Wajue Malaika, Majini na Binadamu Kwa ufupi

Mkuu umesema ukweli.

Mwanadamu ni most favourable creature.

I concur

Mwanadamu hana la ziada zaidi ya ubinafsi tuu.

Kwenye hii dunia yeye ndiye Mtawala lakini hakuna alichofanya zaidi ya kushindwa kuilinda na kuitawala Dunia.
Ubinafsi tuu
 
Mwanadamu hana la ziada zaidi ya ubinafsi tuu.

Kwenye hii dunia yeye ndiye Mtawala lakini hakuna alichofanya zaidi ya kushindwa kuilinda na kuitawala Dunia.
Ubinafsi tuu
conceptually, it's about
1. Choices
2. Preferences

Selfishness is a perspective!
 
Gibberish!!!
Malaika hawajaumbwa kwa "kutumia mwanga" Neno mwanga linatumika kwa malaika kwakua ni viumbe vilivyoumbwa kutenda matendo ya mwanga/Nuru/Mema kama ilivyo asili ya Muumba wao Mungu ambae anatenda yaliyo mema tu.
Ndio maana malaika walioasi huitwa malaika wa giza/kuzimu maana wameikimbia nuru! Same Applied to Human Being
Hakuna Colocarles au coloured Angels.
Nitaeleza kwannini next paragraph

Malaika hawana jinsia wala hawafanani na Mwanadamu..Ni roho
Sem wao wamepewa uwezo wa kujigeuza maumbo mabalimbal kutokana na mahitaji.. Mara nyingi malaika hujigeuza kua wanadamu ili waweze kuingiliana na wanadamu refer Story ya Maria mama wa yesu. Sio hivyo tu pia hujigeuza maumbo mabalimbal kama Moto,upepo,Radi,Wanyama nk...
So Hakuna malaika wa kiume au wa kike wote hawana jinsia! Ni kama wewe ulivyo huna jinsia ila ni mwili wako unajinsia

Paragraph hii inapingana na paragraph ya Juu!

Yote kwa yote Binaadamu ndio kiumbe first class kwa Mungu. The best creation ya Mungu ni mwanadamu ndio maana malaika na uwezo wao wote wameumbwa kumtumikia Mwanadamu

Mwanadamu kwaumba na roho ambayo ni immortal na Mwili ambao ni mortal hivyo inamuwezesha mwanadamu kuweza kuishi sehemu yoyote ile, duniani au mbinguni ambacho ni kitu malaika,shetani au wanyama na mimea wamenyimwa. Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi uungu kwa kutenda mema maishani mwake au uushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Hicho kitendo cha kuchagua ndio kinaufanya tuwe viumbe tuliopendelewa zaidi kuliko kiumbe chochote.

Kwakua roho ya Mwanadamu imetoka kwa Mungu ina Uungu basi anaweza kufanya lolote lile kwa kutumia uwezo wa akili/mind aliojaliwa.
Unaweza kujenga na kubomoa chochote kilicho ndani ya mwili waako au katika mazingira yako kwa kutegemea na unavyofikiria.
Mimi ninavyokuelewa wewe, viwango vya posts zako ndiyo huwa viko namna hii. Siyo kwenye ile post uliyowahi kusema storage inafanyika kwenye mind. Kwenye hii post upo katika ule ubora wako wa siku zote ninaoufahamu. Ubarikiwe kwa post hii
 
WAJUE MALAIKA, MAJINI NA BINADAMU KWA UFUPI.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Leo tutajadili Kwa ufupi Sana habari za viumbe watatu ambao ni Malaika, Majini na Binadamu.
Mada hii inaweza kuwafikirishi mno, mada Tata lakini haitatufanya tusiijadili.

Niite Taikon wa Fasihi, Mwana kutoka Nyota ya Tibeli, nyota yenye mbawa mbili ipaayo upande huu mpaka upande huu.

Ulimwengu na hapa namaanisha sio tuu Dunia hii tunayoishi, bali hata Nyota Kwa Aina zake, Sayari Kwa Aina zake, Setilaiti Kwa Aina zake, na magimba mengine makubwa kadiriyl ya majina na Aina zake yaliyopo ulimwenguni. Yakulikanayo na yasiyojulikana. Yaliyokuwepo ambayo sasa hayapo, na yaliyokuwepo na yaliyopo, yatakayokuwepo ambayo hayapo yote ndio ninayoyamaanisha na kuyahusisha hapa.
Ambayo ndani yake huishi viumbe kulingana na jamii zao, hulika na mahitaji Yao.

Wapo viumbe wa Aina nyingi Sana. Lakini Aina kuu kulingana na malighafi walizotengenezwa nazo kuna Aina kuu nne za viumbe;

1. Viumbe Mwanga
2. Viumbe udongo
3. Viumbe Maji
4. Viumbe Moto
5. Viumbe hewa
6. Viumbe vilivyochanganya malighafi.

Kila kiumbe hapo kinautawala wake na maumbile yake. Na msingi Mkuu WA maumbile hutokea sehemu moja.

MALAIKA
Malaika ni viumbe vilivyoumbwa kwa Mwanga/Nuru. Wapo Malaika wekundu hawa hutoa Nuru nyekundu, Malaika weupe, Samawati, Malaika waridi, Malaika manjano, hata Malaika weusi wenye ukijivu wapo, kila Malaika hutoa Nuru kulingana na rangi yake.
Hata hivyo wapo Malaika wasio na rangi, yaani Colourless.

Malaika kimaumbile wamefanana na binadamu au majini.
Ingawaje tofauti kubwa ni kuwa Malaika wanambawa, wapo Malaika wenye mbawa mbili, wapo wenye mbawa tatu, nne, sita na kumi na mbili kuendelea kulingana na jamii ya hao Malaika.
Mbawa na rangi za Malaika ndio huunda Madaraja au jamii za Malaika.

Malaika hawana jinsia, hivyo hawazaani wala hawazaliwi. Hakuna Malaika wa kike wala wakiume. Ingawaje wanaweza kubeba uhusika wa jinsia yoyote iwe ya kike au yakiume kimajukumu na kiwajibu. Ila sio kwenye suala la kibaiolojia.

Malaika wameumbwa Kwa mfumo wa one phase, au One by one Traffic. Yaani wao hawana option, waumbwa one way. Bila tamaa, hawana wema au ubaya. Hii kisheria inawafanya wasiwe na dhambi au makosa. Yaani Malaika hakosei.

Malaika hawafi wala hawazaliwi, hawazeeki.
Hawana mfumo wa Aina yoyote wa kuzaliana.

Malaika ndio mtawala katika ufalme WA viumbe vilivyoumbwa Kwa Mwanga, ingawaje vipo viumbe vingi Sana vilivyoumbwa Kwa Mwanga ambavyo huishi katika tawala za Malaika katika nyota za mbali.

Malaika Kidini hujulikana na Roho za Mungu, Wafanyakazi, wajumbe na jeshi la Mungu. Ingawaje neno jeshi katika muktadha huu haimaanishi linamlinda Mungu, kwani Kama nikisema hivyo nitakuwa nimeeleza kuwa kumbe Mungu naye anaweza kushambuliwa na kudhuriwa na maadui.


MAJINI
Majini ni viumbe vilivyoumbwa kwa Moto. Viumbe hivi vinafanana na Binadamu au Malaika kimaumbile.
Ninaposema kimaumbile namaanisha, kichwa, tumbo na miguu miwili.
Ingawaje.
Wapo majini au Malaika wenye viungo zaidi isivyokawaida.

Majini yameumbwa katika mfumo WA two way phases, majini Yana jinsia, yapo majini ya kiume na pia yapo majini ya kike. Majini yanazaliana Kama vile wanadamu.
Majini yanazaliwa na kufa Kama ilivyo Kwa binadamu. Ingawaje majini yanaishi miaka mingi ukilinganisha na mwanadamu.

Wastani WA umri wa kuishi kwa majinni ni miaka 1700, huku mengine yakifikisha mpaka miaka 2000.
Jinni lenye miaka 300 bado ni Jinni kijana kabisa Kwa binadamu ni Kama kijana wa miaka 18 hivi. Wakati Kwa upande wa Malaika wao hawahesabu siku yaani hawana miaka.

Majini Kama walivyobinadamu, wapo wema na wapo wabaya.
Majini hula vyakula Kama ilivyo Kwa binadamu, Vyakula vya Majinni huweza kuwa nyama za viumbe wengine, au hata vinywaji vya Mimea. Hata hivyo Jinni linalouwezo WA kujigeuza na kuwa binadamu Kama ilivyo Kwa Malaika.
Ikiwa litafanya hivyo, basi huweza Kula chakula cha nafaka au majani Kama wafanyavyo binadamu lakini vyakula hivyo havitakuwa na mchango wowote katika mifumo Yao.

Jinni ndio mtawala katika ufalme WA viumbe walioumbwa Kwa Moto. Yapo majini yenye mikia Kama mijusi, yapo yenye kwato, yapo majini ambayo huweza kuhusishwa na Alliens

Jinni huweza kuzaa na binadamu, na ikiwa hiyo itatokea, basi Gene za Jinni zitakuwa Dominant wakati Gene za binadamu zikiwa Recessive. Hivyo mtoto Kwa sehemu kubwa atakuwa na asili ya Ujini kuliko ubinadamu.

Majini huishi nyota za karibu na nyota yetu ya Jua. Kumaanisha Majini ni majirani zetu ukilinganisha na Malaika.



BINADAMU
Binadamu ndio Sisi sasa.
Tumeumbwa Kwa udongo. Mfumo wetu ni two phase. Yaani tuna uwezo wa kuchagua mazuri na mabaya.

Binadamu ndio Mfalme katika viumbe walioumbwa na udongo.
Tunajinsia, wapo wakike na wapo wakiume. Tunazaliana.
Tunazaliwa na tunakufa
Wastani WA kuishi Kwa binadamu unategemeana na nyakati kutokana na sababu za athari kadha wa kadhaa!

Tangu miaka ya 5000 huko wastani WA kuishi binadamu ni miaka 70.

Maumbile ya mwanadamu wa kawaida ni miguu miwili na mikono miwili yenye vidole vitano Kwa kila Mkono na mguu. Ingawaje wapo wanadamu wenye zaidi ya vidole hivyo.

Mwanadamu mwenye vidole zaidi ya vitano Kwa kila Mkono au miguu anaasili ya Viumbe vya Ujini. Ni super human.
Hata hivyo wanadamu hawa wapo wachache Duniani na wapo zaidi ukanda ulioathiriwa zaidi na muingiliano na viumbe wa kigeni kutoka nje ya Dunia.

Mwanadamu anauwezo wa kupewa mimba na majini au kulipa Jinni Mimba Kwa Sehemu kubwa mifumo ya uzazi baina ya Jinni na Mwanadamu vinafanana. Wote wanabeba mimba miezi Tisa.
Hata hivyo, mtoto anayezaliwa huwa na sifa za ziada na za kustaaajabisha na vipaji na katana za kushangaza tofauti na binadamu WA kawaida.

Wapo binadamu wenye rangi nyeupe, manjano, Nyeusi, nyekundu ambapo huenda sambamba na rangi ya mboni za macho Yao na rangi ya nywele zao.

Binadamu Kama binadamu Hana uwezo wa kibuni mambo makubwa Kama hatapata msaada kutoka Kwa viumbe vilivyoumbwa na Moto au Mwanga. Yaani majini au Malaika.

Mwanadamu hawezi kuliangalia Jinni au Malaika pasipo kufa, ni mpaka ufanyike mchakato Fulani ndipo awe na uwezo wa kuona majini au Malaika.
Au majini na malaika ndio yajigeuze maumbo ya kibinadamu.
Mwanadamu anauwezo wa kumuona Malaika au Jinni kupitia ndoto pekee. Zaidi ya hapo ni mpaka mchakato maalumu ufanyike.

Hakuna Mwanadamu aliyewahi kumuona MUNGU na haitakuja kutokea mwanadamu akamuona Mungu.
Isipokuwa Mungu anaweza kujidhihirisha kupitia viumbe wake.

Je dhana ya lusifa/Shetani imetokea wapi?
Je Shetani/Lusifa au Jinni au Malaika?
Yaani ipi asili ya Lusifa?

Kumbuka wapo viumbe wenye mchanganyiko wa malighafi.
Yaani kaumbwa Kwa Moto, Mwanga na hewa,
Au kaumbwa na Moto na mwanga pekee,
Au Moto na udongo pekee
Au kachanganywa vyote.

Niishie hapa!

Ulikuwa nami, Taikon mwana kutoka Tibeli. Kuhani katika Hekalu jeusi, kwenye mnara mwekundu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa Sasa MOROGORO
Kwanza tueleze hayo uliyoyaleta ya "Malaika, majini na watu" umeyatoa kitabu kipi cha Mwenyezi Mungu? Kwani hapo umetumia maneno ya uelewa wako kutokea wapi? (references).

Mafano hai. mimi ni Muislam nikiandika kuhusu hayo ntaandika kwa mujibu wa Qur'an pekee. Kitabu kisicho shaka kabisa.
 
Kwanza tueleze hayo uliyoyaleta ya "Malaika, majini na watu" umeyatoa kitabu kipi cha Mwenyezi Mungu? Kwani hapo umetumia maneno ya uelewa wako kutokea wapi? (references).

Mafano hai. mimi ni Muislam nikiandika kuhusu hayo ntaandika kwa mujibu wa Qur'an pekee. Kitabu kisicho shaka kabisa.

Hapo kwenye kisicho na Shaka ndipo unapokosea,
Hakuna kitabu Duniani kisicho na shaka
 
Malaika walioasi Kule mbinguni ndo Haohao majini, mapepo, aliens, nephilims, gods, Hollywood superheroes K.v spiderman superman etc
 
Back
Top Bottom