Wajamani, "it feels good 2 know ur limits."

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Waswahili hulonga..."penye chokochoko.."
Usiache kupapulizia papoe, pakitulia...
Basi ujue mambo yamejipa na ni shwari..
Pakiendelea kufurukuta basi elewa kazi ipo
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

Wengi huamini ukikaza musuli utafanikiwa,
Wengi hujidanganya, "the sky is the limit"
Wengi hujipooza, lolote lawezekana.............
Lakini ukweli wabakia tunayo mipaka ya nguvu..
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

Kauli na makeke huwa hayatupiti........
Tunapopigwa chini huanza kutafuta visingizio......
Lawama kibao kwa wengine, huku kwetu ni ukimya..
Hivi tatizo ni wao au ndoto zetu zisizotekelezeka?
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

Tambua mipaka yako utaishi kwa miraha..
Karaha kwako kando kwani utapanga mipango fanikika
Watakaokucheka zao ni arobaini kwani wataumbuka
Usitawaliwe na kauli za wengine ila misimamo yako
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

"Kisukari kubwa" na kiharusi kwako itakuwa mwiko
Kwa sababu unakula kulingana na mkono wako
Kujilinganisha ni mtego wewe sasa umeukwepa
Kwani kila mmoja alizaliwa kivyake-vyake..
Wajamani,
"it feels good 2 know ur limits."

I am beginning to feel like it is X-MAS..............
 
And the moral of the story is.......?

Nyani Ngabu.............usiniangushe......fasihi simulizi ilikupitia pande ipi?...................."just be yourself and you will do well..........."
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: kui
"Kisukari kubwa" na kiharusi kwako itakuwa mwiko
Kwa sababu unakula kulingana na mkono wako
Kujilinganisha ni mtego wewe sasa umeukwepa
Kwani kila mmoja alizaliwa kivyake-vyake..
Wajamani,

Ruta nani amekuudhi wajameni?
 
Ruta nimekumiss sana! Yaani umeshawahi kwenda Karagwe mapema namna hii kwaajili ya Xmass!

Ndallo Karagwe siyo kwangu......................nimekumiss pia.....................uko wapi saa hii tukanywe togwa hapo........Silent Inn
 
Ndallo Karagwe siyo kwangu......................nimekumiss pia.....................uko wapi saa hii tukanywe togwa hapo........Silent Inn

Ruta nipo jamaa yangu sema siku hizi nimebadilisha mapigo nimehamia Pub moja kama unaelekea kwa Idd yale maeneo ya Raskazoni Nzi wengi!
 
Ruta nipo jamaa yangu sema siku hizi nimebadilisha mapigo nimehamia Pub moja kama unaelekea kwa Idd yale maeneo ya Raskazoni Nzi wengi!

Ndallo....umesahau nzi kufa juu ya kidonda siyo haramu/
 
Last edited by a moderator:
Sio wewe peke yako, good to see him back!

to get such encomiums and acknowledgments from the lovely Kaunga...........it feels good inside out.................to say it in a mere whisper........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom