Wajue ma DED zaidi ya 74 wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni wanachama wa CCM

Wanaccm tunahitaji kuungana,kufunga na kuomba katika kipindi hiki kigumu kwetu. Mungu atasimama pamoja nasi , maana tukiruhusu shetani akasimama na kujitutumua mahakama ya rufani, tutapata taabu sana, na huenda tukaishiwa pumzi hukuhuku kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kabla hatujafika uchaguzi mkuu.TUUNGANE KWA PAMOJA
 
Hii nchi bhana! Ndio tunataka maendeleo kwa walioshika madaraka kufanya upuuzi huu!
Hawa ndio wanaotusumbua kila siku kusema mgombea wa ccm amepita bila kupingwa *****
 
Hata sio chuo kata.. ni chuo private. Alikuwa mwalimu wa partime kuziba nafasi ya mwalim mwingine.. ambae aliondoka wakakosa mtu wa kushika hiyo nafasi.
By then.. nilikuwa mgeni na mambo ya chuo..sijui alipataje ile nafasi.
Chuo cha kata Khaa, Sasa huyo mwalimu au Seminar leader

Chuo kikuu unafundishwa na Mr badala ya PhD holders na professor

Hao bachelors na Masters ni Seminar leader wa kusaidia instructor, Khaa umefundishwa na Mr, vyuo vya kata duu
 
DED wa Mwanga na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwa tiketi ya ccm oysterbay DSM
FB_IMG_1557960339351.jpg
 
Hii ni thread maalumu kwa Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) ambao ni wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wakati huo huo ni makada wa Chama cha Mapinduzi.

View attachment 1098421

View attachment 1098390
1. Kisena M. Mabuba, DED wa Halmashauri ya Misungwi na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Jimbo la Misungwi.

View attachment 1098391
2. Lutengano G. Mwalwiba, DED wa Magu na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu Jimbo la Magu. 2015 alishiriki Kura za Maoni za Ubunge za CCM Tanzania Busokelo.

View attachment 1098393
3. Anna-Claire Shija, DED wa Same na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Same Mashariki na Magharibi. 2015 alishiriki Kura za Maoni za Ubunge wa CCM Tanzania Sengerema.

View attachment 1098395
4. Netho Ndilito, DED wa Mufindi na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Majimbo ya Mufindi Kaskazini na Kusini.

View attachment 1098396
5. John Lipesi Kayombo, DED wa Musoma na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Majimbo ya Musoma Mjini n Vijijini. Alikuwa mNEC wa CCM kupitia Vyuo Vikuu.

View attachment 1098397
6. Esther Anania Chaula, DED wa Ukerewe na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Jimbo la Ukerewe.

View attachment 1098432
7. Elias Mahwago Kayandabila, DED wa Mbogwe na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Jimbo la Mbogwe. 2015 alishiriki Kura za Maoni Ubunge CCM Kigoma Kaskazini.

View attachment 1098495
8. Jefrin Lubuva, DED wa Mwanga aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Osterbay kwa tiketi ya CCM.

9. Adeladius Makwega, DED wa Mbozi na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Jimbo la Mbozi. 2015 alishiriki Kura za Maoni Ubunge CCM Jimbo la Kigamboni.

10. Pius Shija Luhende, DED wa Itigi na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Majimbo ya Manyoni Magh na Mash. 2015 alishiriki Kura za Maoni Ubunge CCM Kishapu.

11. Jimson Peter Mhagama DED wa H/ wilaya ya nyasa kabla ya uteuzi wake alikuwa Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma.

12. Falesy Moh’d Kibasa, DED wa Kondoa DC na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu Jimbo la Kondoa Vijijini. 2015 alishiriki Kura za Maoni Ubunge CCM Jimbo la Iringa.

13. Waziri Mourice, DED wa Karatu na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Karatu. 2015 alishiriki Kura za Maoni za Ubunge CCM Kigoma kusini.

14. Kaigounze Alexius, DED wa Mlele Mkoani Katavi, na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa Jimbo la Mlele.

15. Khalifa K. Mponda, DED wa Kondoa Mji na Msimamizi wa Uchaguzi wa Kondoa Mjini.2015 alishiriki Kura za Maoni Ubunge CCM Jimbo la Moro Kusini Mashariki.

16. Florent Laurent Kyombo, DED wa Mvomero na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Jimbo la Mvomero. 2015 alishiriki Kura za Maoni Ubunge CCM Jimbo la Nkenge.

17. Alphonce Magori, DED wa Butiama msimamizi Uchaguzi Mkuu Musoma vijijini, 2015 aligombea ubunge Jimbo la Musoma Mjini.

18. Listi inaendelea....
18. JUMAA MHINA , DED LONGIDO huyu ni kada kama kunguni na kitanda, amegombea jimbo la kawe 2010, 2015 na kote alishindwa. Huyu Jamaa yupo fair, huwa anapendwa sana na watu, inasemekana anarudi kuchukua jimbo la kinondoni
 
Wanaccm tunahitaji kuungana,kufunga na kuomba katika kipindi hiki kigumu kwetu. Mungu atasimama pamoja nasi , maana tukiruhusu shetani akasimama na kujitutumua mahakama ya rufani, tutapata taabu sana, na huenda tukaishiwa pumzi hukuhuku kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kabla hatujafika uchaguzi mkuu.TUUNGANE KWA PAMOJA
Mkuu hayo maombi yenu hata shetani anawashangaa yataenda kwa Mungu yupi??Mungu hapendi dhuruma yaani bila aibu makada wenu wasimamie uchaguzi wa vyama vingi halafu mnawaambia hao wakurugenzi atakae ruhusu jimbo liende upinzani kazi hana mambo gani hayoo??bila aibu mchana kweupee??
 
57 Reactions
Reply
Back
Top Bottom