Wajasiriangono!!

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Wanawake wanaofuata mali China

ijumaa wikienda
pix.gif
Uwepo wa wajasiriangono hao ndiyo zao la maduka mengi madogo madogo ya kuuza bidhaa kutoka China ndani ya Jiji la Dar na mikoa mingine, hususan nguo, viatu na vipodozi.

Gazeti ‘the Biggest IQ’ Ijumaa Wikienda ndilo pekee linaloweza kuthubutu na kuanika uchafu wote unaofanywa na baadhi ya wanawake wanaounga msafara wa wajasiriamali kwenda China ambapo wakiwa huko hugeuka wawekezaji wa ngono.

Mwandishi wetu aliyerejea ‘juzi-kati’ nchini akitokea kwenye Jiji la Guangzhou, China ana ripoti kamili ya wanawake hao wanaoichafua sifa njema ya Tanzania kwenye himaya ya Rais Hu Jintao.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa paparazi wetu, wanawake wengi wanaokwenda China hupendelea kufikia kwenye Jiji la Guangzhou ambako huweka makazi yao kwenye hoteli za Dongfen, Shushanlo na Baowani.

Uchunguzi huo umebaini kuwa wanawake wengi wakifika katika hoteli hizo, hupanga chumba kwa kushirikiana kisha kuanza kujiuza kwa wanaume ambapo kwa kupitia biashara hiyo, huweza kujiingizia kipato cha kuwawezesha kununua bidhaa za kujaza kwenye maduka yao.

Imebainika kuwa wakifika hotelini, hulipia chumba kwa fedha za China, Yuan RMBI 200 ambazo ni sawa na Shilingi 40,000 za Kitanzania na hutoa huduma ya chapchap a.k.a short-time kwa Yuan RMBI 100 (shilingi 20,000) kwa kichwa.
Kutokana na hali hiyo, wajasiriangono hao hujitahidi kwa kadiri wawezavyo kuwahudumia wateja wengi ili kujiingizia kipato kikubwa, hivyo kuifanya safari yao kuwa na mafanikio.

“Kila wanavyojiuza, malipo yao huyatumia kununulia bidhaa kama nguo, viatu, vipodozi, dawa za nywele, ngozi na vitu vingine. Hununua taratibu na wakipata mzigo wa kutosha ndiyo hurejea Bongo,” inasema ripoti hiyo ya mwandishi wetu.
Uchunguzi zaidi wa mwandishi wetu umebaini kuwa wanawake hao wa Kitanzania kwenye kazi yao ya kujiuza, wateja wao wakubwa ni Waafrika wanaoishi nchini humo kutoka Nigeria, Mali, Senegal na baadhi ya Watanzania.

Akiwa jijini Guangzhou, paparazi wetu alizungumza na mhudumu mmoja wa Hoteli ya Shushanlo ambaye alisema kuwa pamoja na kwamba hivi sasa mambo yanaonekana kwenda sawia kwa Watanzania, lakini huko nyuma biashara ya ngono ilikuwa inawalipa zaidi.“Kwa huduma ya dakika 30, mwanamke wa Kitanzania alilipwa Yuan RMBI 200 (shilingi 40,000 au dola 30) lakini baada ya soko kuvamiwa na wanawake kutoka Rwanda na Uganda, thamani ilishuka ndiyo maana sasa hivi wanachukuliwa kwa Yuan RMBI 100,” alisema mhudumu huyo (jina tunalihifadhi).

Ripoti ya mwandishi wetu inaongeza: “Japo si wote wanaojiuza na kuendesha maduka yao kwa jeuri ya miili yao lakini hali ni mbaya, kwa wanaume wenye wake zao ambao wanakwenda China kufuata bidhaa za biashara ni vema kuangalia nyendo zao. Hali ni mbaya.

“Kumbe maduka mengi yanayochomoza kama uyoga Dar na kwingine, hayatokani na nguvu ya ujasiriamali tunayoijua bali ni faida ya miili yao. Wanawake hao wanaichafua Tanzania.”

Gazeti hili linalaani vikali vitendo vya wanawake hao na linawataka kutambua utu wao kuliko kitu kingine chochote. Maradhi ni mengi lakini pia fedha si kila kitu katika maisha. Mhariri
 
Hatimaye nimeona umuhimu wa kubadili jina la BWABWA (nawashukuru wote walonipa ushauri nasaha kama Nguli, Paka Jimmy na wengineo), na nitatumia jina la BOFLO, kabla sijabadili, ningependa niwashirikishe wadau kama kuna jina lolote nanyi kama mnapendekeza nilitumie, nitalitumia.

~Psalm 23 - The Lord is My Shepherd



The Lord is my shepherd; I shall not want.
He maketh me to lie down in green pastures: he leadeth me beside still waters.
He restoreth my soul: he leadeth me in the
paths of righteousness for his name's sake.
Yea, though I walk through the Valley of the
Shadow of Death, I will fear no evil: for thou art
with me; thy rod and thy staff they comfort me.
Thou preparest a table before me in the presence
of mine enemies: thou anointest my head with oil;
my cup runneth over. Surely goodness and mercy
shall follow me all the days of my life: and I will dwell
in the house of the Lord for ever.
 
mi nafikiri kwa wanawake wafanyabiashara ni kawaida kupata bwana wa "kuwasaidia" wakati wa safari zao za kibiashara na hii imewasaidia kuweza kujiwekea akiba na kukuza mitaji. tutake tusitake, hii ni moja ya siri kubwa sana ya mafanikio ya kibiashara ya wanawake wachuuzi wa bidhaa
 
Tumia jina la "Tundu Dogo" au "Jicho Lisiloona"


Kha! Afdhali asibadili kabisaaaaa abaki nalo kama ndo hivyo!


Oke turudi kwenye topiki; I have my doubts on this; hao si wajisiliamali ; hao ni malaya; huwezi kujaza duka kwa kipato hicho then inamaana watakaa huko mwaka mzima!:D
 
Back
Top Bottom