Judgement
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 10,327
- 4,779
Masiku machache nikiwa Uvira , (Congo Drc) nikapata kuwauliza wenyeji wangu , kitu ambacho huku kwetu si kawaida ukute nyumba ina umeme , na kisha haina mita .
Kwani baada ya kuzungusha kwng macho ndani na nje ya nyumba zilizopata ingia sikuwahi ona kitu mita .
Majibu niliyopewa :
"Hapa sisi bakongo hakunaga hiyo makitu ya uizi wa kuibia washenzi . (Note washenzi kicongo si tusi , kwao washenzi ni wenyeji , mshenzi ni mwenyeji , pia utasikia kuku wa kishenzi ni kuku wa kienyeji n . k)
Hapa mshenzi haibwi ! Wakongo tulikataa mita , unajua kama yule kampuni yakuuzisha sisi umeme , kama anakufungisha mita , ile mita yeye kampuni anainunua kwa faranga .
Na hawezikubali hiyo faranga ya mita ikule kwake! Itakukula wewe mwenye umefungishwa mita , price ya umeme itakua juu"
Kwa ufupi mf. Hai ni kama vile ukute nyumba mbili zinapangishwa , moja ina fenicha ndani , na nyingine haina .
Lakini ukubwa wa nyumba zote unafanana .
Ile yenye fenicha lazima bei yake itakua juu .
Ingawaje fenicha ni za mwenye nyumba .
Wakongo wanalipa umeme kwa makadirio , imekadiriwa kila nyumba , inatakiwa iwe na vitu gani vya kutumia umeme .
Na nyumba zote zinalipa rate 1 .
Wewe kama una vitu vichache vya kutumia umeme , hiyo ni hasara yako .
Kwa hili sisi na wao , wepi wanaliwa ?
Maisha bora kwa kila Mtanzania .