Wajinga waliwao ni wao ! Ama sie ndugu zao! ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,776
Masiku machache nikiwa Uvira , (Congo Drc) nikapata kuwauliza wenyeji wangu , kitu ambacho huku kwetu si kawaida ukute nyumba ina umeme , na kisha haina mita .

Kwani baada ya kuzungusha kwng macho ndani na nje ya nyumba zilizopata ingia sikuwahi ona kitu mita .

Majibu niliyopewa :
"Hapa sisi bakongo hakunaga hiyo makitu ya uizi wa kuibia washenzi . (Note washenzi kicongo si tusi , kwao washenzi ni wenyeji , mshenzi ni mwenyeji , pia utasikia kuku wa kishenzi ni kuku wa kienyeji n . k)
Hapa mshenzi haibwi ! Wakongo tulikataa mita , unajua kama yule kampuni yakuuzisha sisi umeme , kama anakufungisha mita , ile mita yeye kampuni anainunua kwa faranga .
Na hawezikubali hiyo faranga ya mita ikule kwake! Itakukula wewe mwenye umefungishwa mita , price ya umeme itakua juu"

Kwa ufupi mf. Hai ni kama vile ukute nyumba mbili zinapangishwa , moja ina fenicha ndani , na nyingine haina .
Lakini ukubwa wa nyumba zote unafanana .
Ile yenye fenicha lazima bei yake itakua juu .
Ingawaje fenicha ni za mwenye nyumba .

Wakongo wanalipa umeme kwa makadirio , imekadiriwa kila nyumba , inatakiwa iwe na vitu gani vya kutumia umeme .
Na nyumba zote zinalipa rate 1 .
Wewe kama una vitu vichache vya kutumia umeme , hiyo ni hasara yako .

Kwa hili sisi na wao , wepi wanaliwa ?
Maisha bora kwa kila Mtanzania .
 
Mkuu Judgement wabongo tunaibiwa tena mchana kweupee, bacongo banafaidi
 
Mkuu Judgement wabongo tunaibiwa tena mchana kweupee, bacongo banafaidi

Sio siri , yako mambo hua natamani nilie! Lakini wa kumlilia simjui !
Mf. Niliwahi nunua betri mbili za evaredy Kisumu zilikaa redioni mwezi na wiki 1 !
Hii mineshno ya hapa wiki 1 unatupa !
Huu ndy type ya wizi unaonifanyaga nitamani kuhama nchi .
 
Sio siri , yako mambo hua natamani nilie! Lakini wa kumlilia simjui !
Mf. Niliwahi nunua betri mbili za evaredy Kisumu zilikaa redioni mwezi na wiki 1 !
Hii mineshno ya hapa wiki 1 unatupa !
Huu ndy type unaonifanyaga nitamani kuhama nchi .

Unataka kuhamia wapi? Huko Congo au?
 
Tukiacha maskhara ...seriously tunahitaji kufanya system overhaul ya kindakindaki, nobody cares n everybody is complaining including top leadership....!inaumiza mno nchi iko mnadani na makuwadi wa soko huria wanapigana vikumbo kukomba kila wanachoweza kuchukua

Tuache tu kama ilivyo tuko CC, Ngoja maisha tuyasongeshe
 
Ni ukweli usiopingika kwamba watz tunaumizwa sana na haya mafisadi ya CCM. Umeme unapanda bei kwa 68% lakini umeme wenyewe ni wa kulenga kwa manati. Jamani, tunapaswa tuache kulalamika, tufanye jambo mwaka 2015 ili kujinasua kutoka kwenye utumwa huu wa maCCM--ambao tumejitakia wenyewe kupitia sanduku la kura.
 
C.C.M as C.C.M mie ubaya wake siuoni!
Watu waliomo kwenye C.C.M ndiyo nitakubali wana matatizo! Na ndiyo waliyotufikisha hapa tulipo
Mtaani kwetu kuna Mzee anaitwa JUMA MNZINZI (maarufu Mz. Mzinzi)
Huyu Mzee jina lake na mwenyewe ni tofauti kabisa!
Ni mtu mwenye kujiheshimu na kuheshimika .
Wahukumiwe waliomo C.C.M waliyotufikisha hapa .
 
kumbe bamutu bacongo anafaidi.....

Kufaidi ni kweli banafaidi !
Walichonibakiza hoi ni kwenye mpishano wa lugha!
Mayai ya kishenzi ndiyo mayai ya kienyeji .
Afu kuna Viazi vya kishenzi ndiyo viazi vikuu.
Viazi mbatata wanaita viazi vya kiungwana na hivyohivyo kuna Kuku wa kiungwana , Mayai ya kiungwana n . k
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom