Waiuzayo Zanzibar ni hawa,ajaribu kulipoza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waiuzayo Zanzibar ni hawa,ajaribu kulipoza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jan 29, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by amini // 29/01/2012 // Habari // No comments

  [​IMG] Samia Suluhu
  MAFUTA, GESI YAZIDI KUUTIKISA MUUNGANOM
  Chanzo Mwanachi.
  Hakuna Shaka kuwa Samia na Bilali huenda wakawa upande wa Tanganyika na kutafautiana na ndugu zao kwa vile wana fupa kwa muda huu.
  Sunday, 29 January 2012 10:41
  Nora Damian
  SUALA na mafuta na gesi limeshindikana kutatuliwa katika kero 13 za Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar na kupangiwa kusubiri maelekezo kutoka ngazi za juu.
  Mawaziri wanaohusika na Muungano kutoka Tanzania Bara na Zanzibar chini ya Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal jana walikutana kwa saa kadhaa jijini Dar es Salaam katika mkutano uliojadili masuala hayo na baadaye kuibuka na taarifa iliyobainisha ugumu huo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu ndiye aliyepasua jipu la kushindwa kuelewana katika mafuta na gesi baada ya mkutano huo kumalizika jana jioni.Hata hivyo Waziri Samia, alisema wamefanikiwa kutatua kero sita kati ya 13 ndani ya Muungano huo.
  “Tumejitahidi kwa asilimia 75 kushughulikia kero mbalimbali lakini suala la mafuta na gesi tumeshindwa kuelewana hivyo tunasubiri maelekezo kutoka juu,”alisema Suluhu na kuongeza kuwa:“Hata suala la sheria ya uvuvi katika bahari kuu kutumika hadi Zanzibar, halikuridhiwa hivyo tutaendelea kulifanyia kazi,”alisema.
  Alisema Serikali za pande zote mbili itabidi zikae tena ili kujadili suala la mafuta na gesi kwani haiwezekani upande mmoja uendelee kufanya utafiti huku upande mwingine ukiwa umekaa kimya.
  Waziri huyo alisema pia wamekubalina Aprili mwaka huu pande mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar) zipeleke marekebisho ya sheria kwenye mabunge yao ili kuondoa kero ya usajili wa vyombo vya moto.
  Sululu alisema kuwa suala la mgawanyo wa misaada na mikopo tayari limetatuliwa na kwamba kwa sasa hakuna utata tena.
  “Hili la wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili tutafanya utafiti kwa sababu kuna malalamiko kwamba bado linaendelea,”alisema.
  Waziri huyo alisema wamekubaliana pia kuwepo na mfuko wa jimbo na kwamba sheria tayari imeandaliwa ikisubiri kupelekwa kwenye Baraza la Wawakilishi.
  Katika hatua nyingine, Waziri Suluhu alisema kuwa suala la Serikali kuwasilisha andiko katika Umoja wa Mataifa kudai kuongezewa eneo la ziada nje ya maili 200 za ukanda wa kiuchumi katika Bahari ya Hindi halimo kwenye kero za Muungano.
  Alisema kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje ya Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa hakuwa na taarifa kamili kuhusu suala hilo na kwamba alipaswa kwanza kwenda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kujua jinsi ilivyoshiriki katika suala hilo.
  Hivi karibuni Jussa alisema kwamba watapinga Umoja wa Mataifa (UN) kuiongezea mipaka Tanzania eneo la kiuchumi la bahari kuu kabla ya kupatikana muafaka kati ya Serikali ya Muungano na Zanzibar.Kwa muda mrefu suala la kero za Muungano limekuwa likipigiwa kelele na pande zote mbili hali iliyosababisha kuundwa kwa kamati ya kushughulkia kero hizo.
   
 2. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jamani.. hawa wana uhakika wa kuwepo mafuta na gas? Si wasubiri kwanza ifanyike 'test drilling' kujua kama mafuta yapo, na quality yake. Heh..!!
   
 3. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  its open secret ukanda wa pwani Tanzania inao deposits of trillions cubic meters natural gas hata kupelekea utabiri Tanzania is on verge of building gas economy. Usione pirikapirika za extension continental shelf iko kitu!
   
Loading...