya chochote kile anachohisi, kwa maslahi ya Taifa (la Zanzibar?), kinafaa."

5) Ibara ya 117(3) ya Katiba ya Muungano inaipa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mamlaka ya kusikiliza rufaa kutoka Mahakama Kuu (ya Tanzania na ya Zanzibar). Ibara ya 117(4) inaruhusu Bunge au Baraza la Wawakilishi kutunga sheria ya kuweka utaratibu wa kupeleka rufaa kwenye Mahakama ya Rufani. Ibara ya 24(3) ya Katiba ya Zanzibar inafuta mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kusikiliza rufaa zozote zinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu kama zilivyoainishwa na Katiba ya Zanzibar na vile vile na Katiba ya Muungano.

6) Ibara ya 105(1)(b) ya Katiba ya Muungano inamtambua 'Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar' kama mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar. Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar imefuta nafasi hiyo na badala yake kuanzisha nafasi za 'Makamo wawili wa Rais' wa Zanzibar.

Haya yote ni maeneo ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano imevunjwa kutokana na Muafaka wa CCM na CUF. Sijawahi kusikia 'machampioni wa Muungano' wakipigia kelele ukiukwaji huu wa Makubaliano ya Muungano wala wa Katiba ya Muungano. Mimi na chama changu tunaodai kwamba Muungano huu uwekwe kwenye kura ya maoni ili wananchi wa pande zote mbili waamue kama wanataka kuendelea nao ndio tunaotukanwa kwamba tunawadharau Wazanzibari, au ni maadui wa Muungano, au tukiachiwa nchi tutauua Muungano, n.k. Sisi tunadai kufufuliwa kwa Serikali ya Tanganyika kama namna ya kuuokoa Muungano wetu kwa sababu hatuwezi kuendelea kufumbia macho vitu hivi kwa hofu ya 'kuwaudhi Wazanzibari' kama alivyosema Mwalimu miaka 18 iliyopita! We can no longer maintain this lie! Na 'Muungano ni lulu' is an expensive lie. Muungano uliozaliwa under pressure ya imperialist powers, i.e. Marekani na Uingereza na hofu ya Mwalimu na Sheikh Karume juu ya wanamapinduzi wa mrengo wa kushoto kuigeuza Zanzibar kuwa Cuba ya Pwani ya Afrika Mashariki hauwezi ukawa lulu isipokuwa tu kama tunafumbia macho historia halisi ya kuzaliwa kwake.

Nalidhani ni muhimu na mimi niweke mawazo yangu juu ya jambo hili ili kuuweka mjadala into its proper perspective.

Tundu

source: Wavuti - Home
 
Last edited by a moderator:
Jk hangeweza kuwakemea wazanzibar kwa kuvunja muungano kutokana na katiba yao kuitambua Zanzibar kuwa ni nchi.Kwani hakuna kitu kilichofanywa na Zanzibar bila ya idhini yake.Jk alikuwa ana jaribu kukiokoa chama chake ambacho kinatapatapa kama mtu aliye kabwa na kuishiwa pumnzi.
 
Watanganyika tuna ugonjwa mbaya sana wa kupuuzia tahadhari za msingi wakati zinapotolewa na kusahau haraka kiasi kwamba tunashindwa kukumbuka hata baada ya madhira kutufika> Tunakuwa utadhani hatukuwahi kupewa tahadhari.

Kwenye suala la Katiba na Uhai wa Muungano sitasahau kamwe jinsi Tundu Lissu alivyotaanabaisha mara nyingi juu ya athari na maana ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Leo hii mkwamo utakaopelekea Mchakato wa Katiba mpya kuvunjika ni suala la Zanzibar kujitambulisha kama nchi kwenye Katiba yake mpya. Kama kuna muujiza haujapata kutokea duniani na unasubiriwa kwa hamu utokee basi ni muujiza wa Bunge la Katiba kubadilisha Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba na kisha kupata 2/3 ya kura za Wajumbe ili kunusuru Muungano wa nchi mbili na Serikali mbili!

Mpaka hatua hii ya mchakato wa Katiba nawatunuku wafuatao vyeo vifuatavyo:

Mzee Joseph Sinde Warioba -- Baba wa (Rasimu ya) Katiba ya Wananchi
Mh. Tundu Lissu --Shujaa wa Kulinda Katiba ya Muungano
Mh. Jakaya Kikwete --Mwanamageuzi Yabisi/Adui wa Muungano
Mh. Ismail Jussa -- Shujaa wa Dola ya Zanzibar

Changia kwa kuongeza orodha!!
Julai, 2012 katika Bunge Mh. Tundu Lissu alisema haya:

Archieve
: Jumuiya ya UAMSHO Zanzibar

Lakini kabla mnamo Novemba 2011 Mh. Tundu Lissu alikwisha onya kwa kuandika haya:

ni sahihi alichosema tundu lisu lakini ndio mamuzi ya WAZANZIBAR .KUpunguza mbawa muungano maana kila tukidai mabadiliko ni kebehi na dharau .kilichofanywa ni hatua ya makusudi ya upande mmoja kulinda utambulisho wa zanzibar kama TAIFA na kwa hilo sote waznz tunakubaliana (ZANZIBAR KUENDELEA KUBAKI KUWA NCHI).
KUMBUKENI mwaka mmoja tu baada ya muungano baba wa taifa la tanganyika Nyerere aliaza kuvunja makubaliano ya muungano kwa kuahirisha undwaji wa katiba ya muungano kwa mda usiojulikana kwa kutumia bunge ambalo halikupewa mamlaka hayo na mkataba wa muungano. yeye aliyatoa wapi mamlaka hayo mtatueleza kwenye bunge la katiba mjadala ukiaza ,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom