Waitara: Mbowe nipigie simu, sasa mimi ni bosi wako

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,892
22,649
Naibu waziri wa TAMISEMI amemtaka mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ampigie simu ampe malalamiko yake ya kijimbo asione aibu kwa kuwa yeye Mwita kwa sasa ni bosi wake tu.

Kauli hii imekuja baada ya kuzuka mgogoro juu ya mbunge huyo na mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya katika mambo mbalimbali ikiwamo mkuu huyo wa wilaya kudaiwa kuchukua ofisi ya mbunge huyo ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni iliyokuwa katika jengo la uhamiaji wilayani Hai.

Inadaiwa Mbowe amekuwa akilalamika mitaani bila kufikisha malalamiko wizarani husika kwa kuona aibu kuwa Naibu Waziri huyo sasa ni bosi wake na Mbowe alimtishia kwa dharau wakati akiwa Chadema

Inadaiwa mgogoro wa DC Sabaya na Mbowe unazidi kukua tangu DC huyo kuonekana mchapakazi sana jimboni na kumfunika Mbowe ambaye huishi Dar es Salaam na kwenda jimboni Mara chache

'Namuomba Mbowe asilalamike mitaani na wala asione aibu kinipigia maana Mimi ndio bosi wa Ole Sabaya na pia ninayodhama na wilaya ya Hai' alisema Naibu Waziri, Mwita Waitara

USSR
Screenshot_20191231-001812.jpeg
 
USSR,
Hakuna mahali popote ambapo Bilionea Mbowe amelalamika , wanaolalamika ni wadau , lingine unalotakiwa kulifahamu ni hili , Tajiri Freeman Mbowe hatahangaika na mtu masikini kama Sabaya , ukiachana na ukweli kwamba Baba yake Mbowe ndiye aliyempatia nauli Nyerere kwenda UNO kudai uhuru huu mnaotumia kunyanyasa wengine zikiwemo koo zilizotoa nauli ya kuutafuta , Mbowe mwenyewe ndiye aliyemnunulia suruali za heshima Waitara alipokimbia Uvccm baada ya kuambiwa awe anampikia chai Nchimbi ( kama waitara anabisha ajitokeze ) Mbowe ndiye alimnunulia pikipiki Waitara alipokuwa anagombea uenyekiti wa kijiji cha kivule huko matembele , pikipiki ambayo hata hivyo iliibiwa kutoka na ulevi wa Waitara .

Kama anazo akili timamu , Waitara hatakiwi kumdhihaki Mbowe kwa namna yeyote ile , Mbowe ndio alimnusuru alipotaka kutimuliwa Chadema mithili ya paka aliyekunywa maziwa ya mtoto .

..... iko siku nitaweka uzi kuhusiana na hili .
 
Back
Top Bottom