Uchaguzi 2020 Waitara: Nimeisambaratisha CHADEMA Ukonga, sasa nahamia Tarime Vijijini

Ujinga na jamaa atakuwa mjinga na mpumbavu. Ili umsambaratishe mtu au kikundi flani ni lazima ukwamishe mipango yao, sasa kwa kuwakwamisha viongozi halali walio chaguliwa na wananchi katika kutekeleza wajibu wa kuleta maendeleo kwa wananchi ni kutukwamisha sisi wananchi.
Waitara, usijisifie kwa hilo, tunahitaji hoja na sio kukwamishana.
Uimara wa Heche mnajifurahiasha tuu, hata kupata wenyekiti wa kanda ya Serengeti hakuweza kupata, alipigwa chini na mdada. Kama angekuwa maarufu kiasi hicho mnachosema asinge pigwa chini katika nafasi ya Uenyekiti wa kanda ya Serengeti, hicho kitu kisingetokea. amkeni amkeni.
 
Ufipa wanahaha kuokoa jahazi, ila DJ anawangusha sana, Ulevi, Uzinzi, ubabe na Kula ruzuku ya chama kimewakimbiza viongozi wengine na wanachama wa kawaida! CDM kimefia mikononi mwa DJ
Acha ubwege kwa Akili zako finyu unaona Neno DJ ni tusi wakati ni fani nzuri tu inayoleta kipato na wewe mwenyewe huzurula night club na Le mutuz ni madj huwafanya mtembee usiku, ruzuku ya chadema hailiwi kienyeji kama ruzuku ya CCM ambayo hutumika kuwahujumu chadema huku wajanja wachache wakila pesa nyingi kwa kisingizio cha kuifuta chadema, CAG alisema chadema wapo safi na sasa mmepeleka Takukuru mtaambulia patupu, ulevi uzinzi upo huko CCM mbona viongozi wa CCM wamezaa watoto na Shemeji zao, chadema haifi mikononi mwa mbowe wanajua boss zako ndiyo maana kutwa kuwabambikia kesi za kila aina kuwapiga risasi lakini chadema ipo na itadumu milele.
 
Ooh! Kumbe! Mi nilijua anataka kuwatumikia wananchi,kumbe ulikuwa unasambaratisha chama?!so,watanzania wa kawaida kuna kitu wamepata hususani maendeleo yyt kufuatia kuisambaratisha cdm?

Basi ni hivi,kama Mungu aishivyo,unamalizia awamu hii,na hutarudi! Kama Mungu aishivyo!u ll never ever! Na nakufuta!

Tunahitaji viongizi wanaojielewa ,maono mapya,ubunifu nk kwa ajili yamaendeleo,sio wanaosambaratisha wengine!

Sent using Jamii Forums mobile app
Waitara hakwenda CCM kuwatumikia wananchi yeye kaenda huko kwa masilahi yake kuwakomoa chadema
 
Mtu mzima kusema unasambaratisha upinzani amabao upo kwa mjibu wa katiba ni kutokojitambua. Mheshimiwa Magufuli angalia watu unaowapa uwaziri maana huyu naye kuitwa ni waziri ni shida. Sijui kama kwenye hiyo wizara amesaidia chochote.
Wizara wanajuuta kumjua ni mshamba sana utendaji wake wa kazi ni wa hovyo hovyo sana anapenda majungu majungu fitna ni mtu mjinga mjinga sana
 
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa mpaka sasa hivi amekwishamaliza kazi kubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ya kukisambaratisha Chama cha CHADEMA, na kwa sasa ameweka wazi kwa mara nyingine kuwa atakwenda kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara kupitia chama hicho.

Waitara amesisitiza kuwa haondoki Ukonga kwa sababu anamkimbia mtu, bali amekamilisha kazi ya kukisambaratisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hivyo anakwenda Tarime Vijijini ambako ndipo anapotokea, kufanya kazi hiyo.

“Wala hakuna mtu ninayemkimbia, jimbo langu [Ukonga] lipo salama ndani na nje ya chama. Nimeshafanya kazi ya kuwasambaratisha CHADEMA hapa wameshapoteana. Walikuwa na Meya wa Jiji, hayupo, walikuwa na Meya Ilala, hayupo, walikuwa na Meya wa Ubungo, hayupo. Nishamaliza kazi Dar es Salaam, naenda kukamilisha kazi sehemu nyingine,” amesema Waitara.

Kiongozi huyo ambaye alihamia CCM akitokea CHADEMA Julai 2018 amesema kuwa Julai 14 mwaka huu atachukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, na kwamba suala hilo sio siri.
Mwambie Mvimba Macho kwamba habari zake tunazo zile Vault alizofungua GOGOKI kwamba Dally Kimoko!!
 
Tunataka maendeleo sijui Chadema ccm ushu.z.i gani mwambie m/kiti wenu.
 
Kama Mwanza walimkosa kosa kipigo, Tarime watamkamua kinyesi kabisa.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa mpaka sasa hivi amekwishamaliza kazi kubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ya kukisambaratisha Chama cha CHADEMA, na kwa sasa ameweka wazi kwa mara nyingine kuwa atakwenda kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara kupitia chama hicho.

Waitara amesisitiza kuwa haondoki Ukonga kwa sababu anamkimbia mtu, bali amekamilisha kazi ya kukisambaratisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hivyo anakwenda Tarime Vijijini ambako ndipo anapotokea, kufanya kazi hiyo.

“Wala hakuna mtu ninayemkimbia, jimbo langu [Ukonga] lipo salama ndani na nje ya chama. Nimeshafanya kazi ya kuwasambaratisha CHADEMA hapa wameshapoteana. Walikuwa na Meya wa Jiji, hayupo, walikuwa na Meya Ilala, hayupo, walikuwa na Meya wa Ubungo, hayupo. Nishamaliza kazi Dar es Salaam, naenda kukamilisha kazi sehemu nyingine,” amesema Waitara.

Kiongozi huyo ambaye alihamia CCM akitokea CHADEMA Julai 2018 amesema kuwa Julai 14 mwaka huu atachukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, na kwamba suala hilo sio siri.
Na kwa taarifa yenu tutalihami tena Jimbo la Ukonga....
Wana ukonga hututoi CCM...
BRAVOO HAPA KAZI TU!!
 
Uimara wa Heche mnajifurahiasha tuu, hata kupata wenyekiti wa kanda ya Serengeti hakuweza kupata, alipigwa chini na mdada. Kama angekuwa maarufu kiasi hicho mnachosema asinge pigwa chini katika nafasi ya Uenyekiti wa kanda ya Serengeti, hicho kitu kisingetokea. amkeni amkeni.
Nina wasiwasi wako na uelewa wako. Mimi huwa sina chama na si shabikii ujinga. Nimesema alichokifanya waitara ni kuwanyima fursa wananchi kwa kuaribu au kutengeneza mazingira ya wawakilishi wa wananchi ambao wanatokea upinzani kushindwa kufanyakazi. Na hilo kajinasibu yeye mwenyewe. Kimuonekano atasema kawakomoa wapinzani ila kiuhalisia katukomoa wananchi. Hata wanao mkwamisha magu nao akili zao ni kama za Waitara tu coz wanatukoa wananchi wote. Kwa akili zako, kama kuna mradi wa maji katika sehemu ya upinzani then Waitara anaukwamisha, unahisi kamkomoa kiongozi au akina mama wenzio wanao amka usiku kutafuta maji?
Amka wewe, acha ushabiki maandazi, simama kama mtanzania na sio kama cdm au ccm. Hizo akili zenu za uchama, zitabomoa hii nchi.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom