Hao wameingizwa kwenye mtego wa panyaIla hawa Wapinzani Wanaohama na kugombea tena kwa tiketi ya Ccm Sidhani kama Watapata nafasi ya kupitishwa tena Mwaka 2020 Sidhani.
Ina maana ccm wamesha muahakikishia kurudi bungeni wala hata sio wananchi wapiga kura.Jamaa anaropoka sana hadi ccm wanaweza kumpiga chini..
"Nilihama ccm sababu nilikorofishana na Makamba na Nchimbi" ameshau Makamba na Nchimbi bado wapo ndani ya ccm.
"Nimehamia ccm baada ya kuona sina cha kupoteza maana nitarudi tena bungeni"
Hizi kauli zinaweza kumgharimu ndani ya ccm.!
Ni mkurya was Kwanza asiyekuwa na msimamo. Mkurya was Kwanza mwenye tamaa ya fedha ambaye anajijali yeye KULIKO wengine. Anasema KUWA wanagongolamboto wanaenda kuomba au kukaa kwake kujiifadhi. Kama siyo kuwadhalilisha wanagongolamboto Ni nn anaouwezo gani was kuifadhi hata zaidi ya watu 20. Amekimbilia ccm baada ya kuona hatagombea ubunge na yy alivyo bila ubunge haweziishi. Sijawahi kuona mkurya mwenye njaa Kama huyu. Tangu amehama Ni chadema tu Hana jipya. Tutaona mwisho wakeAliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara yupo mubashara Clouds 360 anaelezea jinsi ruzuku ya chama inavyofisadiwa.
Mwita anadai mbunge wa Tarime John Heche alipokuwa mwenyekiti wa Bavicha alikuwa analipwa mshahara sh 1.5 mil kila mwezi kinyume cha utaratibu.
Anadai wabunge wa viti maalumu ndio mtaji wa Mbowe pale CHADEMA.
Anadai yeye ndio mbunge bora wa jiji la Dsm, amejenga madaraja na hospitali pale Chanika na kwamba wakati wa mafuriko wapiga kura wake huja nyumbani kwake kupata hifadhi.
Kadhalika anadai ameondoka Chadema baada ya Mbowe na Dr Mahanga kumhakikishia kuwa hataitishwa kugombea tena 2020.
Mwita anadai mwaka 2008 alihama CCM na kwenda Chadema baada ya kugombana na aliyekuwa Katibu mkuu mzee Makamba na yule mwenyekiti wa UVCCM Dr Nchimbi.
Amesisitiza kuwa amejiuzulu ubunge muda huu baada ya kuona kuna fursa ya yeye kurudi tena bungeni katika uchaguzi mdogo kwa tiketi ya CCM hivyo hakuna atakachopoteza. Pia amedai yeye hakuutaka uenyekiti bali alitamani sana Mwenyekiti wa chama taifa awe Tundu Antipas Lissu.
Amemaliza kwa kusema ameshachukua fomu ya kugombea tena ubunge wa Ukonga na kwamba katika mazingira ya kisiasa akitokewa na baya lolote atamhisi Mbowe!
Source: Clouds tv!