Wajiuzulu wote walio tuhakikishia kuwa Mambo haya hayatajirudia tena

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Miaka 16 iliyopita Mv. Bukoba ilizika zaidi ya watu 1,000 wakatwambia haitajirudia tena.

Na miezi kadhaa imepita Mv. Isle lender Ikazika zaidi ya watu 400 wakatwambia haitajirudia tena

Jana meli nyingine imezika zaidi ya watu 50 sijui watatwambiaje.

Kwanini wasijiuzuru?
 
Serikali imejipanga AJALI KAMA HII HAITAJIRUDIA TENA!zanzibar kuna sumatra?
 
ESTIMATION YA WATU 50 SI SAHIHI KABISA,
IVI MWAJUA IYO MELI HAINA OFISI HAPA DAR?? TIKETI ZILIKUWA MIKONONI MWA WATU KAMA MAAGENT WAKIZIUZA, MAANA YAKE NI KUWA ILO DAFTALI LA ABIRIA WOTE WALIOSAFIRI NI KAMA HALIPO, THIS IS ACCORDING YO TBC HABARI JANA AMBAO WALIIKOSA OFISI BAADA YA KUTAKA KUJUA IDADI YA ABIRIA WALOKUWEMO.

HII SERIKALI INA MAKUSUDI MABAYA SANA DHIDI YA WATU, VIPI MELI INAPAKI KATIKA GATI WAKATI HAINA OFISI?? KIMEO HIKI HATA MWAKYEMBE LAZIMA ALIPULIWE, LABDA KAMA NI MAMBO YA MUUNGANO AMBAO LAZIMA KUULINDA IVYO BUDI KUYAFUNIKA MAMBO AYA ILI KUUDUMISHA MUUNGANO,

AAAAH HII NDIYO TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYo
 
Tatizo mnamsahau Mwenyezi Mungu ,hivi wanapokuwa kuna madaktari bingwa na wazoefu wa kazi zao ,mnataka kutuambia hafi mtu ??? Na pale anapokufa ,hawa hutakiwa kujiuzulu ??

Mbona mimi naona ni jambo la kawaida !! Oneni kazi ya Mwenyezi Mungu wale walioandikiwa kufa wamekufa na waliokuwa siku zao zipo wamepona ,mnahoji kitu gani ?

Yaani Mwenyezi Mungu amesema hazidishiwi wala hapunguziwi muda wa kuishi kiumbe muda wake wa kufariki ukifika.Kila kitu ontime popote uwapo.Kuna ajali mbaya sana za magari ndege treni na vinginevyo na watu wanapona ,kuna gari ukionyeshwa na kuambiwa wtu wamepona huwezi amini.

Zaidi poleni wafiwa na mliopona na mlio hai msiwache kumkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu kila wakati.
 
Serikali ni dhaifu? au ni ya dhaifu!
Hata Gongolamboto walisema hivyohivyo.
 
nilichosikia kwenye taarifa ya habari meli imepinduka kutokana na wimbi kubwa lililosababishwa na upepo mkali........hivi hawa wa hali ya hewa kwa nini hawakutoa tahadhari kuhusu huo upepo..........wakati hali ya upepo ilionekana tangia asubuhi.

kuhusu ofisi na mengineyo yanabidi yafwatiliwe na wahusika wachukuliwe hatua.
 
Tatizo mnamsahau Mwenyezi Mungu ,hivi wanapokuwa kuna madaktari bingwa na wazoefu wa kazi zao ,mnataka kutuambia hafi mtu ??? Na pale anapokufa ,hawa hutakiwa kujiuzulu ??

Mbona mimi naona ni jambo la kawaida !! Oneni kazi ya Mwenyezi Mungu wale walioandikiwa kufa wamekufa na waliokuwa siku zao zipo wamepona ,mnahoji kitu gani ?

Yaani Mwenyezi Mungu amesema hazidishiwi wala hapunguziwi muda wa kuishi kiumbe muda wake wa kufariki ukifika.Kila kitu ontime popote uwapo.Kuna ajali mbaya sana za magari ndege treni na vinginevyo na watu wanapona ,kuna gari ukionyeshwa na kuambiwa wtu wamepona huwezi amini.

Zaidi poleni wafiwa na mliopona na mlio hai msiwache kumkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu kila wakati.

HOJA YAKO NI YA KWELI, LAKINI YA KAIZARI MPE KAIZARI NA YA MUNGU MPE MPE MUNGU, MAANA KUNA AJARI ZA BAHATI MBAYA NA AMBAZO ATA MAZINGIRA YA AJALI IZO UNAONA KABISA NI UZEMBE NA WAMESABABISHA WATU FULANI, MFANO ILE MELI YA ISLANDER WATU WALIJAZWA MPAKA WAKAKALIANA, MELI ILIZIDIWA HATA IKALALIA UPANDE MMOJA,

KUMBUKA MV BKB, ILE MELI ILIKUWA MBOVU KITAMBO LKN BADOO SERIKALI ILIKUWA IKIIPIGISHA MZIGO, HALAFU USEME NI BAHATI MBAYA

WEWE USIMSINGIZIE MUNGU KABISA, JAPO KILA MTU SIKU IKIFIKA LAZIMA UONDOKe
 
Miaka 16 iliyopita Mv. Bukoba ilizika zaidi ya watu 1,000 wakatwambia haitajirudia tena.

Na miezi kadhaa imepita Mv. Isle lender Ikazika zaidi ya watu 400 wakatwambia haitajirudia tena

Jana meli nyingine imezika zaidi ya watu 50 sijui watatwambiaje.

Kwanini wasijiuzuru?

Hukuwaelewa vizuri waliposema haitajirudia tena,Walimaanisha Mv.Spice Islander haitajirudia kuymama,sio meli zingine mkuu
 
abiria walikuwa 282 na manahoza 9..walio okuolewa wakiwa hai mpaka sasa ni 124, kwa hiyo walio kufa si 50 tu...
 
Back
Top Bottom