Uchaguzi 2020 Wajasiriamali wanawake Mzimuni Kinondoni wasema Magufuli tena 2020

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Leo Tarehe 11 Oktoba 2018 kumefanyika mkutano wa wanawake wajasiliamali takribani 100 Kata ya Mzimuni Dar es salaam, na kuhudhuriwa na Bi Aziza Mohamed Ashrafi Mwenyekiti wa UWT, Sunnah Kambi Katibu wa UWT na Ndg, Mohammed Daudi Dole Mwenezi wa CCM Kata ya Mzimuni na Bw. Paul Charles Afisa Maendeleleo Kata ya Mzimuni.

Mgeni rasmi katika mkutano huo ni Afisa wa CCM Makao Makuu Ndg Said Said Nguya kwa niaba ya Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Katika mkutano huo, Ndg Said Said amewaeleza Wakimama hao kuwa CCM inatambua jitihada zao, inaziunga mkono, na Chama Cha Mapinduzi kupitia Ilani ya Uchaguzi ya 2015 - 2020 imewawekea mazingira mazuri na wezeshi wajasiriamali wadogo na kwa upekee wakinamama.

Kwa upande wao, Wanawake Wajasiriamali wa Kata ya Mzimuni wameeleza mbele ya Mgeni rasmi kuwa, wanakipenda Chama Cha Mapinduzi, wameahidi 2020 wanakazi moja tu, kuhakikisha ushindi mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi kupitia kwa Daktari Ndg yetu John Pombe Joseph Magufuli unapatikani.

Hakika siku ya leo imefana sana!

Imetolewa na;
UWT Kata ya Mzimuni.
IMG-20181011-WA0111.jpeg
IMG-20181011-WA0110.jpeg
 
UWT inapaswa kuitwa Umoja Wa Wanawake wa CCM Tanzania.

Huyu aliyeletaga hili neno UWT alikuwa mpumbavu tu ili kuwasubaisha wasiokuwa na uelewa.

Hao wajasiriamali ulitegemea watasemaje mbele ya hao viongozi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom