Pape
JF-Expert Member
- Dec 11, 2008
- 5,488
- 79
Hivi jamani kila siku magazeti yanatangaza kuhusu hawa watu matapeli ambao wanatumia ujanja wa kuwalaghai watu kwamba wanafanya biashara! Hawa matapeli huja na 'gia' kwamba uwape pesa fulani kidogo halafu wakupe faida! Wabongo bado tu wanakamatika tu! Haya...wabongo acheni tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka! Mambo sio rahisi kama unavyofikiri! Watu wameshajua kwamba wengi wa wabongo ni 'mazoba' kwahiyo ndio maana kila kukicha wanakuja na mbinu tofautitofauti! We jiulize kweli dunia ya sasa mtu akupe faida wewe tu hivi hivi? Aaah haiingii akilini! Asiyesikia la mkuu huvunjika guu! Amkeni!