Wajapan kujenga shule ya uhandisi wa tiba jijini Dodoma

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Kampuni ya Japan ya Association of African Economic Development (AFRECO) imeonesha nia ya kujenga chuo cha uhandisi wa tiba (School of Medical Engineering) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kupunguza tatizo la wataalamu wa tiba na vifaatiba nchini.

Rais wa kampuni hiyo, Bwn. Tetsuro Yano ameeleza hayo alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Tunis, Tunisia ambako anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaohusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD8).

Bw. Yano alisema walipokuja Tanzania waligundua kuwa kuna vifaa vinavyonunuliwa lakini vinashindwa kufanyiwa ukarabati pindi vikipata hitilafu sababu hakuna wataalamu. “Kwa kuzingatia hilo tumeona haja ya kuanzisha chuo cha uhandisi tiba ili tuweze kufundisha wataalamu watakaokuwa wakifanya matengenezo ya vifaa badala ya kuagiza mafundi kutoka nje, au kuviacha visitumike tena”, alisema.

Pia alimweleza Waziri Mkuu kwamba walishapokea maombi kutoka UDOM ya kupatiwa basi la kutoa tiba lenye vifaa mahsusi vya hospitali (mobile clinic bus) ambalo litakuwa likisaidia kutoa huduma kwenye vijiji vya jirani na chuo hicho.

Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Sanaa cha Kurashiki cha Japan, Dkt. Tomotaka Naramura alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana nia ya kufungua chuo hicho mwaka 2023.

UDOM.jpeg
 
Basi tunakuja kufanyiwa medical experiments
Wacha nikuandikie hii

"Medical engineering refers to the process of checking medical equipment to make sure it's working properly and is safe to use"
 
Hii ni nzuri naunga mkono. Tuone kama itasaidia maana unakwenda hospital ya serikali unaelezwa kifaa kimeharibika hivyo kapime kwingine uje kuanza matibabu
 
Hii ni nzuri naunga mkono. Tuone kama itasaidia maana unakwenda hospital ya serikali unaelezwa kifaa kimeharibika hivyo kapime kwingine uje kuanza matibabu
Hiyo kozi inatolewa hapa Tanzania na wataalamu wapo. Kufungua chuo sizani kama itamaliza tatizo, labda wakitoa ajira wawakumbuke haswa
 
Basi tunakuja kufanyiwa medical experiments
Itakuwa ni bora kuliko kubishana Yanga na Simba Diamondi na Kiba na Mabasi gani yanawahi kuingia Sauli au You tong...

Tena nadhani Wajapani waanze kuchunguza Ubongo kwanza na athari za Ugali.
 
Udom imeshaoza....wangefanya chuo hiki kijitegemee wasikiharibu na kasumba za Udom
 
Back
Top Bottom