Waitara: CHADEMA inapokea ruzuku ya sh 329 milioni kila mwezi, Dr Mashinji analipwa mshahara sh 7mil kwa mwezi!

Katika mahojihano na 360 ya clouds fm, aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mheshimiwa Mwita Waitara amesema

Kila anayeitaka nafasi ya uenyekiti ndani ya CHADEMA lazima apotee au afukuzwe,

Kaeleza kwamba professor ....' alimuita akamueleza kwamba "Mbowe hakutaki hapa anaongea mpaka anapanda juu ya meza kuonesha msisitizo kwamba huitajiki"

Akasema au unataka yakutokee ya wangwe au ya wengine?

Maana mpaka Leo suala la risasi za Lissu kuna mkanganyiko mara kushoto mara kulia, na mara hatutaki dereva ahojiwe,

Kauli hiyo imenipa wasi wasi sana

Wewe ulitaka alipwe shilingi ngapi?Je katibu wa chama chako kikongwe analipwa shilingi ngapi?Je mbunge analipwa shilingi ngapi ukilinganisha na mwalimu?Brother huna hoja zilizoenda shule bali unaropoka tu.
Mshahara wa Dr Mashinji ni 2% ya ruzuku yote ya Chadema!
 
Aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara yupo mubashara Clouds 360 anaelezea jinsi ruzuku ya chama inavyofisadiwa.

Mwita anadai mbunge wa Tarime John Heche alipokuwa mwenyekiti wa Bavicha alikuwa analipwa mshahara sh 1.5 mil kila mwezi kinyume cha utaratibu.

Anadai wabunge wa viti maalumu ndio mtaji wa Mbowe pale CHADEMA.

Anadai yeye ndio mbunge bora wa jiji la Dsm, amejenga madaraja na hospitali pale Chanika na kwamba wakati wa mafuriko wapiga kura wake huja nyumbani kwake kupata hifadhi.

Kadhalika anadai ameondoka Chadema baada ya Mbowe na Dr Mahanga kumhakikishia kuwa hataitishwa kugombea tena 2020.

Mwita anadai mwaka 2008 alihama CCM na kwenda Chadema baada ya kugombana na aliyekuwa Katibu mkuu mzee Makamba na yule mwenyekiti wa UVCCM Dr Nchimbi.

Amesisitiza kuwa amejiuzulu ubunge muda huu baada ya kuona kuna fursa ya yeye kurudi tena bungeni katika uchaguzi mdogo kwa tiketi ya CCM hivyo hakuna atakachopoteza. Pia amedai yeye hakuutaka uenyekiti bali alitamani sana Mwenyekiti wa chama taifa awe Tundu Antipas Lissu.

Amemaliza kwa kusema ameshachukua fomu ya kugombea tena ubunge wa Ukonga na kwamba katika mazingira ya kisiasa akitokewa na baya lolote atamhisi Mbowe!

Source: Clouds tv!

Hakuna alichopoteza? Hiyo hela ya marudio ya walipa kodi si ingeenda kununua dawa?
 
Kumbe anaogopa kufa," hahahaha, nikipatwa na baya nitamhisi mbowe" ashukuru mungu tu nimeokoka, hao wanao hamahama ingekuwa zile zama zangu mngesikia hao wanao hamahama , nimeshawtia ulemavu
 
Katika mahojihano na 360 ya clouds fm, aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mheshimiwa Mwita Waitara amesema

Kila anayeitaka nafasi ya uenyekiti ndani ya CHADEMA lazima apotee au afukuzwe,

Kaeleza kwamba professor ....' alimuita akamueleza kwamba "Mbowe hakutaki hapa anaongea mpaka anapanda juu ya meza kuonesha msisitizo kwamba huitajiki"

Akasema au unataka yakutokee ya wangwe au ya wengine?

Maana mpaka Leo suala la risasi za Lissu kuna mkanganyiko mara kushoto mara kulia, na mara hatutaki dereva ahojiwe,

Kauli hiyo imenipa wasi wasi sana

Huu ndio ukweli mchungu mkuu. Muda utaongea wakati utakapofika. Kuna mengi sana yanaendelea katika hilo "Genge" la Mwenyekiti. Waitara anaongea yale ambayo wengi wao hata Lissu anatamani lakini anaogopa kutamka hadharani. Ila mioyo yao imekinai Mwenyekiti na GENGE lake.
NB: Mods kwa nini mmeunganisha huu Uzi wa britanicca ?
 
Kumbe anaogopa kufa," hahahaha, nikipatwa na baya nitamhisi mbowe" ashukuru mungu tu nimeokoka, hao wanao hamahama ingekuwa zile zama zangu mngesikia hao wanao hamahama , nimeshawtia ulemavu
Wewe huogopi Kufa?
JF tu unatumia fake ID kwa uwoga wako...huko mtaani si utakuwa unavaa hijab na niqab kabisa!
 
Huyu Waitara ni mkurya wa town si wa kule nyumbani, hakuna mura mnafiki wa hivyo. Na Waitara anajua CDM ndiyo wamemfikisha hapo alipo. Hakutakiwa kuropoka kiasi hicho. Ajiulize makatibu wengine wamekuwa wakilipwa Je?! eg Bashiru, Slaa, Kinana etc. Yeye akomae na CCM yake cdm hapamfai tena .
Mtatiro nae si mkurya, yani wakurya wamekuwa watu wa ovyo sana
 
Milion 329 kwa mwezi
Bilion 3.5 kwa mwaka
Bilion 40 kwa miaka mitano
Bado CHADEMA hawana ofisi za chama wala kupeleka hela majimboni?
5% ya ruzuku kwa miaka mitano ingeweza kujenga ofidi ya kisasa sana CHADEMA
15% ya ruzuku kwa miaka mitano ingepelekwa majimboni chama kingeimarisha sana
lkn 100% zinabaki Dar wanagawana hawa akina Mbowe na wenzake kwa njia za mishahara!
CHADEMA ni chama cha ajabu kabisa na KISIPEWE dola na wananchi
Ni wapigaji tu hawa hawana lolote!!
 
Hahahaa....... Chadema ni kama kijiwe!
 
Back
Top Bottom