Waitara atoa agizo ma Afisa elimu waanze kuwa na vipindi darasani.

Ha ha ha ha ha ulevi bwana dah! Kuna siku Mh Rais nae atapangiwa vipi vya kemia UDSM.
 
Daah!! Hatari sana nilienda kutembea nyumbani kidogo nikakuta afisa elimu wa wilaya yetu kapelekwa shule moja huko vijijini akafundishe sasa sijui atafuatiliaje matatizo ya shule zingine ikiwa yeye mwenyewe tayari anawajibu wa kuingia darasani kila siku
 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) anayesimamia sekta ya elimu Mwita Waitara leo April 6.2019 ametoa maagizo kwa maafisa elimu wote kuwa na vipindi vya kufundisha katika shule zilizopo maeneo yao kwa kuwa hiyo ndio taaluma yao.

Agizo hilo amelitoa leo alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Michezo kwa wanafunzi wa shule za Sekondari [UMMISETA] ambayo kitaifa mwaka huu wa 2019 yamezinduliwa katika mkoa wa Manyara.
____________________________________

Aisee yaani ,ujue katika uongozi kuna kitu kinaitwa Functional departmentalization ,kwamba kila mtu ana majukumu yake na kazi zake katika eneo lake , Afisa elimu kata ni msimamizi elimu kata,Afisa elimu wilaya yeye husimamia elimu wilaya,Afisa elimu mkoa husimamia elimu mkoa hawa watu wana majukumu yao haya,tusiwape mzigo mwingine.

Kuna walimu wakuu huwa hawafundishi wapo wengi tuu na wapo shule nyingi mbona hawambii ? ,Na sasa kama Mkuu wa shule hafundishi yupo busy kusimamia shule , vipi kuhusu Afisa elimu wa kata,wilaya na mkoa ambao wanapaswa simamia shule zote ndani ya maeneo yao.

Sasa ndio kusema OCD na RPC wapangiwe lindo siku moja moja sababu na wao ndio taaluma yao ya upolisi ?

Mbona Tanzania tumejaaliwa kuwa na walimu wengi walio hitimu na wapo nyumbani tuu bila ajira ,kama kuna upungufu tuwaajiri ili kuongeza ufanisi.

Sent using Jamii Forums mobile app


UKUMBUKE WALISHARUHUSIWA KUVUTA BANGI KWA SIRI ILI WAWE WAKALI.

Kwahiyo HUENDA alilivuta akazidisha kipimo chake akajikuta anaropoka Hivyo.

Kwahiyo usishangae Wa Afya naye akawataka waganga Wakuu wa wilaya waingie thieta, RPC ajipangie lindo la kulinda, OCD apangiwe lindo la kulinda Kama NI benk ya NMB AU CRDB ILI MRADI AWE NA LINDO MAANA HIYO NDIYO TAALUMA YAO.

UJINGA HASARA SANA.
 
Naipinga serikali hii kwa namna nyingi sana, ila hoja hii naiunga mkono.

Kama wanauwezo wa kufundisha na muda upo waende wakafundishe, na hao walimu wakuu wafundishe pia na mtanzania yeyote anayeweza kujitolea uwekwe utaratibu iwezekane kufundisha.

Swala la elimu ni la kufa na kupona,
Hii ni too low kwako Mkuu
 
Back
Top Bottom