Waitara: Mwenye mamlaka na fedha za mfuko wa Jimbo ni DC pamoja na DED na si Mbunge

Sijui kama nauliza swali kwa mtu sahihi kwa maana hata yeye inamhusu, lakini kwa kuwa anasifiwa na wagema kwamba tembo liko mulua, ningependa kujua na wanaNchi wajue, nini yalikuwa malengo ya mfuko huo, na mbona kila mbunge anautumia kama mali yake na ni lini tutapewa aodit ya fedha hiyo na impact yake, mbona ina nmna furani ya ufisadi wa fedha ya umma.

Kabla hamjaondoka Mjengoni muliangalie kama halina maslahi mapana kwa Taifa futeni ziende Tamisemi moja kwa Moja kwa mkurugenzi. Ndugai nisamehe kama nitakuwa nimechobya mkono kwenye tundu la siafu.
 
Sheria inasemaje? hebu tusaidie tafadhali...

Maswala ya Mfuko wa Kuchochea maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi yanaongozwa na sheria Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi, 2009 ambayo ni sheria Na. 16 ya 2009 ambayo pia inaweza kufanyiwa rejea kama Sura Na. 96 Toleo la 2015. Sheria hii kwa Kiingereza inaitwa the Constituencies Development Catalyst Fund, 2009. Pia, maswala haya yanaongozwa na Kanuni za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi, 2010 yaani the Constituencies Citation Development Catalyst Fund Regulations, 2010 ambazo ni Tangazo la Serikali Na. 37 la 2010.

Masharti ya Kifungu cha 7 na 11 cha Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi, 2009 yanaelekeza kuwa mamlaka ya kuidhinisha miradi ya maendeleo katika jimbo la uchaguzi na pesa za kuendesha miradi hiyo yako mikononi mwa Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi (the Constituencies Development Catalyst Committee). Mbunge ndio mwenyekiti wa Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria Na. 16 ya 2009.

kwa mujibu wa Kifungu cha 10 (1) cha Sheria Na. 16 ya 2009, Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi inaundwa na wajumbe wafuatao;

(a) Mbunge wa jimbo wa kuchaguliwa (Mwenyekiti)
(b) Afisa Mipango wa Wilaya (Katibu)
(c) Madiwani 2 (kutoka katika jimbo la uchaguzi husika)
(d) Makatibu Kata 2
(e) Mwakilishi wa Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO)

Hivyo basi, Mkuu wa Wilaya hausiki popote katika kufanya maamuzi ya kisera na wa kiuendeshaji wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi isipokuwa Mkurugunzi wa Halmashauri ambaye anahusika kama Afisa Masuhuli (Accounting Officer) wa mfumo na mtia saini (signatory) kwenye account za benki za mfuko kwa mujibu wa Kifungu cha 21 (2) na 22 (3) (a) (i) cha Sheria Na. 1 ya 2009 vikisomeka pamoja na Kanuni ya 4 (3) na 6 ya Tangazo la Serikali Na. 37 la 2010. Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na kuwa Accounting Officer na Signatory bado hana kabisa mamlaka ya kuidhinisha (approve) miradi na pesa za mfuko maendeleo tajwa bali mamlaka hayo yako mikononi mwa Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi.
 
Back
Top Bottom