Waitara awashukia vikali Mawaziri. Zungu amjibu hata yeye alikuwa anafanya hivyo hivyo alipokuwa Naibu Waziri

Leo mbunge Waitara amewashukia naibu Waziri maliasili na Waziri wa ardhi na kuwalaumu kumtegea mabomu njiani. Waitara amesema wahusika wameenda jimboni kwake na kudai wamemshirikisha eneo la mipaka na kuwahamisha watu bonde la mto Msimbazi.

Waitara amewataka mawaziri wa Maliasili na Ardhi waende mkoa wa Mara kwani hawawezi kwenda peke yao na kuwapa wananchi wake taarifa za uongo, Waitara amesisitiza watagombana.

Mwisho amesema amewekewa bomu ambalo hatakubali kulipuka peke yake bali watalipuka wote.

Kuhusu ripoti ya Jaffo, amesema walishaandikiana sana na mgodi lakini ripoti ya Jaffo imeharibu hali ya hewa.

Akimjibu, Naibu spika wa Bunge, Mussa Zungu amenena
Mussa Zungu: Asante mheshimiwa Waitara lakini wewe ulikuwa naibu Waziri wa mazingira na ulikuwa unakwenda kwenye migodi wala wabunge wenzio huwaambii, na umemaliza ukaenda huko uchukuzi, unaenda huko unakagua lakini huwaambii lakini hoja yako ni ya msingi.

Kwa mawaziri mkienda huko muambizane lakini habari ndio hiyo.
Zungu apumzike Sasa.
 
Pumbavu kipindi Ndungai anaingilia mijadala ya bunge hai 2015-19 mlikuwa mnashangilia!! Saizi mnaona umuhimu wa mijadala HURU?.
Waliokuwa wakifurahia pindi wenzio walipokuwa wakishushiwa vitu vizuto kichwani, Sasa zamu yao imefika wanalia Lia.😜
 
Nasikia wanatokaga na bahasha nono kweli kweli
Ulichosema ni kweli tupu. Toka Enzi hizo wabunge wote wanapiga sana kelele kuhusu mgodi huyo. Lakini wakikodiwa ndege na kwenda kuutembelea huo mgodi, wakirudi utakuta kimyaaaa utafikiri siyo wale waliokuwa wanatoa povu.
Hata hii tume ya Mayelle imefuata mule mule.
 
Nanukuu " Wizi wa Kura unasababisha Wizi mwingine kukua mfano tutakutana na Wizi wa mitihani,Mali za umma,Bandalini,madawa,Ajira ..."

Hiyo nukuu inahitaji tafakuri kubwa vinginevyo wacha tuishi tu.
 
Hii nchi tunaenda utafikiri hakuna watu wapya wa kushika nyazifa,, kila siku majina ni yale yale,, vyeo vilevile,, upigaji uleule,,wajinga ni walewale..

Nothing changes
 
Zungu alishapitwa na wakati.
si ndo mbunge wa Ilala huyu au...ila pale Ilala maghorofani ...asee wanampendaaa lazima sasa hivi yuko paleee bar ya Maghorofani anakula urabu....... sijui kwa nini!...anapenda!...na

wapambe wa Ilala wale hawanaga dogo wanamzungukaga hao!...heee!
 
Back
Top Bottom