Wajua wengi wanaabudu na kumtumikia Shetani Wakiamini ndiye Mungu wa Kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajua wengi wanaabudu na kumtumikia Shetani Wakiamini ndiye Mungu wa Kweli?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Pascal Mayalla, Sep 14, 2012.

 1. P

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,183
  Likes Received: 10,223
  Trophy Points: 280
  Wababodi,

  Preamble: Mungu Baba, ana Nguvu za Kimungu za kutenda miujiza ila pia shetani naye, anazo nguvu za kishetani za kutenda miujiza kama ile ile atendayo Mungu!. Hivyo kuna wengi waanaomwabudu na kumtumikia shetani, huku wakipata mafanikio makubwa, majumba, magari ya kifahari, fedha na utajiri wa ajabu, huku wakidhani ndiye Mungu wa Kweli Aliye Juu!.

  "The deviding line betwen Mungu wa Kweli na Shetani is very thin, kwa sababu wote wana "uwezo" ndio maana yako madhehebu makubwa tuu ulimwenguni, wanafanya ibada za masanamu, na kutoa kafara za damu kwa kuchinja, wakijidhania wanamwabudu na kumtumikia Mungu wa Kweli, kumbe wanaye mwabudu na kumtumikia ni shetani!.

  Pia wako wachungaji, mitume na manabii wafanyao miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina la Bwana, huku wakijiaminisha wanatumia nguvu za Mungu, na kwa kulitaja jina la Yesu, lakini kiukweli, wanatumia nguvu za giza bila waumini wao kujijua, wao wakiamini wameponywa na Mungu kumbe ni shetani!.

  Jana baada ya kuingalia mahojiano ya Mkuu wa Freemasons na Gerald Hando kwenye Clouds TV, nimeguzwa kuandika haya yafuatayo!. Nakuomba uyasome tuu kama hadithi kwa sababu sitarajii kutoa reference zozote, kupitia vitabu vitakatifu, ili wewe uendeleekuishikilia imani yako kwa mujibu wa mafundisho ya dini yako, ila tuu niwape angalizo, kitakachokupeleka mbinguni sio hiyo dini unayoiamini, bali ni kumjua Mungu wa Kweli na Uzima na kutimiza mapenzi yake!.

  Dini nyingi zina limit thinking ya waumini wake, sisi Wakristu limit yetu ya thinking ni uwepo wa Mungu, haturusiwi to think beyond, huyu Mungu, alitoka wapi, alianzaje na source yake ni nini, tunafundishwa tuu kuwa yeye ndiye mwanzo na mwisho, Alfa na Omega!.

  Pia tunatajiwa uwepo wa shetani, hatuambiwi huyu shetani alianzaje na kama ni muharibifu hivi, kwa nini Mungu hamuangamizi, dunia ikapata amani!.

  Mimi baada ya kuishi India, nikasoma kidogo Eastern Sciences just for knowledge, ndipo nikagundua kumbe Christianity na Islam ndizo dini mpya za juzijuzi, Hinduism na Budhiism zilitangulia sana, ukizisoma vedas, unapata mwanga mpya wa self awarenes inayakufanya uwe na uwezo wa kuhoji beyond God!.

  Kwa vile mimi ni Mkatoliki die hard!, nilipokuwa Italy, nilitafuta fursa ya kufika St. Peter Basilica, wale wanaofika pale kwa ajili ya kuabudu, you can't query anything, mimi kwa vile nilisha visoma sana vitabu vya Malachi Martin, hivyo nilipofika nilitamani kuutafuta ukweli beyond huu tuusikiao na ndipo nikafahamu!.

  Sipendi kuwatisha wale ambao limit ya thinking yao end with God, ila naomba niwajulishe kuwa mwanzo wa Mungu, pia ndio mwanzo wa satan, na Lucifer, sio tuu ndiye alikuwa 2nd in comand baada ya God the father, he is still is!. Lucifer alipoasi, Mungu alimfukuza ila hana uwezo wa kumuangamiza!. Mungu Baba anauwezo mkubwa kuliko shetani, ila shetani nae anaowezo wa pili chini ya Mungu. Uwezo pekee wa Mungu ambao shetani hana ni Kuumba, na kutoa uhai!. Mengine yote ambayo Mungu anayaweza na shetani pia anayaweza. Hivyo kuna hawa wahubiri kibao wanafanya miujiza kwa jina la Mungu, lakini aliyewapa uwezo huo wa kufanya miujiza hiyo sio Mungu ni shetani!.

  Kabla Mungu hajamuumba Adam, baada ya uasi wa shetani, Mungu akashauriana na NENO, malaika mkuu Mikaeli, na Gabrieli, tuumbe kiumbe kitakacho tutii, ndipo akamuumba Adam!. Mara baada ya Mungu kumumba Adam, kweli Adam alikuwa mtii, shetani akamdhihaki Mungu, kuwa ataupimaje utii wa Adam kama hana temptations, akamsisitiza ili kuupima utii wa kweli, Mungu amruhusu shetani amtempt huyo Adam, akivishinda vishawishi ndipo Mungu atathibitisha kweli yeye Mungu ndiye zaidi!. Shetani akasuggest the type ya temptation!.

  Mungu alipomuumba Eva, pia akaviweka vile viungo vya temptation kama shetani alivyoshauri ni Mungu akawapa maonyo Adam na Eva kuhusu matumizi ya viungo hivyo ambavyo kwenye Biblia vimeitwa "tunda" na tendo limeitwa "mti wa mema na mabaya"!. Mema ni uzima, mabaya ni kifo!. Mungu akawaambia wakila matunda ya mti huo ni hakika watakufa!. na shetani waka bet nani zaidi!.

  Ili kumlinda Adam na Eva na ushiwishi wa shetani, Mungu akaweka malaika wawili wenye upanga wa moto pale getini, kuzuia shetani asipite. Shetani akajigeuza nyoka akapenya getini na kuingia bustanini!. Alipofika ndani, akajigeuza a very handsome man na kumfanyia timing Adam akamange mane mbali kidogo!.

  Eva akashtuka kuona kuna kuna binadamu mwingine zaidi ya Adam!. Ndipo shetani akamuuliza Eva, hicho kiungo "tunda" ni cha nini?, Eva akamjibu, ni cha mema na mabaya Mungu katukataza tusivitumie!. Shetani akamwambia Eva, Mungu amewadanganya, hilo tunda la mti wa katikati, ndilo tunda tamu kuliko matunda yote (kweli au sii kweli?), na ukilila tunda hili, utapata raha kubwa kuliko raha zote duniani (kweli au sii kweli?) lakini zaidi ya yote hayo, shetani akamuhakikishia Eva, kuwa wakila tunda hilo, sio tuu watapata raha kubwa kuliko zote, bali pia watakuwa na uwezo wa Kimungu, wa kujiumbia viumbe wengine wengine wadogo! (prpcreation)!.

  Kwa vile hayo mambo Eva hayajui, shetani akamuonjesha namna ya kumega tunda! kwa kumshughulikia na kweli, Eva alifurahi, alienjoy na kukiri hakuwahi kula tunda tamu kama lile!, na siku hiyo Eva ali mconceive Cain!. Baada ya Eva kuonjeshwa dose ya shetani, Adamu aliporudi, Eva akalazimisha anataka, japo Adamu alisita sana, Eva alimfanyia manjonjo kama alivyoelekezwa na shetani na kumuelekeza Adam jinsi ya kula "tunda", Adam akaingia line, tunda likamegwa, na baada ya kula wakaishia usingizini!.

  Yote hayo yakifanyika Mungu anaona na hakuwa na uwezo wa kumzuia kwa sababu ita was a bet!. Ndipo Mungu akamuita Adam, na for the first time wakajistukia viongo hivyo ni vya nini, wakajiona uchi na kuanza kujificha!. Shetani alishinda, binadamu alimuasi Mungu and HE had no way out, bali kuwafukuza toka ndani bustani na kumpa Adam adhabu ya kula kwa jasho lake baada ya kukubali kudanganywa na mwanamke!, na Eva akapewa adhabu ya kubeba mimba miezi 9 na kuzaa kwa uchungu kufidia utamu wa starehe ya shetani!.

  Tangu hapo ni kweli binadamu wakapata uwezo wa Kimungu kuzaa watoto, Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba maumbile ya procreation kuwa kama "handshake" au hata "polination", vile viungo ni mpango wa shetani, na lile tendo ni la kishetani!.

  Mtoto wa kwanza wa Eva , yule Cain ni product ya shetani ndio maana akazaliwa na tabia za baba yake, na mtoto wa Adam ni Abel. Na ndio maana sisi Wakatoliki tunaamini lile tendo la kumtengeneza mtoto ni dhambi as a result, mtoto ni product ya dhambi hivyo kuzaliwa na ndhambi ya asili (original sin) ya Adamu na Eva na ili kuiondoa kila mtoto hutakiwa kubatizwa ASAP akishazaliwa!.

  Sasa kitu ambacho Gerald Hando hakuambiwa kuhusu hawa freemasons, ni kuwa huyo supreme being wanaye muabudu ambnaye sio Mungu ni nani?, ili uweze kumuabudu shetani, lazima kwanza uamini Mungu ndipo shetani aonyeshe uwezo wake zaidi ya Mungu na kukubali kuwa mfuasi wa shetani kwa kufanyiwa "initiation" once in, always in, na ukichange mind kuamua kutaka kutoka nje, Satan himself, will deal with you!. Ukisha fanyiwa "initiation" unaonyeshwa what will befall you if you decide to walk out!, and you'll never even think!.

  Wako wengi hukimbilia makanisa ya wokovu ili kutafuta miujiza, ila sio wengi ambao wanazijua sources za hizo powers za wachungaji wao, wahubiri wao, mitume wao na manabii wao, ila pia Bwana wetu YESU KRISTO alishatuambia, "watakuja watu, watafanya miujiza, kuponya na kukemea mapepo kwa jina langu, lanini sio wangu!"

  Muumini mmoja akauliza " Sasa tutawatambuaje?, Yesu akamjibu, utawatambua kwa matendo yao!"

  Naomba kuwakilisha!

  Pasco.
  NB. Pasco wa jf ni Mkatoliki Die Hard, ili for interest, Ameisoma Biblia kama "hadithi" tangu ukurasa wa kwanza, mpaka ukurasa wa mwisho, neno kwa neno, mstari kwa mstari, sura kwa sura, kitabu kwa kitabu!. Pia amewasoma Rosea Crusis (Rosecrusians), Bahai La and the New Era, Watch Tower, Hinduism, Budhiism, nimemsoma Dalai Lama, Lobsang Rampha, L-Ron Hubbard na Dianetics, Maharish Maheshi Yaga, Allen G.White na wengine wengi, pia nimehudhuria mihadhara mbalimbali ya kiimani wakiwemo hawa jamaa wa Krishna pale Kisutu. Sijaisoma Quaran tuu!. Na kwa kupitia maswahibu niliyowahi kukumbana nayo mimi ni Shuhuda kuwa Mungu wa Kweli na Uzima aliye Juu yupo, ila na shetani pia yupo!.
   
 2. Shardcole

  Shardcole JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,541
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Mkuu Pasco, huwa nakubali sana michango yako kwenye siasa tu ila hapa kwenye imani umeangukia pua vibaya kwani umejitahidi sana ku-edit neno la Mungu na biblia inasema hivi kwenye kitabu cha ufunuo ni kwamba ole wake yule atayeongeza au kupunguza neno katika uzima.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,463
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pasco ulichofanya ni kutaka kuingia msitu wa Kongo kwa topaz
   
 4. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,680
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Duh umenitoa kwenye usingizi na kama mtoto ni matokeo ya dhambi kwanini kuna ndoa kama kuzaa ni dhambi?
   
 5. mgen

  mgen JF Bronze Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 13,910
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Kwani hapo kaongeza neno gani? uelewe nyoneza inayoongelewa kwenye bible mfano; usiibe! nyongeza inakuwa hivi! usiibe ila ukiwa na njaa sogeza ule ili usife.....
   
Loading...