Waitara: Mwenye mamlaka na fedha za mfuko wa Jimbo ni DC pamoja na DED na si Mbunge

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,550
Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara amemwagiza Mkuu wa Wilaya (DC) ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya kutumia Sh42 milioni za mfuko wa jimbo hilo ambazo zimekaa kwa miaka miwili bila kutumika.

Waitara amesema fedha hizo zilitolewa mwaka wa fedha 2018/19 ambazo hadi sasa hazijapangiwa matumizi yoyote kinyume na taratibu za matumizi ya fedha hizo.

Maagizo hayo aliyatoa jana Jumatano Januari 8, 2020 wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai pamoja na wananchi wa kijiji cha Longoi alipokwenda kutembelea ujenzi wa kituo cha afya.

Alisema fedha hizo ni kwaajili ya kuchochea miradi ya maendeleo. Jimbo la Hai linaongozwa na Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Katika mazungumzo yake, Waitara alisema, "mwenye mamlaka ya kupangia fedha za mfuko ni DC na mkurugenzi na sio mbunge kama anavyofanya mbuge wa Jimbo hili Freeman Mbowe."

Alisema fedha hizo zilitakiwa zitumike tangu mwaka 2019 hadi sasa hazijatumika hivyo ni kosa na kwamba kwa kutumia mamlaka aliyonayo amemtaka Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kutawanya fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo vijijini.

"DC mwagize mkurugenzi atawanye fedha hizo, wananchi watume maombi na DC uzisimamie zitumike kwenye matumizi yanayotakiwa," alisema Waitara.

Aidha alisema Mbowe hana mamlaka ya kupanga matumizi ya fedha hizo bali anatakiwa kuchukua matatizo ya wananchi na kuyawasilisha bungeni.

Alisema Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema amekuwa mtoro wa kufanya kazi za wananchi na badala yake amekuwa akifanya matumizi ya fedha hizo kwa njia ya simu jambo ambalo sio sahihi.

"Sabaya ndie Mkuu wa Wilaya ya Hai na ndiyo mwenye mamlaka ya kuamua nini kifanyike ndani ya wilaya hii," alisema Waitara aliyewahi kuwa Chadema kabla ya kujiuzulu na kutimia CCM.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya alisema endapo mtu yoyote atafanya matumizi mabaya ya fedha za wananchi atamfyatua na kumtupilia mbali baada ya kupewa nguvu hiyo na naibu waziri huyo.

"Mheshimiwa naibu waziri kituo hiki cha afya ulicho kitembelea leo ni jitihada za kuhakikisha wananchi wa ukanda huu wa tambarare wanakumbukwa katika shughuli za maendeleo na tayari mpaka sasa kiasi cha Sh338 milioni zimechangwa kutoka vyama vya ushirika na wananchi na fedha hizo zipo katika akaunti iliyo funguliwa," alisema Sabaya.

Aidha Sabaya alimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha ndani ya wiki moja wananchi wanatuma maombi ya matumizi ya fedha hizo na zigawanywe kwa kufuata sheria za matumizi ya fedha hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kwenye Jimbo lake la Ukonga , alishatembelea na kuona changamoto za Ubovu wa barabara zinazowakabili wapiga kura wake.
Na amechukua hatua zipi kumpa maagizo Mkuu wa Wilaya kuhusu pesa za Jimbo ili kutatua tatizo la Barabara Maeneo mbali mbali katika Jimbo lake..?
 
Vipi kwenye Jimbo lake la Ukonga , alishatembelea na kuona changamoto za Ubovu wa barabara zinazowakabili wapiga kura wake.
Na amechukua hatua zipi kumpa maagizo Mkuu wa Wilaya kuhusu pesa za Jimbo ili kutatua tatizo la Barabara Maeneo mbali mbali katika Jimbo lake..?
"Barabara haziwezi kukusaidia chochote, kaa hapo chini unywe bia" By Waitara
 
Ndipo hapo mkae mkijua kuwa sabaya anayoyafanya yana baraka za wakubwa ndio maana ana kiburi cha uzima

Madudu anayofanya Sabaya huko Hai, ni maelekezo ya ALIYEMTEUA,


Vinginevyo angekwisha WAJIBISHWA,


POLENI WANA HAI,


Kule Arusha alikuwa na kesi ya kijifanya TISS, Watu wakapiga kimya, Unyang'anyi aliouita makonda style mwenyewe, hadi clip mtandaoni, wakubwa zake kimya, hawasikii wala hawaoni, hili la pesa za jimbo Waitara katumwa kwenda kumwongezea nguvu.


HAI KAENI MACHO
 
Hivi punde,
Kauli aliyoitoa mh Waziri ni nzuri na inatakiwa itumike kwa Halmashauri na wilaya zote za Tanzania.
Na itumike kwa miaka yote,usije ikatumika kwa Jimbo au wilaya Mija tu ya Hai. Huku Bukombe hiyo kauli haijatumika,tunaomba itumike wananchi tuletewe barabara,maji na umeme,tunateseka kumbe serikali yetu imetuma fedha muda mrefu zinaelekea tu hazitumiki.mh waitara hongera sana
 
Kauli aliyoitoa mh Waziri ni nzuri na inatakiwa itumike kwa Halmashauri na wilaya zote za Tanzania.
Na itumike kwa miaka yote,usije ikatumika kwa Jimbo au wilaya Mija tu ya Hai. Huku Bukombe hiyo kauli haijatumika,tunaomba itumike wananchi tuletewe barabara,maji na umeme,tunateseka kumbe serikali yetu imetuma fedha muda mrefu zinaelekea tu hazitumiki.mh waitara hongera sana

Kama hujang'olewa ubongo, huwezi sifia huu upuuzi.
 
Waziri mdogo ama Mkubwa hana mamlaka hayo aliyojitapa nayo kuwa anayo, huyo mheshimiwa aache kujidanganya; na kama kweli anayo maana yake anatuaminisha kuwa Mkurugenzi na wanasheria wake, pamoja na DC wote ni vilaza kwa kutojua mamlaka ya Waziri ili wayatumie kabla mpaka aje kuwaambia yeye mwenyewe mamlaka yake, hao wanapaswa kuwajibishwa kwa kukaa hapo kizembe huku wanaangalia hela ya wananchi imekaa tu.

Pamoja na hayo, Sheria ya Mfuko wa Jimbo inahitaji marekebisho makubwa hususani kwenye matumizi ya fedha ya Mfuko huo, wabunge wengi wanaitumia vibaya sababu ya mamlaka waliyopewa na hiyo sheria. Wengi wanatoa fedha ma akwa upendeleo ama hawatoi kabisa sababu bila wao ile fedha haiwezi kutoka, na ikitoka inakuwa kinyume na sheria, ni hoja ya ukaguzi. Mbowe aende kutoa hela hiyo itumike kwa faida ya wananchi.
 
Pesa ya jimbo ipo kisheria, DC hakuna sehemu ambayo inampa room ya kugawa fedha ya jimbo. DED ndo mwenyeuwezo wa kumwomba katibu mkuu wizara ya fedha kibali cha kugawa au kuhamisha fedha yoyote ya serikali iliyo chini yake. Mwita naye anatoa maagizo nje ya sheria ya Budget. DC kaanza lini kuwa accounting officer wa Halmashauri
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom