Wajua jinsi ya kumdhibiti mpenzi anayepiga mizinga?

mwingine unakuta mvivu kujishughulisha hata ukimtuma kitu tu analalalamika mbaya, ukimpa michongo anaiponda but at the end of the day akikuona tu anakupiga mzinga na ukimnyima tu stories zinaanza ooh dogo mbaya,

Kuna wengine wanaleta usista duu na kukandya kazi za maboksi huku hawana kazi. Lakini kila mara wanakupiga mizinga....ukiwaambia kwa nini usitafute hata kazi ya kuchoma chipsi anajifanya matawi ya juu...eti hataki.

Akiwa na shida ana kuja kwako kukuomba umsaidie...sasa unabaki unamshangaa. Kazi hataki, zingine anaziponda, lakini hachoki kuomba hela toka kwa hao wanaofanya hizo kazi anazoziponda yeye.

Watu kwa kulazimisha kuonekana matawi ya juu...shenzi kabisa.
 
Tatizo nyinyi hamjakutana nao, mtu ana kipato kikubwa kuliko wewe na bado akikuona anakupiga mzinga, mwingine unakuta mvivu kujishughulisha hata ukimtuma kitu tu analalalamika mbaya, ukimpa michongo anaiponda but at the end of the day akikuona tu anakupiga mzinga na ukimnyima tu stories zinaanza ooh dogo mbaya, hayo mambo mi siyapend, ni bora utoe kwa mtu mzima au mshkaj unaejua jamaa mchakarikaji sema mishe tu zimemuendea vibaya
huku pambanua hivi toka mwanzo,even though,umesha wai kuwaambia alafu ukaona kama wanarudi tena?je unadhani kuja kuwaanika hapa jf tena chtchat umesolve tatizo?pamoja na hayo jifunze kutoa kwa moyo mmoja sadaka si mpaka kanisan tu ama msikitini,mungu atakuongezea mara dufu pale ulipotoa kwa moyo mkunjufu
 
kaniudhi sana jamaa!hawa ndio wakiwa kivulini wanawasahau walio kwenye jua,kama we fisadi maisha yako ndio yatakua mazuri,na maisha mazur hayafichiki,kama unaonekana mambo safi razima tukuombe.yaani umeniboa kileta uhalo wako hapa chichat

Ni bora akuombe michongo angalau, but mwingine hata ukimpa dili anaponda na bado akikukuta anakupiga mzinga, nimekuudhi vipi kwa nini upende kuomba omba wakati nguvu unazo, bora uombe hata mtaji tujue moja unataka kutoka, but unakuta mtu anaomba kila kitu tena mtu mzima wa afya na kutwa nzima kazi yake kushinda kijiweni kubishana yanga na simba sijui manchester, ccm, chadema na mengineyo, maisha magumu jitume kijana usipende kuwa tegemezi,,,,

Jitahid uombe pale kweli umekwama but sio kila siku hadi watu wanakuchoka,,, mungu amekupa afya njema fanya kazi upate chako maana hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile, sasa kwa nini ule kwa mgongo wa wenzako wanaofanya kazi?
 
Dah tukumbuke kuna kupanda na kushuka. Alokupa wewe ndo kamnyima yeye.. Ukitoa ndio unapata... Km unayo ni vyema kumpa. Kuna wengine wamezoea kuomba ila kama unahisi anashida mstiri nawe u neva know nani atakustiri
 
Dah tukumbuke kuna kupanda na kushuka. Alokupa wewe ndo kamnyima yeye.. Ukitoa ndio unapata... Km unayo ni vyema kumpa. Kuna wengine wamezoea kuomba ila kama unahisi anashida mstiri nawe u neva know nani atakustiri

point,i salute you
 
Wakati ndo sasa, hatuwezi kujua kama kamwambia au hakumwambia, mtoa mada kaleta tu kero yake anayoishuhudia, hakuna sababu ya kutake it personal,

nikirudi kwenye mada, upande wangu nimeiangalia kwa macho 2;-
a. Kweli mpiga mizinga ana shida,
kama ulivyosema maisha ni kupanda na kushuka, leo unacho kesho huna, mtu wa namna hii hata akikupiga mzinga unatoa kwa moyo mkunjufu maana unajua mpaka kaniomba kweli kakwama...

Saa nyingine kama mtu hana ajira kwa nini asipige mzinga fedha za biashara? Hata mtaji wa kuuza maji.....

B. Aina ya pili ni wale wapiga mizinga naturare, yaani hata awe na hela mfukoni lazima akupige mzing, hawa ndo wanaokera, hata ukiomwambia haisaidii sana..... Nikupe mfano mmoja kuna mtu akiniona mimi au yoyote katika marafiki lazima akupige mzinga, mpe sasa hiyo hela bila aibu atakwambia naenda saluni.... Yaani mpigwa mizinga yeye hataki kwenda saluni? Na mtu wa namna hii ambaye unatoa ulichonacho yeye anatapanya inauma........

Kwa hiyo kwa upande wangu inategemea na aina ya mpiga mizinga kwa kweli, mwingine ana shida, hana kipato au kipato kimeshuka n.k hapo kumsaidia haina shaka.....

Ila siungi mkono mtu akupige mzinga halafu aende baa, au akalipe gest.....

BADILI TABIA ninachosema mimi kwa nin usimwambie direct?alafu kumbuka shida hazina tabia unaweza ukapiga mzinga hata mti chezeya shida wewe,alafu kuna emegency kama za kukutana mahala,kwanza ujue mpaka mtu anakuja kukulia shida ujue amekuthamin na kukuheshimu,haifai kutuponda tusiokuanavyo.
 
Last edited by a moderator:
Kuna wengine wanaleta usista duu na kukandya kazi za maboksi huku hawana kazi. Lakini kila mara wanakupiga mizinga....ukiwaambia kwa nini usitafute hata kazi ya kuchoma chipsi anajifanya matawi ya juu...eti hataki.

Akiwa na shida ana kuja kwako kukuomba umsaidie...sasa unabaki unamshangaa. Kazi hataki, zingine anaziponda, lakini hachoki kuomba hela toka kwa hao wanaofanya hizo kazi anazoziponda yeye.

Watu kwa kulazimisha kuonekana matawi ya juu...shenzi kabisa.

Ngoja nipitie CV za visista du vya JF afu nimpelekee mpwa majina kadhaa nimjue huyu mpiga mizinga wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom