Wajasiriamali wamtimua Waziri Nagu


BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,436
Likes
117,316
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,436 117,316 280
Wajasiriamali wamtimua Waziri Nagu

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAJASIRIAMALI zaidi ya 500 kutoka mikoa 17 nchini na nchi jirani za Kenya na Uganda, jana walimtimua kwa hasira Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Mary Nagu, ambaye aliwatembelea katika viwanja vya maonyesho vilivyopo katika viwanja vya Nane Nane mjini hapa.

Wafanyabiashara hao walifikia hatua ya kumtimua waziri huyo, kutokana na hasira za kususwa na viongozin wa serikali tangu kuanza kwa mkutano wa nane wa Leon Sullivan, Jumatatu.

Waziri Nagu aliokolewa na polisi kutoka kwa wananchi hao wenye hasira, ambao baadhi yao walitishia kumdhuru wakidai kuwa serikali imewasababishia hasara kubwa kwa kuwaleta Arusha kwa ajili ya maonyesho na kisha kuwasusa.

Aidha, wajasiariamali hao wametishia kuandamana leo hadi ikulu, kumuona Rais Jakaya Kikwete, wakilalamikia kutapeliwa katika ushiriki wa maonyesho ya biashara ya kimataifa.

Awali, wakizungumza na waandishi wa habari na Mbunge wa Ngorongoro, Vincent ole Telele, wajasiriamali hao walisema hadi jana, maonyesho yao yalikuwa hayapati watembeleaji wa kutosha miongoni mwa washiriki wa mkutano wa Leon Sullivan.

Walisemsa hali hiyo inawafanya wahisi kuwa wametapeliwa na serikali, kwani wao walifika Arusha kushiriki maonyesho hayo baada ya kuhamasishwa mikoani na maofisa wa serikali kuwa katika maonyesho hayo watapata biashara kutoka kwa Wamarekani hao.

Wajasiriamali hao wanaotaka kuandamana wapo katika viwanja vya Chama cha wakulima (TASO), ambako maonyesho yao yamedorora licha ya uwanja kuandaliwa na kuwekewa huduma muhimu zikiwepo taa za usiku. Baadhi yao, wanaouza vyakula vya asili, jana walilazimika kuvimwaga baada ya kuanza kuharibika.

Khadija John, kutoka mkoani Iringa, Rahel Fredy wa Manyara na Mariam Hamadi wa Zanzibar, walisema kwa nyakati tofauti kuwa wamefika katika maonyesho hayo wakitarajia kutembelewa na wageni, lakini badala yake wageni hao kutoka Marekani juzi jioni wamepelekwa katika kituo binafsi cha Cultural Heritage cha mjini hapa.

“Sisi tumekuja huku Arusha baada ya kuhamasishwaa mikoani kuwa kuna maonyesho na Wamarekani na washiriki wengine wa mkutano watakuja kututembelea lakini tunashaa kwua hadi leo, siku moja kabla ya mkutano kwisha, hatujatembelewa na wageni hao,” alisema Hamadi.

Hamadi alisema tangu wafike mkoani Arusha wakitokea Zanzibar, hawajauza bidhaa yoyote na wamekuwa wakiishi kwa taabu kutokana na kutotembelewa na watu katika mabanda yao.

“Walikuja hadi Zanzibar wakatuomba tuje huku, tena tutengeneze business card nyingi, tumekuja nazo hata hao wa kuwapa hawapo,” alisema Hamadi ambaye ni mwanakikundi cha BAMITA.

Alisema sasa wahajui hata watarudi vipi Zanzibar kwani hakuna biashara walizofanya na hakuna hata watazamaji ambao wangeweza kuona bidhaa zao.

Khadija John, ambaye ni mkurugenzi wa kikundi cha KHG cha Iringa, ambacho kinajihusisha na bidhaa za ufumaji, alisema tangu wamefika Arusha wameshindwa kuuza bidhaa zao.

“Kama hali hii ikiendelea kesho itabidi tuandamane twende kwa rais, aeleze nani atalipa gharama zetu,” alisema John.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda yote, Telele alisema anashangazwa na maofisa wa wizara zinahohusika na mambo ya ndani, biashara na utalii kuwatelekeza wajasiriamali hao.

Hadi jana, Telele alionekana kuwa ndiye kiongozi pekee wa juu kutembelea maonesho hayo tangu yalipotembelewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kuridhishwa na maandalizi, alisema kinachoonekana ni wajasiriamali hao kutelekezwa.

“Hata mimi namuomba Rais Kikwete kuwaagiza wahusika kuwaleta hapa washiriki wa Sullivan badala ya kuwapeleka katika maduka binafsi,” alisema Telele.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Mkoa wa Arusha ya maonyesho hayo, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda, wakulima na wafanyabiashara wa Mkoa waArusha, James Kangaro, naye alionyesha kushangazwa na hali hiyo.

“Mimi binafsi nimeonana na Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo na kumueleza hali hii, lakini anasema watakuja tu na tunashangaa kuambiwa jana walikwenda Cultural Heritage na kuwatelekeza wajasiriamali hawa,” alisema Kangaro
 
tgeofrey

tgeofrey

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2008
Messages
533
Likes
1
Points
35
Age
43
tgeofrey

tgeofrey

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2008
533 1 35
Innovertive,invertivity And Creativity Yaani Uvumbuzi, Ugunduzi Na Uumbaji Nikazi Ngumu Sana Iwapo Serekali Itakuwa Inakaa Pembeni. Kama Serekali Inawatelekeza Hawa Watu Kweli Hii Ni Hali Ya Kusikitisha. Pia Waudhuriaji Wa Mkutano Huu Wanamalengo Yao Na Sisi Tuna Malengo Yetu Sasa Yakipishana Inakatisha Tamaa. So What Was Preemptive (epusha Au Epushisha) Measure.tumaini Geofrey
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
tukisema watu wameuziwa mbuzi kwenye gunia tutakuwa tumewaudhi?
 
Kilbark

Kilbark

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2008
Messages
568
Likes
49
Points
45
Kilbark

Kilbark

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2008
568 49 45
Tatizo letu ni kwamba tunaweka matarajio kabla ya tukio yaani tunakuwa zaidi optimistic na ndio maana watu wameanza kuichukia serikali ya muungwana kwa sababu hiyohioyo aliwaahidi maisha bora watu wakatarajia akipata tu ile ameapishwa kesho yake maisha yameshaanza kubadilika. Na matokeo yake ndio hayo.
 
Kite Munganga

Kite Munganga

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2006
Messages
1,366
Likes
148
Points
160
Kite Munganga

Kite Munganga

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2006
1,366 148 160
Kesheni mkisali watakuja tu
 
tgeofrey

tgeofrey

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2008
Messages
533
Likes
1
Points
35
Age
43
tgeofrey

tgeofrey

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2008
533 1 35
Tatizo letu ni kwamba tunaweka matarajio kabla ya tukio yaani tunakuwa zaidi optimistic na ndio maana watu wameanza kuichukia serikali ya muungwana kwa sababu hiyohioyo aliwaahidi maisha bora watu wakatarajia akipata tu ile ameapishwa kesho yake maisha yameshaanza kubadilika. Na matokeo yake ndio hayo.
hapo mzee naona dili ni ufisadi tuu maanda ndio linalipa haraka haraka
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,845
Likes
80
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,845 80 0
waziri mmoja akishapigwa watu wajua kama wananchi wamechoshwa na mipango yao isiyoona mbele.
alotayarisha mipango hiyo hasa ni nani?
 

Forum statistics

Threads 1,235,498
Members 474,615
Posts 29,224,685