Wajasiriamali na waongoza njia mambo yanaendaje wakati huu wa corona

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Hakuna sherehe hapa inakula kwa MC wa sherehe na kumbi za starehe

Hakuna imports hapa kwa wale wazee wa kwenda china kuchukua mzigo,sasa mnauza kitu gani baada ya stock kwisha

Wanamuziki wa bongo flavour ,Hakuna matamasha wala kwenda kupiga muziki kwenye kumbi ulaya au hapa nyumbani

Suppliers wa vyakula kwenye migahawa mashuleni na vyuoni hakuna

Makongamano ya morali na kutiana moyo toka kwa wajanja wale motivotional speakers au waongoza njia hakuna

Wale Dada zetu wa kujifanya bongo movie na kushinda mahotelini chali

Hivi zile picha za kujiremba kuonyesha maisha mazuri zimepungua sana instagram au ilikuwa fake life

Tushare kila mtu anapambana vipi,

Hofu kwa wafanyakazi kuwa serikali au makampuni yanaelekea kukosa mapato na kushindwa kulipa mishahara imekaaje huko?

Angalia miezi mitatu mbele toka sasa kama corona itaendelea hali ya biashara na uzalishaji itakuwaje

Jaribu kufikiria familia yako miezi mitatu ijayo kama corona itaendelea na lockdown zitaendelea huko kwa wenzetu itakuaje mapato ya serikali na biashara,kifuatacho
 
Huu ndo muda kuonesha gape kubwa kati ya matajiri na masikini!
Wengi tuko kwenye state ya kushangaa maisha yanavyobadilika kila kukicha..wengine ndo wanatumia huu muda kukunja note😥😥!..haki ya nani tutakoma!
 
Hivi wale wasanii waliokua wanapiga picha na mahela vp yameisha au ndo zimeyeyuka #Maisha yanaenda kasi kila mtu amekua na nidhamu ya fedha.Mungu ibariki Tanzania
 
Kuna kitu Walimwwngu tunajifunza hapa. Hili la ugonjwa wa Corona ni moja ya darasa kwetu hapa duniani!

Kuna wakati matajiri na masikini tutakuja kuongea lugha moja tu.

God is good, time will tell.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom