Wajasiriamali wanawake wahofia usimamizi wa jeshi katika sakata la korosho Tanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Wanawake wajasiriamali wanaoshughulika na kubangua korosho nchini Tanzania wamelalamikia mpango mpya uliotangazwa na rais Magufuli ambapo sasa jeshi la nchi hiyo litasimamia biashara shughuli hiyo.

Wanawake hao wanasema kuwa hatua hiyo itawanyima fursa ya ununuzi wa kiwango cha kawaida kwa lengo la biashara ndogo ndogo kwani, wana wasiwasi kwamba huenda jeshi likabadili kabisa mfumo wa uuzaji korosho tofauti na walivyo zoea.

Hapo jana ikiwa ni kabla ya muda uliowekwa kwa wafanyabiashara kujiorodhesha ili wanunue korosho ya wakulima mkoani Mtwara, rais alibadili mawazo yake na kuamua kwamba wafanya biashara hao hawatanunua tena korosho hiyo, akihoji kwamba walikuwa wapi.
 
Back
Top Bottom