Wajibu wa kampuni za gesi na mafuta kwa jamii Tanzania

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
WAJIBU wa kampuni zilizowekeza katika sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania kwa jamii, unatafsiriwa kuwa ni vitendo vya hiari ambavyo vinafanywa na kampuni hizo kwa lengo la kuimarisha maisha ya wananchi au kupunguza madhara hasi ya shughuli zinazotokana na miradi ya kampuni hizo katika maeneo ambayo zinaendesha shughuli zao.

Matendo ya hiari ni yale ambayo yanakwenda mbali ya matakwa ya kisheria, mikataba, na makubaliano yaliyoko kwenye leseni.

Programu za uwajibikaji kwa jamii mara nyingi zinajikita kwenye uwekezaji wa miundombinu ya kijamii, kuendeleza rasilimali watu na shughuli nyinginezo na kwa zaidi ya miongo kadhaa, utaratibu huo umechukuliwa kama msukumo wa maendeleo endelevu.

Ikumbukwe kwamba ukuaji wa muda mrefu wa uchumi katika jamii unahitaji utekelezaji imara wa kanuni za biashara zenye tija kwa jamii.

FikraPevu inaamini kwamba, ingawa dhana ya uwajibikaji kwa jamii kwenye sekta ya mafuta na gesi bado mpya nchini Tanzania, dhana hiyo kwa ujumla wake imekuwa ikitekelezwa kwenye sekta nyingine za uchumi kwa miaka mingi sasa.

Soma zaidi hapa=> Wajibu wa kampuni za gesi na mafuta kwa jamii Tanzania | Fikra Pevu
 
Ndio Gesi imepanda kwa ujazo wa ml 1000 kwa 0.4.....

This is real Fact, angalia budget yote, soma mstari kwa mstari...Watanzania acheni uvivu wa kusoma...

Gesi imepanda, so jadili madhara kwa misitu

Ndio maana tuna wasomi wa PHD na Maprofesa lakini mikataba feki wanasaini
 
Back
Top Bottom