Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Sijui mama huyu kanifanyizia nini kwani najisikia amenielemea,
Tangia akiwa kinda nilimpenda kikwelikweli naye kujulishwa.....
Naye nahisi alinipenda japo hakunambia kiuwaziwazi........
Walakini wapambe wake walimjongelea naye kunitupia virago,
Wajamani huyu mama sasa habanduki mawazoni kwangu!
Kutokana na majukumu siko radhi kumshtua
Ninaamini naye huniwazawaza pamoja anipigia ganzi
Sijui ana nini huyu mama mbona anitawala hivyo?
Mengi hutafakari na hamu ya kurudisha siku kunizingira,

Sijui ni lipi ningeliboresha ili hadi leo tungelikuwa sote.
Najua yu mtaani akitesa na mwingineo bila zengwe
Mara kwa mara hutikisa kichwa kwa majonzi na kutaabika
Kisa nikumkosa kuwa ndani ya maisha yangu na kutojua la kufanya

La kushangaza ni kuwa hata wakati wa mahaba ni yeye kutia fora!
Nisipofanya hivyo sipatwi na mpango wa nyevu endelevu!
Hivi haya ayajua au mie tayari amenikitisha kwenye kapu lake?
Mie sitamtonya kwa kukhofu kuanzisha vagi....acha niteseke tu mwaya!

Inspired by this piquant narrative......I can't get her out of my mind
..........jisomee mwenyewe kama waujua umombo au ridhika na hamirojo yanguhttp://www.standardmedia.co.ke/rela...&cid=431&story=I can’t get her out of my mind