idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,284
- 38,312
Waitara ameongea mengi,ila hili limenifikirisha zaidi.
Ameyasema hayo jana wakati wa kufunga kampeni za udiwani kata mojawapo huko Mbeya.
Amesema mwaka 2010 mara baada ya Chadema kuchukua jimbo, ulifika wakati wa kuteua mbunge viti maalum... wakati Sugu akitegemea jina litatoka ndani ya mkoa wa Mbeya hasa kwa kina mama wa kawaida.
Alishangaa kuletewa jina kwenye bahasha toka Dar la Mwana mama Naomi Kaihula makazi wa Kawe Jiji Dar kuwa mbunge viti maalum wa Jiji la Mbeya.
Kitendo hicho kilimkwaza sana Sugu hali iliyopelekea kwenda Makao Makuu Chadema kuhoji swala hilo, kuwa kwa nini jina halijatoka Mbeya kwa akina mama aliohangaika nao usiku na mchana kusaka kura.
Kabla hajajibiwa Sugu aliandika barua ya kujiuzulu Ubunge.. baadaye vikakaliwa vikao kumshawishi Sugu asijiuzulu na kumwahidi kuwa ushauri wake utazingatiwa 2015..
Watahakikisha mbunge viti maalum anatoka mkoa wa Mbeya, Mbowe pia akamsihi atulie jina lake litaingia kwenye Kamati Kuu ya Chama.
2015 Chadema wakashinda tena ubunge Mbeya, jina la viti maalum likatoka tena Dara (Sofia Mwakaganda) na sio kwa akina mama wa jiji la Mbeya kama walivyomwahidi 2010...kwa kuwa Sugu walimhonga kwa kumpa ujumbe Kamati Kuu safari hii hakuweza kuhoji chochote kuhusu jina kutoka Dar....
==========================
Binafsi nampongeza sugu kwa ujasiri aliouonyesha kwa kuwatetea wananchi wake hadi kufikia hatua ya kutaka kujiuzulu ubunge.
Pia ni vyema Chadema ijitafakari, mambo kama haya ndio yanafanya viongozi wengi kuhamia Chama tawala.....
Hili swala la viti maalum limeumiza majimbo mengi sana, akina mama wanapambana na polisi wanapigwa virungu wanamwagiwa maji ya washawasha halafu mwisho wa siku mnaambiwa jina limetoka Dar.